Monday, November 1, 2010

Kikwete, Dk. Slaa ni mchuano mkali

-Arusha Mjini, Mbeya Moshi Mjini Iringa moto
-Dar es Salaam, Arumeru nako mambo mazito
-Upigaji kura wafanyika kwa amani na utulivu

Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini kote yalianza kutangazwa jana jioni katika vituo kadhaa vya kupigia kura huku mchuano mkali ukiwa kati ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, na mgombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.

ARUSHA

Katika Jimbo la Arusha Mjini matokeo ya baadhi ya vituo vya Kata ya Kaloleni yalionyesha kuwa:

Kituo ‘A’

Urais: Kikwete 59, Dk. Slaa 112, Lipumba 4.

Ubunge: Burian CCM , Chadema 113, TLP 1.

Udiwani: CCM 52, Chadema 105, TLP 0.



KITUO A 2

Urais: Kikwete 76, Dk. Slaa 116, TLP 0.

Ubunge: CCM 71, Chadema 120, TLP 2.

Udiwani: CCM 70, Chadema 108, TLP 0.

Kituo A 3

Urais: Kikwete 67, Dk. Slaa 104, Lipumba 1.

Ubunge: 62, Lema 109, TLP 2.

Udiwani CCM 67, Chadema 97, TLP 2.

Kituo D 1

Urais: Kikwete 67, Dk. Slaa 118, Lipumba 5.

Ubunge: CCM 61, Chadema 121, CUF 3. TLP 4

Udiwani: CCM 57, Chadema 111, CUF 14, TLP 24.

Kituo D 2

Urais: Kikwete 64, Dk. Slaa 102, CUF 1, TLP 0.

Ubunge: CCM 64, Chadema 69, CUF 2, TLP 2.

Udiwani: CCM 60, Chadema 91, CUF 10, TLP 2.

Kituo D 3

Urais: Kikwete 50, Dk. Slaa 92, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 48, Chadema 90, CUF 1, TLP 0.

Udiwani: CCM 43, Chadema 89, CUF 6, TLP 0.

Kituo D 4

Urais: Kikwete 67, Dk. Slaa 87, CUF 3.

Ubunge: CCM 68, Chadema 87, TLP 2.

Udiwani: CCM 63, Chadema 84, CUF 6.

ARUMERU MAGHARIBI

Matokeo kamili ni kama ifuatavyo:

Kituo namba 1

Urais: Dk. Slaa 122, Kikwete 74.

Ubunge: Chadema 106, CCM 91

Udiwani: Chadema 126, Marunda 70.

Kituo namba 2:

Urais: Dk. Slaa 135, Kikwete 47.

Ubunge: Chadema 108, CCM 71.

Udiwani: Chadema 123, CCM 57.

Kituo namba 3.

Urais: Dk. Slaa 144, Kikwete 65

Ubunge: Chadema 129, CCM 79

Udiwani Kendo 148, Marunda 62.

Kituo namba 4:

Dk. Slaa 132, Kikwete 51.

UBUNGE:

Kisambu Chadema, CCM 71

UDIWANI:

Chadema 126, CCM 57.

Kituo namba 5.

Urais:Dk. Slaa 116, Kikwete 50

Ubunge:Kisambu Chadema, CCM 72

UDIWANI

Chadema 113, CCM 55

Kituo namba 6:

Urais:Dk. Slaa 161, Kikwete 62.

Ubinge:Chadema 87, CCM 79

Udiwani:Chadema 101, CCM 65

DODOMA

Katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Kata ya Viwandani

Kituo 1

Urais: Kikwete 95, Dk. Slaa 59, Lipumba 6.

Ubunge: CCM 101, Chadema 50, CUF 6.

Kituo 2

Urais: Kikwete 103, Slaa 55, Lipumba 3.

Ubunge: CCM 105, Chadema 48, CUF 4.

Kituo 3

Urais: Kikwete 94, Slaa 55, Lipumba 6.

Ubunge: CCM 93, Chadema 48, CUF 6.

Kituo 4

Urais: Kikwete 101, Slaa 49, CUF 5.

Ubunge: CCM 105, Chadema 41, CUF 8.

Kituo cha Uhindini 1

Urais: Kikwete 62, Slaa 46, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 69, Chadema 33, CUF 5.

Uhindini 2

Urais: Kikwete 59, Slaa 45, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 60, Chadema 34, CUF 1.

Makulu 1

Urais: Kikwete 85, Slaa 70, Lipumba 1.

Ubunge: CCM 74, Chadema 77, CUF 3.

Udiwani: CCM 48, Chadema 110.

Makulu 2

Urais: Kikwete 89, Slaa 72, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 79, Chadema 81, CUF 1.

Udiwani: CCM 51, Chadema 112.

Mukala 1

Urais: Kikwete 73, Slaa 70, Lipumba 1.

Ubunge: CCM 52, Chadema 90, CUF 3.

Udiwani: CCM 38, Chadema 107.

Makalamo 2

Urais: Kikwete 81, Slaa 86, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 60, Chadema 105, CUF 3.

Udiwani: CCM 37, Chadema 130.

Msangalale 1

Urais: Kikwete 111, Slaa 60, Lipumba 1.

Ubunge: CCM 93, Chadema 78, CUF 0.

Udiwani: CCM 52, Chadema 121.

NYERERE

Urais: Kikwete 67, Slaa 55, Lipumba 3.

Ubunge: CCM 70, Chadema 47, CUF 5.

Udiwani: CCM 64, Chadema 58.

POLISI ZAHANATI

Urais: Kikwete 73, Slaa 58, Lipumba 3.

Ubunge: CCM 77, Chadema 52, CUF 4.

Udiwani: CCM 71, Chadema 62.

OFISI YA WEO

Urais: Kikwete 62, Slaa 55, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 70, Chadema 41, CUF 4.

Udiwani: CCM 59, Chadema 54.

Ofisi ya WEO 2

Urais: Kikwete 69, Slaa 39, Lipumba 0.

Ubunge: CCM 76, Chadema 29, CUF 1.

Udiwani: CCM 66, Chadema 43.



IRINGA

IRINGA MJINI

KIHESA

Ubunge: Chadema 322, CCM 162

STENDI KUU

Ubunge: Chadema, 182, CCM 79

MWEMBETOGWA

Ubunge: Chadema 56 CCM 44.

NHC

Ubunge: Chadema 108 CCM 78.

HAZINA

Ubunge: Chadema 159, CCM 75.

MGAMBO YA ZAMANI

Ubunge: Chadema 72, CCM 74.

DARAJANI

Ubunge: Chadema 111, CCM 67.

LDYDCP

Ubunge: Chadema 162, CCM 113.



TOWOGLO

Ubunge: Chadema 196, CCM 144



RUKWA

SUMBAWANGA MJINI:



Kituo cha Kantalamba A

Urais: Slaa 110, Kikwete 57.



KANTALAMBA B

Urais: Slaa 112, Kikwete 53



KANTALAMBA C

Urais: Slaa 107, Kikwete 55



KANTALAMBA D

Urais: Slaa 58, Kikwete 114



POLISI A

Urais: Slaa 57, Kikwete 67.



POLISI B

Urais: Slaa 57, Kikwete 52



MWENGE

Urais: Slaa 61, Kikwete 97.





KATANDALA A

Urais: Slaa 88, Kikwete 83



KATANDALA B

Urais: Slaa 88, Kikwete 64



KATANDALA C

Urais: Slaa 77, Kikwete 85



KATA YA MAZWI

Urais: Slaa 51, Kikwete 108.



DAR ES SALAAM



SHULE YA MSINGI KIJITONYAMA

Urais: Slaa 830, Kikwete 720.

Ubunge: Chadema 651, CCM kura 546.

Udiwani: Chadema 720, 611.



Matokeo kata ya Goba jimbo la Ubungo

URAIS

Kituo A

CCM 106, Chadema 61, Cuf 8

Kituo B

CCM 90, Chadema 70, CUF 8

Kituo C

CCM 99, Chadema 62, Cuf 4



Matokeo ya Ubunge

Kituo A

CCM 69, Chadema 85, CUF 8

Kituo B

CCM 76, Chadema 79, CUF 10

Kituo C

CCM 82, Chadema 84, CUF 0

Udiwani

Kituo A

CCM 74, Chadema 84, CUF 7

Kituo B

CCM 79, Chadema 83, CUF 8



Kituo C

CCM 85, Chadema 67, CUF 7



Kawe Tangibovu

Urais

CCM 69, Chadema 97, CUF hakuna

Kituo B

CCM 60, Chadema 100, CUF 14

Kituo C

CCM 60, Chadema 84, CUF 20

Kituo cha Makumbusho na Gereji

Kikwete 948 Dk Slaa 517 na Lipumba 315

MOSHI

Katika Jimbo la Moshi Mjini, Kata ya Mawenzi; kura za mgombea urais CCM (407), Chadema (339); mgombea ubunge CCM (341), Chadema (400); mgombea udiwani CCM (395), na Chadema (341).

Kata ya Karanga jimboni humo; kura za mgombea urais CCM (574), Chadema (813); mgombea ubunge CCM (226), Chadema (829); mgombea udiwani CCM (619), na Chadema (675).

MBEYA

Kituo cha Mwenge A: Dk. Wilbrod Slaa wa Chadema kura (91), Jakaya Kikwete (55), Ubunge Benson Mpesya wa CCM (51) na Joseph Mbilinyi au Sugu wa Chadema (115).

Mwenge B: Dk. Slaa (105), Kikwete (61), Ubunge Sugu wa Chadema (115) Mpesya wa CCM (51). Kituo cha Mwenge C: Urais Dk. Slaa kura 55, Kikwete kura 99, ubunge Sugu ana kura 120, Mpesya wa CCM ANA KURA 37. Kituo cha Mwenge D: Urais Dk. Slaa ana kura 103, Kikwete wa CCM ana kura 53 wakati ubunge Sugu wa Chadema ana kura 123 na Mpesya wa CCM ana kura 33 na Mwenge E: rais Dk. Slaa ana kura 113, Kikwete wa CCM ana kura 48 na kwenye ubunge Sugu wa Chadema ana kura 130 wakati Mpesya wa CCM ana kura 33.

Kituo cha Soweto A: Urais Kikwete ana kura 68, Dk Slaa wa Chadema ana kura 117 na kwenye ubunge Mpesya wa CCM ana kura 46 wakati Sugu wa Chadema ana kura 134.

Kituo cha Soweto B: Urais Kikwete ana kura 56 na Dk Slaa wa Chadema ana kura 123 wakati kwenye ubunge Mpesya wa CCM ana kura 41 na Sugu wa Chadema ana kura 137.

Kata ya Sisimba Urais Kikwete 79, Dk Slaa 75 na ngazi ya ubunge Sugu wa Chadema ana kura 102 wakati Mpesya wa CCM ana kura 43 na Price Mwaihojo wa CUF ana kura 02.

kuondoka kama kweli walikuwa ni wapiga kura halali.

Wananchi hao walidai kuwa muda wa kisheria ambao majina hayo yalipaswa kubandikwa ni ndani ya kipindi cha siku saba kabla ya zoezi la upigaji kura kufanyika lakini leo iweje yabandikwe asubuhi ya siku ya kupiga kura je uhakiki unafanyiikaje wamehoji.

Mwandishi wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa watu walioshuhudia hali hiyo ambapo majina yaliyokuwa yamebandikwa hapo awali katika kituo cha Bugoyi “A” – 3 kikiwa ni namba 000189620 chenye idadi ya wapiga kura 496 yalibanduliwa na kubandikwa majina mengine mapya mnamo saa 4.06 asubuhi.

Wasimamizi waliokuwa katika kituo hicho walijikuta wakiwa na jukumu la kuwasaidia wapiga kura katika kituo hicho kwa kusaidiana na askari mgambo walibandika majina mapya huku jina la kituo likiendelea kusomeka lile lile la awali lakini namba na idadi ya wapiga kura vikiwa vimebadilika.

Orodha mpya iliyobandikwa kituoni hapo ilionesha kituo hicho kilikuwa na idadi ya wapiga kura 380 badala ya 496 waliokuwepo katika orodha ya awali na namba ya kituo ikiwa ni 00018960 tofauti na ile ya awali ya 000189620.

Baadhi ya wapiga kura waliokuwa katika kituo hicho walisikika wakilamikia kitendo hicho na kueleza wazi kuwa huenda ikasababisha baadhi ya wananchi kushindwa kutumia haki yao ya kikatiba kutokana na

majina yao kutokuwemo katika orodha mpya iliyobandikwa wakati shughuli za upigaji kura zikiwa zimeanza.

“Sasa tunashangaza jamani ina maana wale waliopiga kura asubuhi kwa kutumia orodha hii inayobanduliwa hivi sasa kura zao zitawekwa fungu lipi na sisi ambao ndiyo kwanza tunayaona majina yetu katika orodha hii kura zetu zitakuwa katika fungu lipi?” alihoji mmoja wa wapiga kura katika kituo hicho ambaye hata hivyo hakupenda kutajwa gazetini.

Kwa upande wake msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika Jimbo la

Shinyanga mjini,Festo Kang’ombe alikiri kufanyika kwa mabadiliko hayo kwa kueleza kuwa majina mapya yaliyobandikwa hiyo jana ndiyo sahihi na yaliyothibitishwa na Nec.

“Ni kweli hali hiyo imetokea katika baadhi ya vituo tumelazimika kubandika orodha mpya ya wapiga kura baada ya kupokea daftari la wapiga kura lililohakikiwa kutoka Tume ya uchaguzi, orodha hiyo ndiyo sahihi zile za awali zilikuwa na makosa,” alieleza Kang’ombe.

Mabadiliko kama hayo pia yalifanyika katika kituo cha Bugoyi “A” – 4

ambapo orodha iliyokuwa imebandikwa kituoni hapo kwa kipindi kirefu ili kutoa nafasi kwa wapiga kura kuhakiki majina yao ilibanduliwa na kubandikwa orodha mpya huku mmoja wa wasimamizi wasaidizi akiwahimiza wasimamizi wa vituo hivyo kufuata orodha mpya badala ya ile ya zamani.

Hata hivyo kuhusu muda wa kisheria unaopaswa kwa majina hayo kubandikwa vituoni alisema hawakuwa na jinsi ya kufanya kutokana na

Tume yenyewe kuchelewesha kurejesha daftari la wapiga kura lililohakikiwa na hivyo kulazimika kubandika majina hayo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea.

Kumekuwepo na malalamiko kama hayo katika maeneo ya Uzungini kata ya Mjini na Majengo kituo cha AIC Chekechea Majengo kata ya Kamabarage pia katika jimbo la Shinyanga.

NEC YAAHIRISHA UCHAGUZI MAJIMBO SABA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeahirisha uchaguzi wa ubunge katika majimbo saba na udiwani wa kata 21 nchi nzima.

Taarifa ya Nec iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na NIPASHE kupata nakala yake ilisema hatua hiyo ilifikiwa katikam kikao chake kilichofanyika jana na kubaini upungufu uliojitokeza hususani katika karatasi za kura.

Miongoni mwa majimbo yaliyoathirika kutokana na kuahirishwa kwa uchaguzi wa ubunge, matatu yapo upande wa Tanzania Bara na manne yapo Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Nec, Rajab Kiravu, majimbo ya Tanzania Bara na mikoa yake kwenye mabano ni Nkenge (Kagera) Mpanda Mjini na Mpanda Vijijini (Rukwa).

Upande wa Zanzibar, majimbo yaliyoathirika ni Mwanakwerekwe, Mtoni na Magogoni kisiwani Unguja na Wete lililopo Pemba.

Kiravu alizitaka kata ambazo uchaguzi wake uliahirishwa na wilaya zilizopo kwenye mabano kuwa ni Mtonya (Newala) Endegikot (Mbulu), Kitaraka (Manyoni), Kisiwani (Same), Janga (Kibaha).

Kata nyingine ambazo zote wilayani Rufiji ni Kibiti, Chemchem, Ngorongo, Kipugira na Mjawa ambapo katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora, kata zilizohusika ni Kigwa na Ibelamilundi.

Pia zipo kata za Kisanga (Sikonge), Mji Mwema (Njombe), Msogezi (Ulanga), Kimuli (Karagwe), Kitagata (Kasulu), Buseresere (Chato) na Mkuyuni na Mirongo (Mwanza).

Kiravu alisema wananchi waliruhusiwa kupiga kura za urais na udiwani katika majimbo ambayo uchaguzi wa ubunge ulisitishwa, huku uchaguzi wa ubunge na urais uliendelea katika kata ambazo uchaguzi wa udiwani ulisitishwa.

Kiravu alisema katika taarifa hiyo kuwa, siku ya kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa baadaye.

No comments: