Na Esther Macha, Mbeya
KUSHAMIRI kwa mfumo dume katika wilaya ya Mbeya
kunaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi kwa wanawake ambao ndio nguvu
kazi kubwa katika kilimo, kipato wanmachopata baada ya mavuno huishia mikononi
mwa wanaume wanaojihusiusha na vitendo vya starehe na kusahau malezi ya familia
zao.
Uchunguzi uliofanywa na Majira kwa takribani wiki
moja kwa msaada wa mtandao wa jinsia
Tanzania (TGNP)umegundua kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji na ukatili
wanavyofanyiwa wanawake wa vijiji vya Ifiga,Iwalanje na Nsongwi juu Kata ya Ijombe vinavyotokana na nguvu ya
wanaume ya kuhodhi mali zilizopatikana kwa kuwashirikisha wanawake.
Mmoja wa awanawake wa Kijiji cha Ifiga Bi Salah Jailos
alisema kuwa wakati wa msimu wa kilimo
unapowadia hushirikiana na waume zao kwa
karibu bila kuwepo ugomvi wowote ndani ya familia zao mpaka mazao yanapokomaa.
Alisema kuwa inapofika kipindi cha kuvuna wanaume huanza kubadilika kwa kutafuta sababu mbali
mbali za kuonyesha chuki ndani ya nyumba
ili aweze kupata sababu za kuvuna peke yake mazao na kuuza pepe yake bila
kumshirikisha mke wake.
“Hali hii inatusikitisha sana kwani akishauza mazao haya
huondoka nyumbani na kwenda kufanya starehe zake na wanawake wengine , lakini
fedha baada ya kuisha hurudi nyumbani na kuanza kutafuta visababu vidogo vidogo
kwa kuanza kudai chakula na kutoa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja
na kudai kuwa chakula kibichi mara hufai kuishi na mimi mara nataka kuoa
mke mwingine maadamu tu apate sababu za kujitetea ili mwanamke nionekane
mbaya”alisema mwanamke huyo.
Mwanamke mwingine mkazi wa Usongwe Juu Bi.Benadeta Hamisi
alisema kufutia vitendo hivyo vya wanaume tunaomba waache kwani iweje wakati wa
kilimo tulime wote lakini inapofika
wakati wa mavuno wawe wababe wa kuuza mazao9 peke yao kwa ujumla huu ni ukatili
wa kijinsia kwa sisi wanawake wa Kata ya Ijombe.
“Tunaomba waume zetu waache tabia hii kwani mazao haya
tunalima sote hivyo hata wakati wa kuvuna inatakiwa tuwe pamoja na hata kuuza
vile vile inatakiwa kusimama kwa pamoja kama mke na mume ioli fedha hizo
zitakapopatikana mazao na kuuza yaweze
kusaidia kulea familia zetu pamoja na kusomesha”alisema Bi. Hamis.
Hata hivyo mwanamke huyo alisema athari ambazo wanapata
baada ya kuachiwa familia ni kupata shida ya
kuhudumia familia ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto namahitaji mengine
ya nyumbani ambayo ni muhimu.
Akizungumzia malalamiko hayo kwa Wanawake wa vijiji
hivyo, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ifiga Bw.Raphael Siyejele alisema hana taarifa za kiofisi za
wanaume kuwanyanyasa wake zao labda kama zipo ngazi zingine.
No comments:
Post a Comment