Monday, June 1, 2009

Umasikini wetu nguzo ya mafisadi

MWANAHISABATI, mtunzi wa vitabu na mpiga picha raia wa Uingereza, Lewis Carroll, aliyezaliwa mwaka 1832 na kufariki 1898, aliwahi kuandika maelezo yenye mantiki na nguvu za hoja hata katika ulimwengu wa leo.

Carroll, enzi za uhai wake, aliandika akihimiza umuhimu wa kufanya jambo lenye mantiki kwa wakati uliopo. Alizungumzia mazingira hayo ya uhimizaji kwa kuandika; “The rule is, jam tomorrow and jam yesterday - but never jam today.”

Mantiki au ujumbe uliomo katika maandishi hayo ya Carroll ndiyo tunayoweza kuyatumia katika kuthibitisha kuwa viongozi wakuu wa kitaifa, wanayumba.

Kuyumba kwa viongozi hao wakuu, wakiwamo wa vyombo vya usalama ni dhahiri. Lakini kikubwa cha kujiuliza na cha kutia shaka ni swali kwamba, je, kuyumba huko kutafikia kiwango gani na athari zake zitabomoa kwa kiasi gani taifa.

Je, Taifa linaweza kubomoka katika kipengele cha demokrasia pekee na maeneo mengine yakabaki salama? Au Taifa linabomoka katika kipengele cha maadili ya viongozi pekee na sehemu iliyobaki ya jamii ikawa salama? Au Taifa linabomoka kwa ujumla wake?

Leo nijadili hali hiyo kwa kutazama kipegele cha demokrasia na hususan haki ya kuchagua na kuchaguliwa, wengine hutafsiri kuwa haki ya kupiga na kupigiwa kura, na zaidi nitaangalia kile kinachowezwa kuitwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, mwakani, hususan nafasi za ubunge.

Kimsingi, pamoja na upungufu mwingi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, bado suala la kuchagua na kuchaguliwa limepewa nafasi katika Katiba.

Kwa kadiri tunavyosogelea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, zipo dalili za wazi kuwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wenye mabilioni haramu wamefanikiwa kuwayumbisha viongozi waandamizi nchini pamoja na mfumo wa usalama wa nchi.

Tumeanza kupata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba watuhumiwa hao wa ufisadi wamejipanga, wameamua kuwekeza mabilioni yao kwa lengo la kupanga safu za viongozi wanaowataka, na hasa ngazi ya ubunge.

Kwanza tujiulize, kwa nini walenge ngazi hiyo, badala ya madiwani au nafasi nyingine kama wenyeviti wa vijiji? Sababu zipo nyingine, mojawapo ni ukweli kwamba mbunge ni mtu muhimu kwa wafanyabiashara wakubwa.

Soma zaidi

No comments: