Monday, November 8, 2010
BREAKING NYUUUUUZZZZ: TAKUKURU YATOA TAMKO JUU YA CHENGE
Bosi wa TAKUKURU Dk. Edward Hosea
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.
TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.
Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.
Simu: 2150043-6/2150360
Nukushi: (022) 2150047
Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao www.pccb.go.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya JMT Andrew Chenge na TAKUKURU wote kwa nyakati tofauti wamedai kuwa Chenge hakuhusika katika kashfa ya rada.
Lakini tuhuma na ushahidi uliopo katika barua ya SFO kwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa JMT ya tarehe 21 March 2008 inaonyesha kuwa Chenge, bado anao Mkono katika tuhuma hizi nzito. Na bado anawajibika kuwajibu wa Tanzania alipata wapi USD 1.5 Million badala ya kuja na majibu mepesi kwa maswali magumu kuwa "hivyo ni visent vyangu na nina haki ya kikatiba kutokueleza nilikozipata"
Ninachoshindwa kuelewa ni wanasiasa wa Tanzania na Watendaji wao; Je wanatufanya Watanzania hamnazo au mazezeta sana? Je, kwa barua hii na tuhuma zilizoelekezwa kwake ana majibu gani ya kutupa hata kama anadai SFO wamem- clear. Hizo USD 1.5 Million alizitoa wapi? Na huyu ndiye sasa anataka awe Spika wa Bunge letu.
Ole wao wabunge wakimchagua 2015 si mbali, mtakutana na hukumu ya moto!
Je PCCB na Chenge Wamedanganya? Ni kweli SFO hawajamhusisha Chenge na tuhuma hizi?
Edwin
Post a Comment