Wednesday, June 29, 2011

Mwanamke wa kwanza kuongoza IMF

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Christine Lagarde ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF. Waziri wa Fedha wa Ufaransa Christine Lagarde ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF.Kufuatia uteuzi huo Ufaransa itakuwa imeshikilia kiti hicho kwa miaka 26 kati ya miaka 33 iliyopita.


Christine Lagarde mwenye umri wa miaka 55, alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa waziri wa fedha katika muugano wa nchi saba zilizostawi maarufu kama G-7.

Lagade anatarajiwa kujiuzulu kutoka serikali ya Ufaransa ili kuandikisha historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuongoza shirika la fedha duniani IMF.


Uteuzi wake umefuatia kujiuzulu wa mfaransa mwenzake Dominique Strauss Kahn, baada ya kukabiliwa na kashfa ya ubakaji.
Sio wengi walioshangazwa na uteuzi wa wakili huyo wa zamani ambaye ana sifa nzuri kote duniani.

Amekuwa msuluhishi wa matatizo mengi ya kiuchumi yanayokumba mataifa kadhaa barani ulaya katika miaka ya hivi karibuni.


Kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa ameungwa mkono na China na India na hivyo kuteuliwa kwake kama mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la fedha duniani ilikuwa jambo lililotarajiwa.

Kuna maelewano ambayo hayajanakiliwa kuwa raia wa mataifa ya bara ulaya pekee ndio wanaopaswa kuteuliwa kuhudumu kama mkurugenzi mkuu wa IMF huku raia wa marekani wakipewa nafasi za kuongoza benki kuu ya dunia.
Mataifa yaliostawi yanataka kupewa nafasi kuu katika siasa za dunia, lakini huu ni wakati mgumu kwa mataifa ya ulaya huku mzozo wa kiuchumi wa Ugiriki ukitishia kuathiri mataifa mengine katika kanda hiyo.


Muungano wa ulaya na IMF zimeishurutisha serikali ya Ugiriki kupunguza matumizi yake ili kuendelea kupata msaada kutoka kwao.

Lagarde amekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kutatua matatizo hayo ya nchi wanachama wa EU.BBC

No comments: