MKAGUZI Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovic Utouh ameitaka
serikali kubadili mfumo wake wa kutoa bajeti kwani bado ni mbovu.
Utouh
pia aliionya serikali kuwa makini katika kuanda bajeti yake kwa kuwa
katika kipindi cha miaka miwili iliyopita haikufanya vizuri katika
usimamizi wa fedha.
Utouh aliyasema hayo katika kikao cha mwisho cha uwajibikaji kilichofanyika jijini Dar es salaam juzi .
“Kwa
mfumo huu tuliokuwa nao kunahitajika mabadiliko ya haraka kuweza
kunusuru nchi yetu bila hivyo kila siku bajeti zitakuwa mbovu
tu”alisema Ludovick.
Alieleza kuwa kufikia malengo hayo
kunahitajika mabadiliko kwa wananchi na serikali kujua bajeti kwa
usahihi kabla hazijapitishwa katika bunge.
Naye Mwenyekiti wa
Kamati ya Fedha za Hesabu za Serikali (PAC) Joh Cheyo alisema wabunge
wameonyesha uwezo wao kuangalia mahesabu ya serikali kwa umakini na siyo
kwa upinzani,hivyo ni dhahiri kuna mabadiliko na siku za nyuma.
Cheyo
alieleza kuwa mkutano uliokuwa ukielendelea kwa siku tatu umewapa
mwangaza zaidi wa kuliangalia Taifa kwani wamepata changamoto kutoka kwa
wageni waliotoka nchi za jirani na kuhudhuria kwa kutoa ushauri na
majadiliano.
“Tumepata uzoefu kwa wageni toka Uganda, Malawi na Sudan kwa kweli wametupa changamoto za maswali na ushauri”alisema Cheyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya
Umma Zito Kabwe alisema kuwa wananchi wameona hatua iliyo chukuliwa na
serikali katika swala la uwajibikaji,hivyo ni vyema kuwa makini katika
swala hilo kunusuru Taifa.
“Htimaye wananchi wameona hatua zilizo
chukuliwa na serikali kwa swala la uwajibikaji, ni vyema kujifunza
kabla hayaja kukuta makubwa” alisema Zito.
Zito alifafanua kuwa
huu siyo muda wa kukaa na kuongelea mambo yaliyo pita bali ni wakati
mzuri wa kuundwa sheria za utekelezaji wa bajeti.
No comments:
Post a Comment