Na Boniface Meena
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),
kimelaani kukamatwa na kushambuliwa kwa viongozi wa madaktari ikiwamo Dk
Ulimboka Steven ikieleza kuwa hatua hiyo haiwezi kuwa suluhu bali
itachochea zaidi mgogoro wa madaktari na Serikali.
Taarifa
iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John
Mnyika inaeleza pia kwamba udhaifu wa Serikali kuharakisha kwenda
mahakamani kabla ya Bunge kupewa fursa ya kujadili madai ya madaktari na
kuisimamia Serikali umelifikisha taifa katika hali iliyopo sasa.
"Nalaani
uamuzi wa Serikali wa kutumia vyombo vya dola kukamata na kushambulia
viongozi wa madaktari ikiwemo Dk Ulimboka Steven kwa hauwezi kuwa suluhu
bali utachochea zaidi mgogoro kati ya madaktari na Serikali,"
ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo ya Mnyika na kuongeza:
“Nichukue
fursa hii kuwaomba madaktari kufanya kila kinachowezekana kuokoa uhai
wa wagonjwa katika kipindi hiki kigumu.” Mnyika alisema kuwa ameomba
wabunge wapewe nakala ya Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu
madai ya madaktari na hoja ya taarifa husika iwekwe katika orodha ya
shughuli za Bunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea ili ijadiliwe na
kupitisha maazimio, kuwezesha hatua za muda mfupi, wa kati na muda mrefu
kuupatia ufumbuzi mgogoro huo na kuboresha sekta ya afya nchini.
“Natarajia
kwamba Spika atawezesha kamati kuwasilisha taarifa yake na Bunge
kujadili baada ya Serikali kutoa kauli yake bungeni,”alisema. Mnyika
alisema ikiwa wabunge wataelezwa ukweli na kupewa taarifa kamili
wataweza kuisimamia Serikali na kuwaeleza ukweli madaktari kipi
kinawezekana na kipi hakiwezekani.
Alisema kuwa ingawa Waziri
Mkuu Mizengo Pinda ametoa maelezo bungeni kuwa Serikali itatoa kauli
bungeni kuhusu mgomo huo, Bunge halitaruhusiwa kujadili kauli husika,
hivyo kukoseshwa fursa ya kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi.
No comments:
Post a Comment