Tuesday, June 7, 2011
Mchungaji wa KKKT afungwa jela miaka 6 kwa jaribio la kumbaka mwanafunzi
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka sita jela mwalimu wa shule ya sekondari ya Pomerini wilaya ya Kilolo mkoani hapa Michael Ngilangwa ambaye ni mchungaji wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Njombe kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake.
Mahakama hiyo chini ya hakimu Martha Mpaze imetoa hukumu hiyo juzi baada ya mwalimu huyo kupatikana na hatia katika mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili katika kesi iliyofunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) mkoa wa Iringa alisema kuwa mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakani hapo hivyo ili imetoa adhabu hiyo kwa mchungaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine.
Alisema katika kosa la kwanza mwalimu huyo anadaiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake huyo jina (limehifadhiwa) ili kumsaidia masomo ambapo adhabu yake ni kulipa faini ya shilingi laki tano ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, na kosa la pili ni kutaka kumbaka mwanafunzi huyo ambapo mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miaka mitano.(Imeandikwa na Francis Godwin kutoka Iringa)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment