MKOA wa Kigoma umeongoza kwa kutoa wabunge wengi wa upinzani dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kuna wabunge watano wa upinzani katika mkoa huo, CCM imepoteza wabunge zaidi ya 25 Tanzania Bara.
Kigoma inafuatiwa kwa karibu na Kilimanjaro ambao umetoa majimbo manne kwa upinzani huku yaliyosalia yakitwaliwa na CCM.
Mkoa wa Kigoma umepeleka majimbo matano kwa vyama vya upinzani na ni miongoni mwa majimbo manane ya uchaguzi katika mkoa huo wa Magharibi mwa Tanzania.
Kati yao, manne yamekwenda NCCR-Mageuzi na moja Chadema, iliyotetea kiti chake cha Kigoma Kaskazini kupitia kwa Zitto Kabwe.
Majimbo yaliyokwenda NCCR-Mageuzi ni Kasulu Mjini; Kasulu Vijijini; Kigoma Kusini na Muhambwe. Kabla ya kugawanywa kwa majimbo ya Kasulu, CCM ilikuwa na wabunge katika majimbo hayo; Kasulu Mashariki na Magharibi kama ilivyokuwa kwa Muhambwe.
Kigoma Kaskazini, Zitto aliibuka mshindi kwa kupata kura 23,315 dhidi ya kura 18,416 za mgombea wa CCM, Robinson Lembo huku mgombea wa CUF, Omari Nkwarulo akipata kura 4,834.
Kasulu Mjini, mgombea wa NCCR-Mageuzi, Moses Machali alishinda dhidi ya Raphael Neka wa CCM, huku aliyewahi kuwa Naibu Waziri katika Awamu ya Nne, Daniel Nsanzugwanko, akishindwa Kasulu Vijijini na mwanamama wa NCCR - Mageuzi, Zaitun Buyogera. CCM imeshinda Manyovu, kwa mgombea wake, Albert Ntibaliba ‘Obama’ kuwashinda Basilius Budida wa Chadema na Sabuni Samson wa CUF.
Muhambwe wilayani Kibondo mgombea wa NCCR-Mageuzi, Felix Mkosamali ameibuka mshindi dhidi ya Jamal Tamim wa CCM na Athuman Masudi wa CUF. Buyungu, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza alishinda kwa kura 17,500 dhidi ya 11,000 za mgombea wa NCCR- Mageuzi, Mawazo Athanas. Peter Serukamba ametetea jimbo lake la Kigoma Mjini.
Lakini mbali ya kupoteza majimbo hayo manne ya Kigoma, CCM ilikuwa pia imepoteza majimbo ya Nyamagana, Ilemela, Iringa Mjini, Musoma Mjini, Arusha Mjini, Vunjo, Hai, Moshi Mjini, Lindi Mjini, Maswa Mashariki, Maswa Magharibi na Mbulu. Mengine ni Karatu, Rombo, Ubungo, Kawe, Meatu, Bukombe, Singida Kaskazini na Mbozi Magharibi.
Lakini CCM pia imeonesha makali yake katika majimbo ya Tabora ambako imeshinda kwa kura nyingi.
Majimbo iliyoshinda na wagombea katika mabano ni Ismail Rage (Tabora Mjini); Samuel Sitta (Urambo Mashariki); Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi); Dk. Athumani Mfutakamba (Igalula); Rostam Aziz (Igunga) na Sumar Mamlo (Tabora Kaskazini).
Aidha, wagombea wa majimbo ya Bukene, Nzega na Sikonge walikuwa wakifanya vizuri.
Majimbo yaliyokwenda upinzani Nyamagana Ezekiel Wenje wa Chadema (38,171), Lawrence Masha (CCM) kura 27,883 na kumpita kwa kura 10,288.
Iringa Mjini Peter Msigwa wa Chadema (17,748), Monica Mbega wa CCM (16,916), Mariam Mwakingwe wa NCCR- Mageuzi (950), ambapo kura zilizopigwa ni 35,610. Arusha Mjini Godbless Lema wa Chadema (56,561), Batilda Buriani wa CCM (37,460).
Musoma Mjini Vincent Nyerere wa Chadema (21,335), Vedasto Mathayo wa CCM (14,072) Mustapha Wandwi wa CUF (253), Chrisant Nyakitita wa DP (53) na Tabu Said wa NCCR- Mageuzi (19). Lindi Mjini Salum Bariani wa CUF (13,155), Mohamed Abdulaziz wa CCM (11,443) .
Ilemela Highness Samson wa Chadema (31,269), Anthony Diallo wa CCM (26,270). Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wa Chadema (46,411), Benson Mpesya wa CCM (24,327).
Kasulu Vijijini Zaituni Buyogela wa NCCR- Mageuzi (26,130), Daniel Nsanzugwako (18,482).
Maswa Magharibi John Shibuda wa Chadema (17,556), Robert Kisena wa CCM (12,135).
Maswa Mashariki Sylvester Mkoja wa Chadema (17,075), Peter Bunyongoli wa CCM (14,014).
Moshi Mjini Philemon Ndesamburo wa Chadema (28,697), Justin Salakana CCM (18,792). Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wa Chadema (23,315), Robinson Lembo (18,416) na Omari Nkwarulo wa CUF (4,834).
Kasulu Mjini Michael John wa NCCR Mageuzi (15,399), Sylvester Koka wa CCM (10,849). Mbulu Mustapher Akunay wa Chadema (48,428), Philip Marmo wa CCM (27,216), Eliusi Amedeus wa CUF (540).
Karatu Mchungaji Israel Yohana wa Chadema (41,109), Willibrod Lori wa CCM (26,211). Rombo Joseph Selasini wa Chadema (29,566), Basil Mramba (27,649) na Vitus Merinyo wa Demokrasia Makini (439).
Ubungo John Mnyika wa Chadema (66,742), Hawa Ng’humbi CCM (50,544) Julius Mtatiro wa CUF (12,964), Prosper John wa AFP (437), Emil Ruvunja wa APPT-Maendeleo (317), Amina Mcheka wa Chausta (519), Kaminambeo Rajabu wa DP (149) na Samira Lakhan wa Jahazi Asilia (138).
Wengine ni Kazimoto Thabiti wa NCCR-Mageuzi (253), Rashid Mawazo wa NLD (94), Rachel George wa NRA (47), Kibogoyo Rweyunga wa SAU (40), Kambona Mwansasu wa TLP (113), Zablon Mazengo wa UDP (48), Kamana Mrenda wa UMD (22) na Naomi Mabruki wa UPDP (69).
Kawe Halima Mdee wa Chadema (43,365), akifuatiwa na Angela Kizigha wa CCM (34,412), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi (11,970), Shaban Mapeya wa CUF (9,131), Grace Rendi wa UDP (673), Nathaniel Mlaki wa NLD (375), Michael Nderumai wa SAU (50), Steven Katumbi wa TLP (215) na Richard Mahalaka (215).
Muhambwe Felix Mkosamali wa NCCR-Mageuzi (25,391), Jamal Tamim wa CCM (15,141) na Athuman Masudi wa CUF (481).
Vunjo Augustino Mrema wa TLP (30,810), Cryspin Meela wa CCM (23,870). Wengine ni John Mrema wa Chadema (616) na Stanley Lyimo wa NLD (23). Hai Freeman Mbowe wa Chadema (28,585) na Fuya Kimbita (23,349).
Meatu Meshack Opulukwa wa Chadema (13,890) na Salum Khamis wa CCM (12,390). Majimbo yaliyotwaliwa na CCM Bukoba Mjini Khamis Kagasheki (CCM) kura 18,491 na Wilfred Lwakatare (Chadema) kura 13,800.
Bukoba Vijijini Jackson Rweikiza (CCM) kura 57,852, Aristides Ndibalema (Chadema) kura 5,859 na Twaha Taslimu (CUF) kura 4,565. Dodoma Mjini David Malole (CCM) kura 52,243 na Enock Muhembano (Chadema) kura 15, 806.
Tarime Nyambari Nyangwine (CCM) kura 28,604 na Mwita Waitara (Chadema) kura 27,334. Mwanga Jumanne Maghembe (CCM) kura 20,730 na Shaffi Msuya (Chadema) kura 4,719.
Nyang’wale Hussein Amary (CCM) kura 19,987, Nguru Tanganyika (Chadema) kura 2,271 na Andrew Masanja (CUF) kura 1,032.
Korogwe Mjini Yusuf Nassir (CCM) kura 12,090, Calistus Shekibuha (Chadema) kura 1,720 na Jumaa Mgogo (CUF) kura 400.
Mbarali Dickson Kirufi (CCM) kura 34,869, Kazamoyo Kangwa (Chadema) kura 16,090 na Getrude Dwila (TLP) kura 487. Peramiho Jenista Mhagama (CCM) kura 28,753 na Mchungaji Chilokota kura 2,562.
Tunduru Kaskazini Ramo Makani (CCM) kura 19,573, Mzee Rajabu (CUF) kura 17,365 na Randi Daudi (Chadema) kura 604. Tunduru Kusini Mtutura Mtutura (CCM) kura 16,856 na Mohamed Mambo (CUF) kura 10,930.
Singida Mjini Mohamedi Dewji (CCM) kura 21,169, Joseph Isango (Chadema) kura 3,457 na Rashidi Mindicar (CUF) kura 648. Arumeru Magharibi Godluck ole Medeye (CCM) kura 35,544 na Jackson ole Kisambo (Chadema) kura 27,425.
Arumeru Mashariki Jeremiah Sumari (CCM) kura 34,379 na Joshua Nassare (Chadema) kura 19,189.
Mkinga Dustan Kitandula (CCM) kura 16,967 na Bakari Mbega (CUF) kura 11,252. Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (CCM) kura 11,361, Agnes Emmanuel (Chadema) kura 2,201 na Abdallah Zugo (CUF) kura 1,086.
Kibaha Mjini Sylvestry Koka (CCM) kura 14,028, Habibu Mchange (Chadema) kura 10,450 na Lidya Bendera (CUF) kura 529. Kisarawe Selemani Jaffo (CCM) kura 19,832, Kondo Adamu (CUF) kura 3,577 na Athumani Athumani (UPDP) kura 1,114.
Pangani Salehe Pamba (CCM) kura 9,342, Omari Ally (CUF) kura 4,521 na Abdallah Omari (Chadema) kura 1,222. Mafia Abdulkarim Shah (CCM) kura 8,137, Wahab Twairut (CUF) kura 5,384 na Abdul Selemain (Chadema) kura 1,553.
Igunga Rostam Aziz (CCM) kura 35,674 na Leopald Mahona (CUF) kura 11,733. Urambo Mashariki Samwel Sitta (CCM) kura 19,947, Msafiri Mtemelwa (Chadema) kura 5,134 na Zombwe Edward (CUF) kura 1,009.
Urambo Magharibi Juma Kapuya (CCM) kura 18,691, Kiyungi Kiyungi (CUF) kura 11,733 na Rashidi Kafuram (Jahazi Asilia) kura 290. Tabora Mjini Ismail Rage (CCM) kura 27,329, Kapasha Kapasha (CUF) kura 7,792 na Musa Kwikima (Chadema) kura 3,682.
Igalula Athumani Mfutakamba (CCM) kura 8,971, Erick Kabepele (Chadema) kura 1,972 na Migwayasila Hasani (CUF) kura 1,729. Tabora Kaskazini Sumar Mamlo(CCM) kura 18,882, David Kasoga (CUF) kura 2,098 na Subiri Mmta (Chadema) kura 888.
Sikonge mgombea Said Nkumba (CCM) alikuwa akiongoza na Nzega Hamisi Kingwangala (CCM) alikuwa mbele na Bukene, Sulemani Zed (CCM) alikuwa na kura nyingi hadi jana.
Shinyanga Mjini Stephen Masele (CCM) kura 18,750 na Philipo Shelembi (Chadema) kura 18,507.
Monduli Edward Lowassa (CCM) kura 30,236, Shiranga Mollel (Chadema) kura 2,356 na James Mavaya (CUF) kura 67. Njombe Magharibi Grayson Lwenge (CCM) kura 27,000 na Thomas Nyimbo (Chadema) kura 13,000.
Njombe Kaskazini Deo Sanga (CCM) kura 29,000 na Alatanga Nyagawa (Chadema) kura 8,500. Same Mashariki Anne Kilango (CCM) kura 15, 979 na Chadema kura 9,917.
Mtwara Mjini Hasnain Murji (CCM) kura 17,004, Uledi Abdallah (CUF) kura 10,560 na Athumani Jetha (Chadema) kura 1,089.
Kilosa Mustafa Mkulo (CCM) kura 31,004, Willy Dikunile(CUF) kura 3,484 na Kisegere Zainam (Chadema) 2,552. Mpaka jana mchana majimbo ya Gairo na Mikumi hayakuwa yametangaza matokeo ya ubunge.
Kinondoni Idd Azzan (CCM) kura 51,372, Philip Mugendi (Chadema) kura 27,355 na Nassor Haji (CUF) kura 22,660. Tanga Omar Nundu (CCM) kura 40,225, Mussa Mbarouk (CUF) kura 24,262 na Kassim Mbaraka (Chadema) kura 5,750. Kilolo Peter Msolla (CCM) kura 45,719 Clay Mwitula kura 3,117.
Bagamoyo Shukuru Kawambwa (CCM), kura 15,829, Neema Msuya (Chadema) kura 2,364 na Zahoro Vuai (CUF) kura 1,861. Mvomero Amos Makalla (CCM) kura 41,431, Matokeo Oden (Chadema) kura 18, 801 na Rehama Maguvu (UDP) kura 969.
Moshi Vijijini Cyril Chami (CCM) kura 31,352, Anthony Komu (Chadema) kura 20,394 na Elias Obote (DP) kura 240.
Hanang Mary Nagu (CCM) kura 37,270 na Rose Kamili (Chadema) kura 21,174.
Temeke Abbas Mtemvu (CCM) kura 58,339, Luca Limbu (CUF) kura 28,877 na Dickson Ng’hily (Chadema) kura 27,899. Siha Aggrey Mwanry (CCM) kura 15,255 na Tunu Ibrahim (Chadema) kura 7,758.
Morogoro Kusini Mashariki Lucy Nkya (CCM) kura 20, 324,Aquiline Magalambula (Chadema) kura 1,770 na Blandina Mwasabite (CUF) kura 3,509.
Morogoro Kusini Innocent Kalogeris (CCM) kura 20,917, Juma Tembo (Chadema) kura 4,798 na Nasra Asenga (AFP) kura 631. Longido Lekule Laizer (CCM) kura 17,687, mgombea wa Chadema kura 230.
Kondoa Kaskazini Zabein Mhita (CCM) kura 33,413, Deni Rashid (CUF) kura 17,413 na Majara Maulid (Chadema) kura 2,612. Kondoa Kusini Juma Nkamia (CCM) kura 38,343 na Hassan Misanya (CUF) kura 8,295.
Sumbawanga Mjini Aeish Hilaly (CCM) kura 17,328, Norbert Yamsebo (Chadema) kura 17,132 na Ifgenia Leba (CUF) kura 76.
Nkasi Kaskazini Ali Kessy (CCM) kura 11,883, Kessy Sudi (Chadema) kura 10,031 na Vickson Konga (NCCR –Mageuzi) kura 330 Nkasi Kusini Desderius Mipata (CCM) kura 10,788, Hypolito Kaninga (Chadema) kura 8,358 Babati Mjini CCM kura 13,506, Chadema 6,866 na UDP kura 581 Ruangwa CCM kura 27,671, CUF kura 9,024.
No comments:
Post a Comment