Friday, April 1, 2011

Wasemavyo wananchi kuhusu mfumuko wa bei nchini

Herieth Kabende(Mkazi wa Ubungo Makuburi)
Bei ni tatizo, kwani ziko juu hazina uafadhali.
Viongozi wako wapi? Wanafanya nini?
Kwa mfano maharage kilo ilikuwa tsh.600/=-700/= sasa ni tsh.1800/=-2000/=, nauli zimepanda kutoka tsh.100-150/= kwa wanafunzi na watu wazima kutoka tsh.250-300/=
“Kama shida ni mafuta basi wafanye ustaarabu utakao wasitiri wananchi wenzao hata hasa wenye kima cha chini ambao ndio wengi.”

Eliabu Maganga(Mkazi wa Tabata)
Kauli kutoka kwenye uongozi wa serikali ni za kejeli kwamba “Kila mtu atajijua”
Viongozi wamelewa madaraka kwani ahadi zao ni sifuri kutokana na hali halisi inavyojionesha, kushuka kwa ajira, kushuka kwa huduma bora pamoja kutokupandisha mishahara ya wafanyakazi.
“Serikali ifunge mkanda katika kupunguza gharama za mafuta.”

Amina Mcheka(Mkazi wa Mburahati)
Kutoka kwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mustafa Mkulo inaonekana serikali haijui namna ya kutatua hili tatizo.
Kwa mfano mshahara ni ule ule, huku sukari, unga,na nauli vikiwa vimepanda.
“Kodi ipunguzwe kwa bidhaa ya mafuta pia ukusanyaji wa kodi uboreshwe kani ni mbovu.”

Msafiri Shabani(Mkazi wa Mabibo)
Kupitia kauli za Rais kwamba bei ipungue kutoka tsh.2000/= hadi tsh. 1700/= la sivyo wahusika wachuku-liwe hatua,lakina hadi sasa bei haijapungua na hatua hazijachukuliwa kwa wahusika kwa hiyo yalikuwa ni maneno bila utendaji.
Sababu hasa ya mfumuko wa bei ni mafuta ambayo kitovu chake ni EWURA kwani inatoa majibu ya ubabaishaji….”Mara meli za mafuta zimetekwa, ama nchi za kiarabu zinaleta shida kwa suala zima la maisha, hivyo basi hakuna haja ya kuwa na EWURA.”
Hivyo basi, serikali iiangalie EWURA kwa undani zaidi na ichukue hatua.

Maua Abdul(Mkazi wa Mwananyamala)
Mfumuko wa bei umetuathiri sana kama wananchi kwani mishahara ni ile ile.
“Serikali iangalie kwa umakini na ufahamu zaidi uwiano kati ya hali halisi ya sasa ya Mwananchi na hiyo mifumuko ya bei.”

Badi Darusi(Mkazi wa Kigogo)
Chanzo cha mfumuko wa bei ni kupanda kwa bei za mafuta, mfumo wa kibepari na kushushwa kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
“Kuna haja ya kuelewesha wananchi kuhusu mwelekeo wa bajeti ya uchumi wa nchi pia pamoja na kujua sera ya uchumi mkuu wa taifa (macro economy).”

No comments: