Matokeo ya kura za urais jana yalizidi kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), yakionyesha kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akiongoza na kufuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akiwa nyuma.
Wagombea wengine wane walikuwa wameachwa nyuma sana katika matokeo hayo.
Hadi jana, matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame, yalihusisha majimbo 177 ambapo Kikwete alipata kura 3,604,219, Dk. Slaa kura 1,388,568 na Prof. Lipumba kura 469,780.
Soma zaidi
No comments:
Post a Comment