Thursday, April 28, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Uchambuzi wa seria ya KILIMO KWANZA,Ajira, Biashara na Maisha Endelevu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umezindua muhtasari ya uchambuzi wa sera ya KILIMO KWANZA: Maana na umuhimu wake kwa jamii iliyoko pembezoni, Wanawake, Wanaume wa Tanzania na Ajira, Maisha endelevu na Biashara
Muhutasari huu umelenga kutoa uch ambuzi yakinifu wa sera za serikali na mgawanyo wa bajeti katika sekta hizi mbili muhimu. Ajira na Maisha Endelevu na Kilimo, kwani zina mahusiano ya karibu na maendeleo ya wanawake walioko pembezonina wanaume; na ni kitovu cha kampeni yetu ya: “Haki ya Uchumi: Rasilimali ziwanufaishe wanawake walioko pembezoni.


Kila muhtasari wa uchambuzi wa sera tulioufanyia kazi uliuliza maswali kadhaa kuwa ni kwa kiasi gani sera hizi zinaweka vipaumbele mahitaji muhimu ya wanawake hasa wa kipato cha chini wa vijijini na mijini sio tu kinadharia bali kwa mikakati imara ya mgawanyo sawa wa rasilimali?
Idadi kubwa ya wanawake wa Kitanzania wanategemea kilimo cha mikono kwa maisha endelevu, kama chanzo cha kujipatia kipato, pia kama chanzo cha chakula cha kila siku kwa familia na jamii. Pia idadi kubwa ya wanawake na wanaume bado imeendelea kutegemea sekta ya kipato isiyo rasmi kama chanzo cha kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji ya kila siku kwa wote wanaoishi vijijini na mijini
TGNP katika uchambuzi huu wa sera hizi mbili, tumeona


kuwa sera na bajeti zinaweka kipaumbele madai na mahitaji ya makampuni makubwa ya nje na ndani kama msingi wa kuendesha na kukuza biashara ya nje. Kutokana na kipaumbele hiki umuhimu wa kusimamia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kujitegemea umesahaulika pamoja na mkakati wa maendeleo ya wananchi wenyewe.


Lengo kuu la sera ya KILIMO KWANZA ni kuweka nguvu kwa wazalishajiwakubwa kwa kuwapa kupata vipaumbele kutoka serikalini hasa katika maeneo ya mikopo, misamaha ya kodi, ruzuku na nyinginezo. Pia wamekuwa wakitumia njia hiyo kudai soko huria katika ardhi, umiliki wa ardhi, kwa kigezo kuwa watawafikia wananchi wa hali ya kawaida walioko vijijini.


Changamoto kubwa katika sera hii ya sasa ya KILIMO ni jinsi inavyoonekana kukubali na kuukabiribisha mfumo mpya wa matumizi ya mbegu zilizorekebishwa – “genetically modified seeds” (GM), maarufu kama “mbegu za miujiza” (Miracle Seeds), unaolenga kuzalisha mbegu za mazao katika maabara, kilimo cha mazao ya nishati (Biofuel), matumizi makubwa ya mbolea za viwandani na madawa ya kilimo.

Uchambuzi uliofanywa kuhusu mfumo huu hapa Afrika na Asia umeweka wazi athari na changamoto za tekonolojia hii ya uzalishaji mbegu inayomlazimisha mkulima mdogo kuwa na majukumu makubwa kinyume na uwezo wake. Mfumo unaelekeza nguvu zake katika kilimo kikubwa wakati walengwa ni masikini. Hatua hii inapelekea mashirika makubwa yanayojihusisha na kilimo na biashara kunufaika kupitia ukodishaji wa mashamba, uuzaji wa pembejeo, madawa na mbolea na kuwaacha wakulima masikini mikono mitupu.

Wakati mwingine hawa ndio wamekuwa wananunuzi wa kubwa wa mazao yanayozalishwa kwa kulangua, mabenki makubwa pia yameonesha kunufaika zaidi kuliko mwananchi masikini kutokana na kudai riba kubwa katika mikopo ya kilimo hasa hiki cha uzalishaji wa mbegu.
Mfumo huu wa mbegu za GM umekuwa kikwazo kwa wakulima wadogo kwa sababu hawawezi kuhifadhi mazao yao ili kuandaa mbegu kwa ajili ya msimu unaofuata, kwa hiyo unawalazimisha wakulima wadogo kuendelea na mtindo wa kununua mbegu madukani kila mwaka badala ya kuzalisha za kwao kwa njia za asili. Athari nyingine ni matumizi ya zana kubwa katika kilimo kinachotumia mitambo na mafuta, hivyo kusababisha makampuni makubwa ya mafuta kujiingiza humo, kama wanufaika wakubwa na hivyo kujenga nguvu kubwa ya ushawishi ya kuendeleza aina hii ya kilimo.


Ili kutimiza hili, sehemu ya ardhi ya kilimo cha chakula lazima itumike, na hivyo mkulima kulazimika kugawa muda wake kati ya kilimo cha mazao ya biashara ambayo serikali inayataka (na kwa yeye kupata fedha kulipia kodi), na kilimo cha chakula kwa ajili ya familia yake.
Kwaupande mwingine kukimbilia teknolojia hii, serikali inajivua wajibu wa kumwendeleza mkulima mdogo na kufungua milango kwa masetla; hivyo kumfanya abaki kibarua kwenye ardhi yake aliyoirithi.


Mfumo wa GM umekuwa ukishinikizwa Tanzania na nchi jirani na Jumuiko la Mapinduzi ya Kijani Kibichi Afrika, (AGRA), Ukuzaji wa Kilimo katika mwambao wa Kusini na mashirika makubwa ya kilimo cha biashara. Banki ya StanBanki na kampuni za Monsanto, SAB Miller, Diageo, Syngenta na General Mills, wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye kilimo ambacho hakitoi usalama wa chakula wala ajira kwa Watanzania, bali ni kunufaika katika kuuza chakula nje na mzao ya nishati mbadala na kuongeza bei ya chakula katika soko la ndani.


Uchambuzi wetu wa Sera ya Ajira, Maisha na endelevu na Biashara umeongozwa na swali je,ni mikakati gani imewekwa ya kuongeza Ajira na maisha endelevu kwa Watanzania wote wanawake na wanaume? Mtazamo wa serikali na mwelekeo wake umeonekana kuwa ni kuangalia vikundi vidogo vya uzalishaji ambavyo hata hivyo wanaonufaika nao ni wanawake na wanaume wajasirimali wenye uwezo walioko mijini wakati walio wengi vijijini wakiwa wameachwa.
Kwa sasa idadi kubwa ya wanawake na wanaume wa vijijini na mijini wamenyang’anywa kila fursa ya uzalishaji kwa ajili ya maisha endelevu, kama vile ardhi, maji, misitu, nk. Athari hizi ni matokeo ya unyang’anyaji wa ardhi za wananchi, mikakati ya mipango miji, kukimbizwa na kufukuzwa kwa wamachinga, vibanda vidogo, bomoa bomoa na kuingiza ardhi katika biashara huria. Wakati huo huo mfumo wa uchumi kuuza mazao nje ya nchi bila mkakati mathubuti ya kuendeleza soko la ndani unaendelea kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha tabaka kati ya masikini na tajiri kwa wote wanaoishi vijijini na mijini.


Katika mkanganyiko huu wanawake wanakumbana na changamoto zaidi zinazotokana na mfumo dume ulioko serikalini na katika taasisi za kijamii kwa kupata nafasi chache za ajira, mikopo, ardhi, na elimu kuliko wanaume.
Kwa mfano katika kiwango cha asilimia 14 ya masaa yote ya ya siku wanawake huwa wanafanya kazi isiyo na malipo, wakati wanaume ni asilimia 5 tu ya muda wao hutumika kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo. Utafiti wa kitaifa wa soko la ajirawa mwaka 2006, uliainisha kwamba asilimia 66 ya wanaofanya kazi kama wasaidizi kwenye familia bila malipo ni wanawake. Wakati huo huo, taratibu wa kumiliki na kurithi ardhi ya familia unaendelezwa kwa kufuata mfumo dume wa mila na desturi ambazo zinawanyima haki wanawake.
Wanaharakati wa kifeministi wanaamini kuwa Watanzania wote wanaume na wanawake wana haki sawa ya kupata ajira na maisha endelevu. Kufikia ajira kwa wote kunategemea mabadiliko ya kisasa katika mikakati ya maendeleo sera za nchi.

Imetolewa na:
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji

Nape: Ni kawaida 'kulimana' barua CCM

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ametetea uamuzi wa chama hicho kuwaandikia barua watuhumiwa wa ufisadi.

Nnauye amesema, huo ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho si lazima litolewe kama azimio kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Akizungumza na HABARILEO, Nape amesema, kama kuna jambo limejadiliwa ndani ya kikao cha chama na linamhusu mwanachama ili liwe la kiofisi ni lazima mhusika ajulishwe kwa barua.

“Suala la barua ambalo sasa linaonekana kuwa mjadala mkubwa sio big deal, hili ni jambo la kawaida kwamba kuna mambo yamejadiliwa na kufikiwa kwa maamuzi hivyo wahusika lazima wataarifiwe kwa barua,” amesema Nnauye ambaye kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi.

Ametoa mfano kuwa, hata alipoteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi licha ya kuwa alikuwemo kwenye kikao kilichotangazwa uamuzi huo, lakini aliandikiwa barua rasmi ya kutaarifiwa juu ya uteuzi huo.

“Hata Katibu Mkuu wetu pale alipo ana barua inayo mtaarifu juu ya uteuzi wake, haitoshi kumtangaza mbele ya vyombo vya habari halafu asipewe barua, hivyo hivyo maamuzi yanayohusu mwanachama mwingine ye yote awe na tuhuma kama hizo za ufisadi au mambo mengine lazima pia yawekwe kwenye maandishi na ataarifiwe,” amefafanua Nape.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya kushutumiwa na baadhi ya makada wa CCM kuwa ndani ya NEC hakukuwa na azimio la watuhumiwa wa ufisadi kuandikiwa barua wala kupewa siku 90 za kujiondoa kwenye uongozi.

Wanaomshutumu wanadai kuwa anatoa matamshi kwa maslahi yake binafsi, lakini Nape alieleza kuwa wanachokisema majukwaani sio utashi wao, bali ni taratibu za chama hasa suala la barua na hilo la siku 90.

“Hili la barua wanalisema sana na lile la siku 90, hizo siku 90 kikatiba ni muda wa kufanyika kwa vikao vya NEC kutoka kimoja kwenda kingine, hivyo hiki tunachokisema hatukukitoa mbinguni kiko kwenye Katiba yetu. Sisi tumeziweka hivyo kwa kuwa kwenye kikao kijacho Sekeretarieti ni lazima tutoe taarifa ya yatokanayo na kikao kilichopita na mojawapo hilo suala la ufisadi,” alisema Nape.

“Hawa wamekosa hoja za kuzungumza, ni vyema wakaondoka kuliko kujadili na kupindisha mambo ambayo yako kwenye taratibu za chama,” alisema mwanasiasa huyo machachari.

Wednesday, April 27, 2011

CHADEMA yakana kubeba mafisadi

-Mbowe asema hana mahusiano na watuhumiwa
WAKATI watuhumiwa wa ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakielezwa kuwa wanajipanga kupinga uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa kuwataka wajiuzulu au watimuliwe, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekana kutumika kuwabeba watuhumiwa hao.

Watuhumiwa ambao sasa wanaelezwa kujipanga kupinga hadharani maamuzi hayo ya NEC kwa maelezo kwamba hicho si kikao kilichowachagua, ni Andrew Chenge na Rostam Aziz, ambao tayari wameenguliwa katika Kamati Kuu lakini wakabaki na nafasi nyinginezo ikiwamo ujumbe wa NEC; na Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa NEC.

Taarifa zinasema ukiacha mkakati wao binafsi, kuna uwezekano kuwa watatumia ‘vinywa’ vya baadhi ya taasisi zenye mafungamano na dini, baadhi ya waandishi wa habari na viongozi kadhaa vyama vya siasa ndani na nje ya CCM.

Habari zinaeleza kwamba sikukuu ya Pasaka inayoanza wiki hii inatarajiwa kutumika kufanya vikao maalumu mkoani Arusha, ambako watu kadhaa wamealikwa kushiriki.

“Sasa mstari wa mapambano umechorwa, ni mpambano upande wa wanaotakiwa kung’oka dhidi ya wale wanaoshinikiza uamuzi wa NEC wa kuwang’oa utekelezwe,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Taarifa zinasema katika moja ya sura za mkakati huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa, anatajwa kutumiwa bila kujua na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, walio karibu na Lowassa, kutekeleza malengo ya watuhumiwa hao wa CCM.

Tuhuma za kutumiwa kwa Dk. Slaa na CHADEMA zimekwishakuanza kuwekwa hadharani na viongozi wapya wa CCM, akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC ya chama hicho, Nape Nnauye, ambaye katika mkutano uliofanyika viwanja vya Mwembe-Kisonge Zanzibar, mwanzoni mwa wiki, alisema mkakati huo wa watuhumiwa unahusisha baadhi ya vyama vya siasa, magazeti na asasi za dini kujibu mapigo.

“Tumewapa miezi mitatu watuhumiwa wote wa ufisadi katika chama chetu wajiondoe wenyewe. Baadhi wanajaribu kupinga na kujibu mapigo kwa kutumia magazeti, vyama vya siasa na taasisi za dini...tunajua tutashinda na wao lazima waondoke.

“Tumeandaa mkakati wa kusafisha chama kutoka ngazi za chini mpaka katika ngazi ya Taifa. Tumechunguza na tunajua wanaotakiwa kuondoka ndani ya chama chetu. Lakini baadhi ya watu wamejitokeza kutaja majina ya watuhumiwa ndani ya chama chetu; hiyo si kazi yao,”alisema Nape.

Hayo yakiendelea, taarifa zaidi zinaeleza kuwa watuhumiwa hao wanatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa habari kueleza sababu za kutokukubaliana na uamuzi wa NEC.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, alisema chama chake hakina uhusiano wowote na mafisadi na hakina mpango wa kushirikiana nao.

“Huo ni umbea wenye lengo na dhamira chafu ya kuvuruga CHADEMA. Ni wajibu wetu kuibua mafisadi kwa kadiri tunavyopata ushahidi. Tulianza 2007 na tutaendelea kwa awamu,” alisema na kuendelea:

“Binafsi sijawahi kuwa na uhusiano na mtuhumiwa yeyote wa ufisadi zaidi ya uhusiano wa shughuli za Bunge.”

Taarifa hizo zinabainisha kuwa mkutano huo na wanahabari ni sehemu ya mkakati ambao umetanguliwa na mikutano ya baadhi ya vyama vya siasa kuwataja viongozi wengine wa CCM kuwa ni mafisadi ili kuongeza wigo wa watuhumiwa.

“Kutokana na kazi ya utangulizi ya baadhi ya vyama vya siasa, hasa kimojawapo kilichojizolea umaarufu siku za karibuni kwa kuwataja mafisadi wapya, watuhumiwa hao sasa watafanya press conference kueleza kuwa si wao pekee wanaotajwa kuwa mafisadi, kwa hiyo ama wabaki ndani ya chama au kama wanaondoka waondoke na wengine wanaotajwa,” anaeleza mwananchi mmoja anayejitambulisha kwa jina la Fareed akiwasilisha mawazo yake katika mtandao.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, mbali na CHADEMA, vyama vingine vinavyotajwa kuhusishwa kwenye mkakati huo ni CUF, NCCR-Mageuzi, UDP, TLP na DP.

“Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, ameingizwa mkenge na wanasiasa wenzake kuitoa orodha mpya ya mafisadi, bila kujua kuwa mpango huo umepikwa.

“Wafuasi wa watuhumiwa hao kwa kutumia watu wa CHADEMA ambao wako nao karibu wamemuingiza mkenge Dk. Slaa aitoe list of shame (orodha ya fedheha) mpya ili kuleta mvurugano ndani ya CCM.

“Siyo coincidence hata kidogo kuwa CHADEMA waliibuka na orodha yenye majina mapya siku chache tu baada ya CCM kuwataka kina Rostam, Lowassa na Chenge wajiuzulu.

“Inaeleweka wazi kuwa Rostam na Lowassa wako karibu sana na baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani na wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nao.

"Wanachotaka kufanya ni kuibua tuhuma mpya za uongo dhidi ya Kikwete, Magufuli, Malecela, Sitta, Mwakyembe, Sumaye na viongozi wengine wa CCM wajitetee kwenye vikao vya NEC vijavyo kwa kusema kuwa mbona kuna viongozi wengine CCM wenye tuhuma, lakini wanatakiwa wajiuzulu wao tu," anasema mwananchi huyo akinukuu wapambe wa watuhumiwa.

Katika hatua nyingine, inaelezwa kuwa Sekretariati ya CCM imekwisha kuandaa barua kuwataarifu watuhumiwa hao kujiuzulu kama ambavyo uamuzi wa NEC unavyotaka.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika barua watakazoandikiwa hawatapewa nafasi ya kuzijibu isipokuwa kutaarifiwa rasmi kuhusu uamuzi wa NEC.

Nape anasema viongozi waliotajwa ni sehemu ya wajumbe wa NEC ambao walikuwamo katika kikao kilichofikia uamuzi huo na kwa hiyo walikubaliana na uamuzi wa kikao.

Katika mikutano kadhaa iliyokwisha kufanyika mara baada ya hatua ya wiki iliyopita ya kile kilichoitwa “kujivua gamba” mjini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amekwisha kuweka bayana kuwa chama hicho kilifanya makosa katika kujisimamia na kuonekana ni chama cha wafanyabiashara na hivyo kupoteza sifa ya kuwa chama cha wanyonge.

Akizungumza wiki hii mjini Zanzibar, Nape kwa upande wake alisema uamuzi wa chama hicho kuwapa miezi mitatu wajumbe wa NEC wanaotuhumiwa kwa ufisadi, hauna maana ya kuwaogopa bali ni utaratibu uliowekwa.

“Msiwe na wasiwasi; ni kama kumvua pweza baharini, akifika nchi kavu unamtandika mikwaju kisha mnampika baada ya kulainika na ndivyo tafsiri ya muda waliopewa,” alisema Nape.

Nape alikilinganisha na kitendo cha kujivua gamba kwa CCM na kuwasha mwenge unaomulika kwenye chuki, pasipo na matumaini, pasipokuwa na nidhamu na kupaweka sawa na kwamba mwenge huo hautazimika.

Lakini akizungumzia jinsi watuhumiwa hao wanavyojihami Nape alisema:

“Tunazo taarifa kwamba baadhi ya watu waliotoswa katika chama chetu wameanza kutumia magazeti. Tunawaambia hawatashinda vita hiyo; CCM ni chama kikubwa na makini.”

Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Chiligati, amewataka wanachama wanaojiona wamechafuka ama kwa tuhuma za ufisadi kuanzia ngazi ya matawi, majimbo, wilaya, mikoa na kwenye NEC wajiondoe kwenye nyadhifa zao.

Chiligati alisema anawashangaa wanaobeza uamuzi wa NEC kujiuzulu kuwa wajaribu katika vyama vyao, kama havikusambaratika, kwani ni uamuzi mgumu ambao CCM iliuchukua na imevuka salama.

“Kuachia ngazi ni jambo gumu sana na si la kubeza hata kidogo; tumelazimika kujiuzulu kukinusuru chama, ingelikuwa vile vyama vingine mngevisikia vimesambaratika … wajaribu waone,” alisema Chiligati.

Kwa upande wake Msekwa, mbali ya kuelezea historia ya “kujivua gamba” kwa chama hicho, alielezea mpango mkakati wa CCM katika kujenga chama kipya chenye matumaini kwa Watanzania.

Thursday, April 21, 2011

GUIDELINES and CONCEPT NOTE FOR PERFOMANCES AND PRESENTATIONS DURING GENDER FESTIVAL 2011 PLENARY & WORKSHOP

TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME
GENDER FESTIVAL 2011

GENDER DEMOCRACY AND DEVELOPMENT:
LAND, LABOUR & LIVELIHOODS!

GUIDELINES and CONCEPT NOTE FOR PERFOMANCES AND PRESENTATIONS DURING GENDER FESTIVAL 2011 PLENARY & WORKSHOP

1. Background to the Festival!
1.1. About the Organisers

The Gender Festival is coordinated by the Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) and the Feminist Activist Coalition (FemAct), working together with other partners, including intermediary gender networks at district level and the many grassroots outreach groups who are part of the Gender and Development Seminar Series.

Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) is an activist non-governmental organisation advocating for feminist social transformation that leads to gender equality and equity, women’s advancement, social justice, and access to and control over resources by women, youth and other marginalised groups. The organisation works to build a transformative feminist social movement that can contribute towards achieving a transformed society characterised by gender equity, women’s empowerment, democracy, human rights and social justice.

The Feminist Activist Coalition (FemAct) is a coalition of over 40 non-governmental organisations that has been working for social change in Tanzania and beyond since 1996. The coalition aims to develop, strategise, and implement a collective activist agenda for progressive and gender-focused transformation of economic, social and political policies, processes, and programmes.

1.2 About the Gender Festival

The Gender Festival is an open forum for likeminded individuals and organisations to come together to share experiences and knowledge, to celebrate achievements and assess challenges ahead, to strengthen networking and coalition-building, to build capacity and to contribute to public debate and plan collectively for social change from a feminist perspective.

The Festival provides the space, and opportunity for more than 2000 activists interested in women/feminist movement building, from all walks of life, to come together from all over the country and outside. This four-day event integrates analysis, research, activism, capacity development, strategic planning and art with effective and dynamic results.

Individual organisations and/or networks are invited to ‘claim’ and organise the separate workshops within the proposed workshop framework because of limited space for new themes. Abstracts submitted should be no more than 1page. They can be written in either English or Kiswahili, using accessible language.

Culture and art are the most powerful vehicles of transmitting ideologies and they are used effectively by both the dominant cliques we oppose and the transformative feminist movement and all those who are agitating for change. They are at the centre of any communication/advocacy strategy and consciousness raising works of underground movements. Participants are invited to share in plenary and in workshops their own art productions: such as works of fiction, cartoons, plays, poetry, songs, dance, films, pop culture, etc which are used to decentre and challenge mainstream culture and male dominated creative enterprise, so as to radically change the collective psyche of society.

1.3 Gender Festival 2011

The overall theme of the 10th Gender Festival is: Gender, Democracy and Development: Land, Labour and Livelihoods!

The present theme – ‘Land, Labour and Livelihoods’ – builds on the themes that have guided earlier Festivals, while retaining the broad emphasis on Economic Justice. This year’s Festival focuses on the specific struggles and initiatives of grassroots, marginalised women and their organisations and coalitions around Land, Labour and Livelihoods in the context of neo-liberalism and patriarchy.

The new scramble for African resources, including land, water, forests, minerals, oil and natural gas, by multinational corporations and their governments is threatening the livelihoods and welfare of the majority of people, and women most of all. International Financial Institutions including World Bank and IMF, along with other donors, continue to impose neo-liberal conditionalities on African governments. Feminist and other panAfrican activists demand an alternative macro-economic framework so as to liberate Africa economically and politically. The transformative feminist movement is in the front line of this struggle, because marginalised women are the most exploited and oppressed, and the most radical in linking private and public struggles into one broad movement for change.

1.4 Festival Format

The Festival is composed of a combination of plenaries, sub-plenaries and workshops focusing on the following major areas:

The themes for the Gender Festival 2011:
The Gender Festival is organised around one key theme at plenary level, with sub-themes at workshop level. Participants will choose which workshop to attend according to their personal interests. Day One includes the Opening of the Gender Festival, with a focus on the main theme for the day, and the launch of the Gender Exhibition.

The plenary sessions provide the conceptual framework for the day. They are held every morning with a variety of short (15 minutes) art and literal presentations. During the second and third day afternoon workshops will be organised on relevant skills building for strengthening advocacy, organising and movement building initiatives. These will include workshops on: writing, feminist performance (music, poetry, dance, and drama), media usage, ICT, organising skills, action oriented research skills, fundraising and canvas art.

Day One – 13th September 2011:

Morning Plenary: Opening of Gender Festival 2011
Conceptualisation and Focus of the Gender Festival: Women Struggles over Employment, Livelihoods and Labour
Afternoon Plenary Discussion: Burning Issues

Discussants should focus on the employment and livelihoods conditions in the formal and informal sectors and their implications for the rights and power of marginalised women and the community concluding at national levels. This includes access to employment in the formal/informal sectors, equitable returns, employment benefits, types of employments available to women compared to men; the care economy in the market, state and family, including paid and unpaid work, with a focus on home based care for people with chronic disease; and appreciation and respect for women’s labour. We say the right to livelihoods and a liveable income, are a human right!

Day Two – 14th September 2011:

Morning Plenary: Women Struggles Over Means To (Self) Employment And Livelihoods: Land, Water, Physical Space & Markets
Discussants should focus on the practical inputs that are needed to enable women to not only own the land, but use it for agriculture or otherwise. Education, good health, materials and conducive environments are but a few of the means to enable (self) employment towards a dignified sustainable livelihood. the livelihoods of many women and their communities have been swept away by land-grabbing for production of food and bio-fuels for export. This takes us back to the 1980’s and the Structural Adjustment Programmes but even before that where societal order was disrupted in the last stages of the pre-colonial era and the colonial era itself. Education, health, access to resources and control over resources are central if women are to be empowered to be economically independent, and provide for their needs and that of their families. We say the means to employment and livelihoods, are a human right!

Mid Day Workshop Themes:

• Struggles over Natural Resources and their Use in the context of ‘land-grabbing’
• Struggles Over People Centred Constitutions in Africa
• Sex, Sexuality, Bodily Integrity, Politics of Choice and struggles against GBV in the workplace public and private
• Politics of Trade, Aid and Debt at all levels
• Economic Independence of Women: Challenges, Strategies, towards a full employment policy
• Women workers/producers organising for wages and incomes in paid and unpaid work through labour unions, support groups, ‘circles’, grassroots women’s groups and community based activism

Afternoon Skills Building Sessions for Organising and Movement Building: Media Usage, Writers Forum, Analysis and Research, Organising, Canvas art, Fundraising, Infotainment, Photo gallery, ICT.

Day Three – 15th September 2011:


Morning Plenary: Women Struggles Over Wages, Incomes, Working conditions, Social/Economic Security & Wellbeing
The day will focus on examples of movement strategies and outcomes from grassroots to regional level. Achievements, lessons learnt and challenges on from building women’s movement on economic justice. Discussants should ask themselves, why do people work? Employment is a means to life, therefore women who are at work should work without fear of being harassed, and have a sense of personal fulfilment. This is employment either in the formal and informal sectors, paid and unpaid labour. We say Dignity and Work are a human right!

Mid Day Workshop Themes:


• Struggles over Natural Resources and their Use in the context of ‘land-grabbing’
• Struggles Over People Centred Constitutions in Africa
• Sex, Sexuality, Bodily Integrity, Politics of Choice and struggles against GBV in the workplace public and private
• Politics of Trade, Aid and Debt at all levels
• Economic Independence of Women: Challenges, Strategies, towards a full employment policy
• Women workers/producers organising for wages and incomes in paid and unpaid work through labour unions, support groups, ‘circles’, grassroots women’s groups and community based activism

Afternoon Skills Building Sessions for Organising and Movement Building: Media Usage, Writers Forum, Analysis and Research, Organising, Canvas art, Fundraising, Infotainment, Photo gallery, ICT.

Day Four 16th September 2011:

Morning Plenary: Strategies for Feminist Organising and Movement Building for Women’s Access and Control over Land, Labour and Livelihoods

The workshops during this day will focus on the ‘Way Forward’ how do we carry on the discussions of the first three days? How do we take back the skills that we have learnt to our respective communities/groups? How do we improve on existing work based on the discussions of the first three day? Economic development and national growth prioritise export-oriented growth with little or no regard to employment and livelihoods; big investors are given priority over micro and small scale producers, a large proportion of whom are women; the entire society depends on women’s and children’s unpaid labour with little or no resource support. We say livelihoods, are a human right!

Mid Day Workshop Themes:


• Struggles over Natural Resources and their Use in the context of ‘land-grabbing’
• Struggles Over People Centred Constitutions in Africa
• Sex, Sexuality, Bodily Integrity, Politics of Choice and struggles against GBV in the workplace public and private
• Politics of Trade, Aid and Debt at all levels
• Economic Independence of Women: Challenges, Strategies, towards a full employment policy
• Women workers/producers organising for wages and incomes in paid and unpaid work through labour unions, support groups, ‘circles’, grassroots women’s groups and community based activism

Afternoon Plenary: Action, Strategies and Demands

Gender Festival Objectives

1. Generating, reflecting and sharing knowledge on Land, Labour & Livelihoods;
2. Celebrating the power of our numbers and strengthen alliances towards collective movement for economic justice and women’s empowerment across social sectors at all levels of society;
3. Enhancing our position as women/feminist activists building on participants’ own experiences and knowledge
4. Documenting and sharing feminist struggles and contributions to the public debate on Land, Labour & Livelihoods; and
5. Networking, sharing information and having fun!

The Cross –cutting Themes which thread through all workshops:

1. Analysis/experiences of Transformative Feminist Movement Building, including feminist participatory leadership and organising styles, in the context of the pan African movement
2. Global Financial and Economic Crisis and the Search for an Alternative to Neo-liberal Macro Economic Policy
3. Politics of culture and ‘tradition’ and Impact of Religious Fundamentalism and Traditionalism on Women’s Lives

4. Looking at employment and livelihoods, both formal & informal, paid and unpaid, at all levels
5. Power and voice in decision-making at all levels about resources, policies, strategies, budgets, expenditures in both private and public spheres; including access to, ownership and control over productive resources
6. Lessons learned about organising and movement building at all levels

2. General Guidelines:

2.1 Plenary Sessions

Prepare a paper, case study, video, art performance, visual art or cultural expression
• Performances and Presentations should address a relevant plenary theme by addressing the entire question or an aspect or angle therein
• Performances and Presentations should be focused on women/feminist movement building and people-centred gender, democracy and development issues
• Indicate the relevance of the presentation at local, international and/or regional levels.

2.2 Workshop Coordination (Workshop Coordinators are welcome to request an additional theme as long as it coincides with the plenary theme of the day)

• Each workshop is expected to be organised in such a way as to encourage a high level of participation from all. Workshop organisers are therefore encouraged to use a variety of methods for organising presentations and discussion. These might include any of the following methods, alone or in combination:
• Skit/video/artistic and cultural expressions and discussion
• Panel presentations
• Presentation of two full papers [maximum 10 min each], including participants interaction, followed by discussion
• A debate for and against a motion, followed by discussion
• Small group work
• The workshop organiser is responsible for coordinating the workshop, identifying potential co-presenters, and developing the workshop plan, which will be shared with the Secretariat. The workshop organiser will follow-up to ensure that all papers/presentations are submitted on time, according to the deadline dates to be shared, and for ensuring that the Secretariat has received the final copy in hard print and on diskette. The workshop organiser will liaise with the Secretariat on a regular basis.
• Workshops coordinated should address a relevant sub-theme by addressing the entire question or an aspect or angle therein
• Presentations and performances should reflect on the current situation and strategies
• Performances and Presentations should be focused on women/feminist movement building and people-centred gender, democracy and development issues
• The secretariat provides a venue for workshops, including chairs, tent and public speaking devices. Other costs of workshops are the sole responsibility of workshop organisers and other presenters. The secretariat will not be providing honorarium, therefore, for organising a workshop, or for preparation of individual papers or skits. However, the secretariat will be responsible for reproducing enough copies of paper abstracts to share with participants in a given workshop.

3. Process and Timeframe:

Papers, case studies and workshops for facilitation will be selected utilising the following process:

3.1 Those interested should prepare an abstract for a paper, case study, performance or workshop to be coordinated in one of the relevant sub-themes following the guidelines stipulated above. The abstract should be submitted to TGNP by June 30th, 2011, at the latest. All are requested to specify which day their inputs are intended for and to which sub-theme their abstract relates. All are also requested to give an indication of how a workshop around their paper and case study should be facilitated to achieve the desired output.

3.2 If your paper, case study or workshop is selected to be presented or facilitated at the conference you will be informed by 8th July 2011. You will then need to complete the paper (and abstract, if relevant) or final workshop description by 10th August 2011 at the latest, so as to allow time for reproduction of all papers, and translation of plenary papers and of all abstracts.

Gender Festival 2011 General Announcement

Dear Members, partners and supports of the African Feminist Movement,

Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) and Feminist Activist Coalition (FemAct) are pleased to announce the 10th Gender Festival (Tamasha la Jinsia) which will focus on Land, Labour and Livelihoods within the broad theme of Gender, Democracy and Development. The Festival will take place from the 13th – 16th September.

Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) is an activist non-governmental organization advocating for feminist social transformation that leads to gender equality and equity, women’s advancement, social justice, and access to and control over resources by women, youth and other marginalised groups. The organisation works to build a transformative feminist social movement that can contribute towards achieving a transformed society with high sensitivity to issues of gender, democracy, human rights and social justice.

The Feminist Activist Coalition (FemAct) is a coalition of over 40 non-governmental organisations that has been working for social change in Tanzania and beyond since 1996. The coalition aims to develop, strategise, and implement a collective activist agenda for progressive and gender-focused transformation of economic, social and political policies, processes, and programmes.

Building on ongoing efforts towards transformative feminist movement building, this year’s Gender Festival will be organised in a more creative way in order to widen ownership and encourage originality. The main theme, plenary themes and workshop themes have come through our interaction and consultations with key partners and activists from grassroots, national, regional and international levels. The Gender Festival will therefore also be space for sharing ongoing struggles for women/ feminist movement building at all levels.

The present theme – ‘Land, Labour and Livelihoods’ – builds on the themes that have guided earlier Festivals, while retaining the broad emphasis on Economic Justice. This year’s Festival focuses on the specific struggles and initiatives of grassroots, marginalised women and their organisations and coalitions around Land, Labour and Livelihoods in the context of neo-liberalism and patriarchy. The transformative feminist movement is in the front line of this struggle, because marginalised women are the most exploited and oppressed, and the most radical in linking private and public struggles into one broad movement for change.

Gender Festival Objectives are to provide space for:

1. Women/feminist and human rights activists to generate, reflect and share knowledge on Land, Labour & Livelihoods;
2. Celebrate the power of our numbers and strengthen alliances towards collective movement for economic justice and women empowerment across social sectors at all levels of society;
3. Enhancing our position as women/feminist activists building on participants’ own experiences and knowledge
4. Documenting and sharing feminist struggles and contributions to the public debate on Land, Labour & Livelihoods; and
5. Networking, sharing information and having fun!
Community activists, women/feminist groups, Community Based Organisations, Non Governmental Organisations and coalitions are highly encouraged to use the Gender Festival space creatively to coordinate a workshop, present/perform during the plenary sessions and exhibit in relation to the themes and subthemes of the Festival. TGNP and FemAct encourage the use of artistic and literal presentations equally.

Why Transformative Feminist Movement Building & Why Now?

Transformative feminism concerns the struggles for liberation of girls/women in both private and public spheres from patriarchy and neo-liberalism, and their efforts to create entirely new forms of gender and class relations in which both women and men live and are able to fulfil themselves in all their potential. Transformative feminism links struggles of women and men against all major forms of exploitation, oppression and discrimination, including male domination, class exploitation, imperial domination, racism, ethnicism, fundamentalism, traditionalism, and discrimination on the basis of disability, HIV, age and gender identity.

Transformative feminists believe that change is possible, and this belief provides them with hope in the midst of despair. Transformative feminism is rooted in the unity between theory and practice, analysis and action. Feminists highlight the power of personal reflections on individual/collective experiences of struggle as well as more systematic analysis and research about structures, systems and struggles. Transformative feminists deliberately adopt cooperative styles of work to challenge the competitive nature of capitalist society. Alternative ways of organising, producing and communicating are developed so as to support one another and to nurture new recruits to transformative feminist theory and practice.

Festival Format
Plenary sessions are held every morning to provide the conceptual framework for the day.
Day One: Opening of Gender Festival 2011 & Conceptualisation and Focus of the Gender Festival: Women Struggles over Employment, Livelihoods and Labour
Day Two: Women Struggles Over Means To (Self) Employment And Livelihoods: Land, Water, Physical Space & Markets
Day Three: Women Struggles Over Wages, Incomes, Working conditions, Social/Economic Security & Wellbeing
Day Four: Strategies for Feminist Organizing and Movement Building for Women’s Access and Control over Land, Labour and Livelihoods

Separate workshops will be organised from day two on the following subthemes:
• Struggles over Natural Resources and their Use in the context of ‘land-grabbing’
• Struggles Over People Centred Constitutions in Africa
• Sex, Sexuality, Bodily Integrity, Politics of Choice and struggles against GBV in the workplace public and private
• Politics of Trade, Aid and Debt at all levels
• Economic Independence of Women: Challenges, Strategies, towards a full employment policy
• Women workers/producers organising for wages and incomes in paid and unpaid work through labour unions, support groups, ‘circles’, grassroots women’s groups and community based activism

During the second and third day afternoon workshops will be organised on relevant skills building for strengthening advocacy, organising and movement building initiatives. These will include workshops on: writing, feminist performance (music, poetry, dance, and drama), media usage, ICT, organising skills, action oriented research skills, fundraising and canvas art.

You and your organization/ group can participate in the Festival through:
• Preparing presentation of different kinds (papers, poetry, video, song, art performance) or organizing a workshop panel or debate relating to the various sub-themes above;
• Coordinating a workshop or skills building session;
• Mobilising and facilitating a large group from your country, region, area, constituency or organization to attend and contribute at the festival;
• Creating an interactive exhibition that may include publications, photographs, appropriate technology materials, handcraft and others;
• Preparing Artistic Performances related to Festival themes;
• Active attendance and contributions during the Festival;
• Financial contribution and fundraising to support specific events; and
• Other forms of contribution to enhance the festival.

Please communicate to us as soon as possible your organization’s proposed contribution to the festival so that we can include you in the plan and the programme. Ideas for additional sub-themes related to the broad theme are also welcome. To present a paper, prepare a case study, or facilitate a workshop, please refer to the guidelines for papers, case studies and workshops which will soon be available online at www.tgnp.org. We also welcome suggestions and innovative ideas for ways to organize, coordinate and conduct this year’s festival.

Participation is open to all interested organizations and individuals, who are encouraged to fundraise for their participation (registration fee and other related costs will be available on TGNP website soon). In order to secure funding, TGNP can provide letters of invitation to support fundraising endeavors. Early registration and notification of envisaged role in the event will be highly appreciated as it will ease registration process for both TGNP and yourself. You can also register online at www.tgnp.org

The official languages of the festival will be Kiswahili and English.

We look forward to your communication with the Gender Festival organizing team, based at the Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) through info@tgnp.org (subject: GF 2011) or gf_coordinator@tgnp.org


Sincerely,


Ms. Mary Rusimbi,
Chairperson TGNP

&

Ms. Jesca Mkuchu,
Chairperson FemAct

Atunukiwa tuzo ya kimataifa ya Mwanamke Jasiri

UBALOZI wa Marekani nchini, umemtunuku Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya kutetea haki za mwanamke ya Kivulini Women’s Rights Organization ya Mwanza, Maimuna Kanyamala Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri ya mwaka 2011.

Akizungumza kabla ya kumkabidhi tuzo hiyo Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alisema ubalozi wake umemtunukia Kanyamala kutokana na kujielekeza katika kutetea haki za wanawake hususani katika kusisitiza kuweka mazingira ya mazuri ya kuishi wanawake katika jamii ni kuondokana na vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Katika kutimiza majukumu yake, alikutana na changamoto nyingi sana kutoka kwa jamii, wakipinga kampeni za kuhamasisha jamii kupata uelewa, Kanyamala amekumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wake katika ukanda wake walikuwa wanamtuhumu kuwa ni chanzo cha ‘kuwavimbisha vichwa wanawake’ na ni ‘mpinzani wa wanaume,” alisema Balozi Lenhardt.

Aidha, Balozi Lenhardt alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia ni tatizo kubwa ulimwenguni na kuwa nchi yake imejikita kusaidia zaidi ya Dola za Marekani milioni saba kwa ajili ya kupunguza ubaguzi wa kijinsia na vitendo vya kikatili kwa Tanzania.

Kanyamala anakuwa ni mwanamke wa nne kutunukiwa tuzo hiyo iliyoanzishwa kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke aliyeonesha ujasiri wa kiwango cha juu na uongozi mzuri katika kutetea masuala ya haki za wanawake.

Wengine ni Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya kwa mwaka 2010, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (2009) kutokana na ujasiri aliouonesha katika kukosoa na kuupa changamoto uongozi wa chama chake ili ushughulikie kikamilifu rushwa na Helen Kijo-Bisimba (2008) wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kusaidia na kuimarisha haki za wanawake.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, pamoja na Ubalozi wa Marekani kutambua mchango wa watu walio chini kabisa, Kanyamala alisema pamoja na kukumbana na changamoto nyingi, kamwe hatarudi nyuma kutetea na kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

“Tangu kuanzishwa kwa taasisi yetu zaidi miaka ya 10 iliyopita, tumekutana na changamoto nyingi, watu walifikia hata kunihoji kama vile nimeolewa na kuonekana napingana na mila na desturi na pia imani za dini za watu, lakini hayo yote hayakunifanya nirudi nyuma,” alisema mama huyo ambaye ameshawasaidia wanawake zaidi ya 2,000 katika kanda hiyo.

Naye Kilango alisema akiwa mbunge na mwanamke, atapaza sauti bungeni ili kumzungumzia kazi ya Kanyamala ambayo inatakiwa kufanywa na viongozi na pia kutoa changamoto kwa wanawake wengine kupambana na vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake.

Serikali kuvua gamba kama CCM

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema, baada ya Operesheni Vua Gamba kukamilika ndani ya chama hicho, mkakati huo utahamishiwa kwa watendaji wote wa Serikali wanaoshindwa kutekeleza Ilani ya Chama hicho.

Alisema hayo juzi wakati yeye na Naibu Katibu Mkuu CCM, Bara, John Chilligati waliposalimia wananchi wa Iringa Mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika nje ya ofisi kuu ya CCM ya mkoa mjini hapa.

Nnauye alisema, katika kukisafisha chama hicho baada ya Sekretarieti mpya kuundwa, viongozi wote ndani ya chama wanaotajwa kwenye kashfa kubwa zikiwamo za Richmond, Kagoda, Dowans na Rada, wanatakiwa ndani ya siku 90 walizopewa wawe wamejiuzulu nyadhifa zao.

"Tumewaambia wenzetu mnaotajwatajwa kwenye kashfa hizo, jipimeni wenyewe na kisha mwajibike, vinginevyo tutawakamata na kuwatosa kwa aibu," alisema na kuongeza, kwamba baadhi yao wamekwishaandikiwa barua za kuombwa wajiuzulu.

Hata hivyo, alisema kipimo cha nani anatakiwa kuachia ngazi ndani ya chama hicho wanacho wao wenyewe na kamwe hawatatumia kelele za chuki kutoka kwa baadhi ya wapinzani.

Nnauye alisema, Operesheni hiyo inayotarajiwa kwenda hadi ngazi ya mashina na matawi, itaingia serikalini kwa sababu wanawafahamu baadhi ya watendaji wasiotekeleza Ilani ya chama hicho zaidi ya kujaza matumbo yao.

Alisema, kufanikiwa kwa Operesheni hiyo kutakiwezesha chama hicho kuingia katika uchaguzi wake mkuu ujao na wa Serikali wa mwaka 2015 kikiwa na sura za viongozi waadilifu na kurudisha imani kwa wananchi.

Chilligati aliwataka viongozi waliosababisha chama hicho kupoteza umaarufu hata kukifanya kipoteze baadhi ya majimbo, kuacha kusubiri uamuzi wa kujiuzulu nyadhifa zao, ili kuwapisha wanachama wengine waadilifu na wenye uwezo kuongoza chama hicho.

"Wanaokitesa chama mpaka kinasemwa vibaya si tu kwamba wako kule kwenye NEC hata huku kwenu wapo na mnawafahamu na ndiyo maana katika uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoteza jimbo hili la Iringa Mjini kwa Chadema," alisema.

Chilligati alisema, kwa kuwa mageuzi ya sasa ndani ya chama hicho yanataka kukirudisha kwa wanachama wenyewe, viongozi watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo yatakayowawezesha kufanya kazi za siasa kwa wanachama wanaowachagua.

"Pamoja na mkutano huu, kubwa lililotuleta hapa Iringa ni kumkabidhi Nnauye Chuo chetu cha Siasa cha Ihemi ili akijenge upya," alisema.

Alisema chuo hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Iringa, kitatumika kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi zote watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa chama hicho, mwakani.

Shughuli za kumkabidhi Nnauye chuo hicho zilifanyika jana chuoni hapo.

Wednesday, April 20, 2011

TAMKO LA TGNP KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA

TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME (TGNP)
P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road, Tel. 255 22 244.3450/ 244.3205/ 244.3286; Mobile 255 7 0754 784050/ 0754 788706; Fax 255 22 244.3244; Email info@tgnp.org; Website www.tgnp.org


Aprili 18, 2011
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba uandikwe upya
Mtandao wa Jinsia Tanzania tumeupokea uamuzi wa Bunge wa kusogeza mbele muda wa kuujadili muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba wa 2011 kwa masikitiko makubwa.Uamuzi wa Bunge unaoitaka serikali kuufanyia marekebisho muswada huo na kuutafsiri kwa Kiswahili ni wamsingi ingawa una mapungufu. Tulitarajia kwamba Bunge lingeishauri waziwazi serikali kuuondoa muswada huo Bungeni na kuanzisha mchakato shirikishi wa kutunga muswada mpya.
Kwa hiyo, tunaunga mkono msimamo wa wananchi wanaoitaka serikali kuandaa muswada mpya unaozingatia maoni ya makundi mbalimbali ya wananchi.

Tunapenda kusisistiza msimamo wetu kwamba wananchi hawapaswi kutungiwa sheria ya kuanzisha mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya na chombo chochote kabla hawajajadiliana na kukubaliana juu ya dira, tunu na maadili ya Taifa lao. Msingi wa madai yetu ni mapungufu makubwa yaliyomo kwenye muswada wa marejeo ya katiba wa 2011 uliowasilishwa na serikali Bungeni kwa hati ya dharura. Muswada huu ulitungwa na serikali kabla ya kuanzishwa kwa mjadala wa kitaifa na ndio maana ulikuwa na kasoro nyingi zisizokubalika na watu wengi waliopata wafursa ya kuusoma na kutoa maoni yao.

Tunasisitiza kwamba, mjadala wa kujenga muafaka wa kitaifa unapaswa kuutangulia mchakato wa kisheria wa kutunga katiba mpya. Mjadala wa Kitaifa ndio utakaoainisha: wigo wa uwakilishi wa makundi mbalimbali; sifa za wajumbe wa mkutano wa kitaifa wa katiba na kazi zake; sifa za wajumbe wa tume huru ya katiba na hadidu za rejea za tume hiyo; sifa za wajumbe wa Bunge la




Katiba, muundo na kazi zake; na utaratibu wa kuandaa na kusimamia kura ya maoni.
Ili mjadala huo uwe na tija, wananchi wanahitaji muda wa kutosha wa kujadiliana na kukubaliana kwanza juu ya dira, misingi ya kisiasa na kiuchumi na maadili ya taifa lao. Vilevile serikali inahitaji muda wa kutosha wa kukusanya maoni ya wananchi na kuyachambua kabla ya kuandaa sheria ya kusimamia mchakato wa kutunga katiba mpya. Kazi ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa inapaswa kufanywa na chombo huru kinachoundwa na wataalamu wenye misimamo thabiti na sio vyombo au taasisi za dola. Tunaitaka Serikali kuheshimu maamuzi ya wananchi yatakayotolewa wakati wa mjadala huo. Tunasisitiza kwamba maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayozaa sheria nzuri ya mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya.


Tunalitaka Bunge kutimiza wajibu wake wakikatiba kwa kuishauri Serikali juu ya namna bora ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa ili wananchi wote waweze kushiriki kwa amani,utulivu na kuvumiliana. Bunge linapaswa pia kushirikiana na serikali katika kuweka mazingira muafaka ya kisiasa na kisheria ili mchakato wa kutunga katiba ukamilike kwa mujibu wa matarajio ya watanzania wote. Tunawataka wanasiasa wote kutambua wajibu wao wa kutetea maslahi ya taifa na kuepuke kuweka mbele maslahi ya vyama vyao wanapowasilisha hoja zao ndani na nje ya Bunge. Ili kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia haki na wajibu wao wa kuunda katiba mpya, mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa na wadau wote wa siasa nchini:


a) Kuafikiana juu ya mfumo wa kuratibu mjadala wa kitaifa utakaoweka misingi ya kisiasa na kisheria ya kutunga katiba mpya.


b) Kuafikiana juu ya sheria ya kuunda Bunge la katiba na sheria ya kuandaa na kusimamia kura ya maoni. Sheria hizi zitatungwa na Bunge kwa kuzingatia mapendekezo ya wananchi yatakayotokana na mjadala ya kitaifa ulioratibiwa na tume huru ya katiba.


c) Kushirikiana kuweka mazingira muafaka ya kisiasa yatakayowezesha wananchi wote kushiriki katika mchakato wa kutunga katiba mpya bila hofu au kuburuzwa na kundi la watu au taasisi yoyote.


d) Bunge kutotunga sheria yoyote yenye lengo au mwelekeo wa kuchakachua mchakato wa kutunga katiba mpya katika kipindi chote cha mchakato wa kutunga katiba mpya.


e) Kuafikiana juu ya muda wa mchakato wa kutunga katiba.


f) Kuafikiana juu ya namna ya kutoa elimu kwa wananchi wote ili waweze kushiriki ipasavyo katika mchakato wa kutunga katiba.




MJADALA KWANZA, SHERIA BAADAYE!
Imetolewa Dar es salaam na
Mary Rusimbi
Mwenyekiti wa Bodi TGNP

Tuesday, April 19, 2011

Waliohojiwa Baraza la Maadili kutimuliwa

BARAZA la Maadili ya Viongozi wa Umma, limesema viongozi wa umma takribani 23 waliosimamishwa mbele yake kuhojiwa juu ya kutowasilisha matamko yao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, baada ya kuamua na kumshauri Rais, huenda wakakosa sifa ya kuwa viongozi.

Pia Baraza hilo limesisitiza kuwa kazi yake si tu kufuatilia ujazaji wa matamko ya mali na madeni ya viongozi wa umma bali kusimamia maadili ya viongozi hao na kuhakikisha kila kiongozi anazingatia maadili hayo.

Pamoja na hayo, Baraza hilo jana lilihoji na kusikiliza maelezo ya viongozi wawili wa umma ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msaidizi wa Masuala ya Siasa wa Rais, Rajab Luhwavi, ambaye wiki iliyopita alifikishwa mbele ya Baraza hilo chini ya ulinzi wa Polisi.

Akitoa majumuisho ya kazi ya Baraza hilo ya kuhoji viongozi wa umma 23, ambao wanalalamikiwa na Sekretarieti ya Maadili kwa kutowasilisha matamko yao, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema Baraza hilo limekamilisha awamu ya kwanza ya kusikiliza maelezo ya viongozi wa umma wasiowasilisha matamko yao kwa Sekretarieti ya Maadili ambao wasipoangalia wanaweza kupoteza uongozi.

“Napenda ifahamike kuwa Baraza hili kazi yake si kushughulikia kutojaza fomu za matamko ya mali na madeni ya viongozi, tunazo kazi nyingi za kushughulikia za uvunjifu wa maadili na hawa tunawahoji, inawezekana wakakosa sifa za kuwa viongozi lakini kwa sasa tutazingatia utetezi wao na kumshauri aliyetutuma kwa hatua zaidi,” alisema Lubuva.

Aidha, alisema viongozi wengi waliohojiwa na Baraza hilo wametumia utetezi wa kutotumiwa barua na fomu za matamko na Sekretarieti ya Maadili, jambo ambalo si utetezi unaokubalika, kwa kuwa Sheria ya Maadili namba 13 ya mwaka 1995 inatamka wazi kuwa ni wajibu wa kiongozi kujaza yeye binafsi fomu hizo na kuziwasilisha kwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma.

Pia alivitaka vyombo au taasisi kama vile halmashauri za wilaya ambazo hupokea barua na fomu za viongozi wa umma, kwa jumla na kuwasambazia, kuhakikisha kuwa kila kiongozi amepata fomu yake, kujaza na kuirudisha, vinginevyo lawama za kutojaza fomu zinaweza
kuangukia vyombo au taasisi hizo.

“Tumekutana na kesi za aina hiyo katika mashauri tuliyosikiliza, ndiyo maana tunasema tutazingatia kesi kwa kesi na mazingira yake, lakini suala la kujaza hizi fomu, ieleweke kuwa ni wajibu wa viongozi wenyewe kwa kuwa wao ndio waliapa na kuahidi kuwajibika,” alisema.

Awali Mukandala akijijitea mbele ya jopo la Baraza hilo lenye majaji watatu; Lubuva, Jaji mstaafu Balozi Hamis Msumi na Katibu Mkuu mstaafu Deodatus Tibakweitira, alisema tangu ashike wadhifa huo wa Makamu Mkuu wa Chuo, hajawahi kutojaza fomu na kwamba mwaka anaodaiwa kutojaza wa 2009, ana uhakika alijaza na kuziwasilisha kunakotakiwa.

Alitoa kielelezo cha kuthibitisha kujaza na kuwasilisha fomu hizo kwa Sekretarieti ya Maadili ambacho ni barua ya sekretarieti hiyo, ya kumjulisha kupokea fomu zake ya Agosti 6, mwaka jana, na kumtaarifu kuwa watamfanyia uhakiki wa mali na madeni yake kwa mujibu wa tamko lake la mwaka 2009 ambalo anadaiwa hajawasilisha.

Mwanasheria wa Sekterieti ya Maadili, Hassan Mayunga, alidai mbele ya Baraza hilo kuwa barua aliyotumiwa Mukandala ilikosewa kimaandishi, kwa kuwa uhakiki hufanywa kwa baadhi ya viongozi na hutumiwa barua moja ambayo hubadilishwa majina na anuani tu.

Hata hivyo, timu hiyo ya mawakili pia iliendelea kudai kuwa hata tamko la mwaka 2009 alilowasilisha Mukandala baada ya kutakiwa kufanya hivyo na timu ya uhakiki kufuatia tamko lake la awali kutoonekana, nalo linaonekana kuwa na utata kutokana na tarehe ya kiapo kuwa Januari 2010 wakati tamko hilo liliwasilishwa Aprili mosi mwaka huu.

Luhwavi katika utetezi wake, alidai mbele ya jopo hilo kuwa tangu kushika kwake wadhifa wa Naibu Msaidizi wa Masuala ya Siasa wa Rais, hajawahi kupelekewa barua wala fomu za kujaza na kwamba aliwahi kufuatilia Sekretarieti ya Maadili ambao walimjibu kuwa kama yumo kwenye orodha ya viongozi wa umma, atatumiwa taarifa.

Thursday, April 14, 2011

CAG alalamika kupuuzwa na Serikali

SERIKALI haikutekeleza mapendekezo yote 15 yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2010, hali aliyoieleza kuwa inakwamisha ufanisi serikalini na katika mashirika ya umma.

CAG amelalamikia hatua hiyo ya Serikali katika ripoti yake ya mwaka 2010, iliyotolewa wiki hii na kuorodhesha mapendekezo yote aliyotoa huku akionya kuwa kudharauliwa kwake, kutasababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo.

Baadhi ya mapendekezo aliyosema hayakufanyiwa kazi ni pamoja na ushauri wa kuitaka Serikali ipunguze ununuzi wa magari ya kifahari na kupunguza gharama za warsha, ili mapato yanayokusanywa yatumike kwenye shughuli za maendeleo.

Pia alilalamikia kutotekelezwa kwa mapendekezo ya kuondoa wabunge kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, ili kuepuka mgongano wa maslahi kwa kuwa ni wabunge hao hao wanaosimamia utendaji kazi za mashirika hayo kupitia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

Mapendekezo mengine aliyolalamikia kutotekelezwa na Serikali ni kuboresha ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali, kuziba mianya ya ukwepaji kodi hususani kwenye mafuta ya magari na mitambo, kupunguza misamaha ya kodi na kupanua wigo wa kodi.

CAG alisema katika ripoti hiyo, kuwa hata alipoomba maelezo ya kina kuhusu uhalali wa malipo ya dola milioni 4.8 za Marekani kwa kampuni ya M/s Dowans kwa ajili ya kukodisha ndege maalumu, Serikali haikumpa majibu yoyote sasa yapata mwaka.

Mbali na maombi ya kupata taarifa za Dowans ambayo hayajatekelezwa, CAG alilalamikia pia ushauri wake wa Serikali kuligawa mara mbili Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC); shirika moja lishughulikie biashara na lingine litoe leseni, ukaguzi na kufanya kazi za udhibiti, ili kuleta ufanisi katika biashara ya mafuta, haukutekelezwa.

Mapendekezo mengine aliyosema yalipuuzwa ni kuruhusu Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), kusimamia hesabu za mashirika na kampuni zote ambazo Serikali ina hisa.

Mkaguzi huyo pia alipendekeza bodi za wakurugenzi za mashirika ya umma kuhakikisha watendaji wakuu wa mashirika hayo wanawajibika zaidi kwa matokeo ya utendaji kazi wao, lakini alieleza kuwa ushauri huo haujatekelezwa.

Zanzibar wataka Serikali ndogo

CHAMA cha Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kimeonesha wasiwasi juu ya ukubwa wa muundo wa Serikali na kutopangiliwa kwa idara zake na kumwomba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, kuupitia upya muundo huo.

Pia kimemwomba aangalie uwezekano wa kupunguza pengo kubwa la mshahara kati ya watendaji waandamizi na watumishi wa umma wanaoanza kazi, ili kuongeza ufanisi.

“Tunamwomba Rais aangalie ukubwa wa serikali yake, mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi kwa kuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Tunahitaji kuwa na Serikali ndogo na kuokoa fedha kwa ajili ya mishahara bora kwa wote,” alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Mwinyi Mohamed.

Khamis alitoa ombi hilo kwa Rais Shein wakati akizungumza Jumatano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, inayofanyika kila mwaka Mei Mosi huku akidai kuwa Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa kwa sasa idara zake zimekaa vibaya.

“Mahakama ya Kazi iko chini ya Mahakama Kuu, idara zinazohusika na ajira kwa watoto, usalama kazini na malipo kwa wafanyakazi zipo chini ya Wizara ya Ustawi wa Jamii, hii si sawa, idara hizi zinapaswa kuwa chini ya Wizara ya Kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema.

Alisema kutopangiliwa ipasavyo kwa idara zinazohusiana na ajira, pia kunawavunja moyo wafadhili kama vile Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kusaidia maendeleo ya ajira kwa kuwa wanadhani Serikali haiko makini.

Aidha, chama hicho pia kilionesha wasiwasi wake juu ya kupanda kwa bei ya bidhaa kutokana na kukosekana kwa chombo maalumu cha kudhibiti bei ambacho kinatakiwa kuboresha pia maslahi ya wafanyakazi na kuziba pengo la mishahara.

“Haikubaliki kwa mfano, baadhi ya wakurugenzi wanalipwa mshahara wa mwezi unaofikia Sh milioni 1.5 wakati mfanyakazi wa kawaida mwenye shahada, analipwa Sh 150,000 kwa mwezi na mshahara wa kima cha chini wa Serikali ni Sh 100,000,” alisema na kushauri kima cha chini kiwe Sh 350,000.

Wednesday, April 13, 2011

Maaskofu wapinga muswada wa Katiba

MAPENDEKEZO ya Muswada wa Sheria ya Kuongoza Mchakato wa kukusanya maoni kuhusu Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yameendelea kupingwa na sasa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limeungana na Jumuiya ya Wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA). Katika mdahalo uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, UDASA waliendesha kongamano kuhusu Katiba mpya wazungumzaji wakuu wakiwa Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samata na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga. Katika madahalo huo sehemu kubwa ya wazungumzaji walipinga mapendekezo ya muswada huo na hasa vipengele vinavyozuia mijadala ya Katiba mpya kutohoji au kujadili mamlaka Rais, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kwamba atakayefanya hivyo atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela. Kwa mujibu wa wazungumzaji hao kipengele hicho kinapingana na fursa ya sasa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa uhuru wa mijadala bila kuweka mipaka kwa kuegemea mipaka fulani na hasa madaraka. Vuguvugu hilo la wasomi kupinga muswada huo sasa linaungwa mkono na Baraza la Maaskofu Tanzania ambalo kupitia kwa Mwenyekiti wake wa Tume ya Haki, Askofu Paul Ruzoka, wamemuandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria wakipendekeza hekima itumike kuimarisha utulivu wakati wote wa mchakato wa Katiba mpya. Barua hiyo iliyoandikwa Aprili 5, mwaka huu inaeleza; “Muswada wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi wa mwaka 2011 Namba 1 wa tarehe 11 Machi, 2011 umetangazwa katika siku chache zilizopita. Baada ya kuusoma muswada huu tulishangazwa kuona kwamba mchakato wote unaanzia na kuishia kwa Rais na kwamba Chombo Kikuu cha kuratibu mchakato wote ni Tume itakayoteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala. Tunatambua kwamba kilio cha kutaka Katiba mpya kilitokana na utashi mwema na pia hasira njema ya jamii ya Watanzania wakitaka mabadiliko yaliyo na hekima na utu. Tunahofia kwamba maudhui na mwelekeo wa muswada wa marekebisho ya Katiba unaopelekwa Bungeni havitakidhi mahitaji mazito ya watu na huenda ukachochea hasira ambayo imekwisha jidhihirisha katika jamii yetu. Tunakuomba ulisimamie zoezi la marekebisho ya katiba kwa hekima sana ukiongoza tafakari jadidi na elimu angavu itakayo wezesha zoezi lote kuwa la mazungumzo ya kitaifa kweli kweli huku amani, maelewano na makubaliano vikilindwa sana katika wakati mgumu huu. Tafadhali lipatie taifa muda wa kufaa na chombo huru kinachoaminika kuongoza wananchi kufikia makubaliano yatakayojenga msingi imara wa taifa letu kwa wakati ujao,” inaeleza barua hiyo iliyosainiwa na Askofu Ruzoka.

Tuesday, April 12, 2011

Vigogo CCM watakiwa wajiuzulu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa miezi mitatu kwa wanachama wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi wajiuzulu, wakikaidi watawajibishwa.

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, amesema, wanaCCM hao wakiwemo vigogo wanapoteza haiba ya CCM katika macho ya Watanzania.

Kwa muda mrefu, wanachama kadhaa wa CCM wamekuwa wakitajwa kuhusika katika vitendo vya rushwa na wakahusishwa kwenye kashfa kadhaa ikiwemo ya uzalishaji wa umeme wa dharura ya kampuni hewa ya Richmond, kashfa ya Dowans, kashfa ya ununuzi wa rada, na kashfa ya ulipaji wa madeni ya nje kupitia akaunti ya EPA Benki kuu Tanzania (BOT) kupitia kampuni ya Kagoda.

Kwa mujibu wa Kikwete, Halmashauri Kuu ya CCM imezungumza na watuhumiwa hao wakati wa mkutano uliomalizika jana usiku mjini Dodoma, na wameelewana.

“Tusionekane kuwa ni chama ambacho vitendo vya rushwa hatuchukizwi navyo” amesema Kikwete wakati anafunga mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ulioanza juzi asubuhi.

Amesema, CCM imeanza kuchukua hatua, wanaotajwa kuhusika kwenye ufisadi na rushwa wanafahamika, hivyo wasionewe haya, wao wenyewe wawajibike, wasipofanya hivyo ‘wataoneshwa ulipo mlango’.

Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema, chama hicho kimeamua kuwashughulikia WanaCCM wala rushwa na mafisadi.

“Haogopwi mtu, na Mwenyekiti alisema, tumekusudia, tunakwenda kujivua gamba” alisema Nnauye jana usiku wakati anazungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Halmashauri Kuu kwenye jengo la White House mjini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, John Chiligati amesema, watuhumiwa hao wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wanatajwa vibaya kwenye jamii, hivyo wawajibike hata kama hakuna ushahidi.

“Tumewaambia wao wenyewe wapime, wachukue hatua za kuwajibika” amesema na kubainisha kuwa wasipotekeleza waliyokubaliana, CCM itawawajibisha hivyo wasisubiri kuoneshwa ulipo mlango.

Chiligati amewaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, kuanzia sasa, CCM ipo makini kupambana na vitendo vinavyoleta sura mbaya katika chama hicho na amewaambia watuhumiwa kuwa “ usiulize ushahidi upo wapi”

Kikwete ameishukuru iliyokuwa Kamati Kuu ya CCM kwa kukubali kujiuzulu kwa maslahi ya chama hicho kwa kuwa wameonesha wanajali maslahi ya wanachama.

Ameishukuru Kamati Kuu mpya yenye wazee na vijana wasiozidi umri wa miaka 35, na ameishukuru pia iliyokuwa Sekretarieti ya CCM iliyojiuzulu kwa ujasiri wao na kujali maslahi ya chama chao.

Kikwete amesema, anaamini kwamba, Kamati Kuu mpya itakidhi matarajio ya kuijenga upya CCM, na amesema, kuwa miongoni mwa wajumbe ni wakongwe, wawe kama panga la zamani, makali yale yale.

“Tumekubaliana, mwenzetu anayelegalega tunamwambia, mwenzetu unalegalega” amesema Kikwete akimaanisha kuwa, kuanzia sasa hakuna kuoneana haya CCM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road, Tel. 255 022 2443205/2443286/2443450; Mobile 255 0754 784050, 0715 784050; 0784 784050 Fax 255 022 2443244; Email info@tgnp.org ; web www.tgnp.org Aprili 11, 2011



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Uchambuzi wa madai ya wanaharakati kuhusu mchakato wa Muswada na Katiba Mpya ya Tanzania Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), tumekuwa tukifuatilia kwa karibu mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano Tanzania unaoendelea hapa nchini. Kwa muda mrefu sasa wananchi wamekuwa wakidai Katiba mpya ambayo itashirikisha mawazo ya walio wengi. Kwanza, tunaipongeza serikali kwa kuona kuwa wananchi wana mahitaji ya kuwa na Katiba mpya baada ya ile ya mwaka 1977 kutokukidhi haja za wakati huu na hivyo kuonekana kuwepo na mapungufu mengi. Tunasikitika kuona kwamba wakati tupo katika hatua za awali kabisa za kuujadili muswada huu, kumeibuka makundi ya wanasiasa wanaotumia mwanya huo kuvuruga utaratibu mzima wa kukusanya maoni ya wananchi. Ili Katiba iwe na uhalali wa kisiasa na mamlaka ya kusheria, wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga Katiba mpya.Katika mchakato huu ni muhimu kuwemo na demokrasia na ushiriki wa wananchi wote wanawake, wanaume,vijana, watu wanaoishi na ulemavu na watu wote walioko pembezoni ili kuleta mabadiliko chanya na pia kuleta haki na usawa kwa wote. Tunajua kuwa kama wananchi watanyamazia au watashindwa kutoa maoni yao juu ya muswada huu, itakuwa mwanzo wa kuwa na Katiba isiyo ya wananchi wote. Tumesikitishwa na makundi ya wananchi wanaokubali kutumiwa vibaya kuzomea kwenye mikutano ya kujadili muswada huu na kuleta vurugu. Pia tunalaani kitendo cha wanasiasa kuwatumia vibaya watoto wadogo wasio na uelewa wa kuchangia muswada huu na kuwajaza katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Aprili 8,2011 na kusababisha wananchi wenye mapenzi mema na Taifa letu kukosa nafasi ya kuchangia kutokana na kukaa nje ya ukumbi.Tunalaani kitendo cha Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kutumia silaha na wakati mwingine kuwatishia wananchi waliojitokeza kutoa maoni yao na kuwanyima haki ya kiraia na haki ya kibinadamu, hasa matumuzi ya askari wengi waliotumika mjini Dodoma Aprili 7,2011 na kusababisha wananchi wengine kuogopa kujitokeza kutoa maoni Aprili 8,2011. Tunaitaka jamii ielewe kuwa tunatafuta Katiba ya wananchi kwa maslahi yetu sisi sote wananchi na sio ya wanasiasa au watawala kwa hiyo suala hili liachiwe wananchi walisimamie wenyewe kwa uhuru ili ipatikane Katiba itakayolinda maslahi ya wananchi wote na sio kundi dogo la wanasiasa. Tumeshuhudia katika miaka ya 90 mabadiliko mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na hasa baada ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa. Sisi kama wanaharakati watetezi wa wanyonge, tunaamini kabisa kuwa kuna haja sasa ya kuwa na Katiba mpya ambayo itabeba maoni, mapendekezo na madai ya wananchi walio wengi. Katiba ambayo itajali makundi yote na kutoa kipaumbele cha kuwepo uwiano ulio sawa kwa wanawake na wanaume. Katiba ambayo itazingatia kutoa sheria na sera ambazo zinawanufaisha wananchi wote hasa walioko pembezoni kwa kuzingatia mahitaji yao muhimu hasa ya ajira, afya, elimu, maji, ardhi na mengineo. Sisi kama wanaharakati tumefanya uchambuzi wa kina wa muswada huu na kubaini mapungufu kadhaa. Yafuatayo ni madai na mapendekezo yanayotokana na uchambuzi tulioufanya na mjadala unavyoendelea: 1. Uwiano katika ushiriki na uwakilishi wa vyombo vya Katiba Kwa mujibu wa Ibara ya 6 (1), tunadai, Tume ya kuongoza mchakato huu lazima iwe na uwakilishi asilimia 50:50 wanawake na wanaume, uteuzi wa wajumbe usifanywe na rais peke yake, badala yake bunge au vyombo vingine vyenye mamlaka, pia uteuzi uzingatie wajumbe toka kila jimbo zikiwemo asasi za kiraia, asasi za kidini na makundi ya watu wanaoishi na ulemavu, VVU na Ukimwi. 2. Jina la muswada wenyewe liwakilishe mchakato wa wananchi walio wengi wanavyopendekeza kwa maana ya kutengeneza Katiba mpya, na sio muswada wa sheria ya marejeo ya Katiba iliyopo ( Constitutional review Act, 2011). Kwa mujibu wa kifungu cha 3 neno Katiba limetafsiriwa kumaanisha marekebisho katika Katiba ya sasa 3. Katika kifungu cha 8(1) Hadidu za rejea zisiandaliwe na Rais kama ilivyooneshwa badala yake bunge liunde kamati maalum kwa ajili ya kutoa maamuzi pia kuwepo na usawa wa kijinsia katika uwakilishi wake kwa maana ya wanawake na wanaume na viongozi toka ngazi za kijamii ambao pia watakubaliana muda husika wa kuanza mchakato wa Katiba mpya na muda wa kumaliza mchakato huo. 4. Kifungu cha 17(3) lazima kutengeneza chombo kitakachohakikisha kuwa makundi yote yanawakilishwa katika mikutano na mijadala ya kupata Katiba mpya kwa kujali zaidi wananchi walioko pembezoni hasa wanawake na wanaume, vijana, wanaoishi na VVU na Ukimwi, wanaoishi na ulemavu, wafugaji, wavuvi, wakulima, wanaofanya kazi zisizo rasmi na wengineo 5. Lugha ya muswada iwe ya kiswahili, kwa kuwa muswada huu wa kuandaa Katiba mpya si muswada kama miswada mingine ya sheria za kawaida, na kwa kuwa suala la Katiba ni nyeti na linaliwahusu na kuwagusa watanzania wote, ushiriki wa kila aina katika mchakato wote ni muhimu sana. Tumeshangazwa sana na hatua ya serikali ya kuamua kutumia lugha ya (kiingereza) ambayo watanzania walio wengi hawaielewi kabisa. 6. Katika kifungu cha 21(1) Rais asiwe na madaraka na nguvu za kuunda Baraza la Katiba, badala yake kuwepo na chombo cha kuchagua Baraza la Katiba kama ilivyopendekezwa kwenye tume ya kuongoza mchakato wa kupata Katiba mpya na lichaguliwe moja kwa moja na wananchi 7. Katika kifungu cha 26 jukumu la kusimamia kupata kura za maoni litekelezwe na chombo huru na sio Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Tunapendekeza pia mchakato huu usiongozwe au kusukumwa kwa maslahi ya viongozi wachache bali tuhamasishe na kuwezesha watanzania wote wapate nafasi ya kutoa sauti na madai yao. 8. Vyama vya siasa na makundi mengine yasiyolitakia taifa hili mema waache mara moja kuwatumia wananchi masikini kwa kuwahonga ili wavuruge utaratibu wa mijadala. Matumizi ya watoto wadogo, kujadili ajenda za vyama kwenye mijadala badala ya kuchangia muswada, kuzomea na kufayanya vurugu ziachwe mara moja. 9. Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama visiingilie utaratibu kwa kuwatisha wananchi na mabomu ya machozi na silaha kwani hali hii inawatisha wananchi walio wengi kushiriki ipasavyo katika mijadala hii pia vitendo hivi ni kinyume na haki za binadamu. Imetolewa na: Usu Mallya ………………. Mkurugenzi Mtendaji

Monday, April 11, 2011

Mkuchika: Ufisadi ndio umetumaliza

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Kapteni George Mkuchika, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaonekana machoni mwa umma kuwa kinakabiliwa na tuhuma za ufisadi. Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa kutokana na hali hiyo, imeonekana kuwa na umuhimu wa kubadili timu ya uongozi yaani Sekretarieti na Kamati Kuu (CC). Alisema CCM kina wapenzi wengi ambao wanaendelea kukiamini kwa kuwa si viongozi wote wanakabiliwa na tuhuma za rushwa. Aliongeza kuwa hata tathmini iliyofanywa na mikoa haikueleza kama ni wanachama wote na viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi. Mkuchika alisema kuwa anaamini watu wapya wa watakaochaguliwa na wajumbe wa NEC watafanya vizuri kazi za chama. Mkuchika alisema sekretarieti mpya itaundwa na watu watakaokuwa kazini wakati wote kwa lengo la kushiriki vizuri katika mapambano ya kisiasa. Kwa mujibu wa Mkuchika, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mpambano wa kisiasa umekuwa mkubwa kuliko ilivyokuwa wakati wa chama kimoja. Juzi saa 5:30 usiku aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alizungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha kujiuzulu kwa sekretarieti na CC, hatua ambayo aliieleza kuwa ni mwanzo wa mageuzi ndani ya CCM kwa lengo la kujijenga upya na kukiimarisha katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Akizungumza baada ya kumalizika kwa kikao cha CC, Chiligati alisema imeonekana kuwa kuna haja ya kukifanyia chama mageuzi. “Aidha, kamati Kuu imejadili kwa kina ajenda kuhusu hoja na haja ya mageuzi ndani ya Chama na imefanya uamuzi wa wajumbe wote kujiuzulu ili kumpa nafasi Mwenyekiti wa Chama kuunda upya Kamati Kuu na sekretarieti ya chama,” alisema. Chiligati alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba aliyoitangaza Rais Kikwete wakati wa sherehe za miaka 34 ya CCM mjini Dodoma. Kikao cha NEC kilianza jana saa 6:00 mchana huku miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni uteuzi wa wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba kuwa wajumbe wa chombo hicho. Pia kikao hicho kitafanya uteuzi wa Katibu wa Kamati ya wabunge wa CCM na Katibu wa Wawakilishi wa CCM; tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na taarifa kuhusu muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ameomba ushirikiano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ili kukivusha chama hicho. Rais Kikwete alisema hayo jana mchana mjini Dodoma wakati akifungua kikao cha NEC. Alisema kuwa CCM inapoingia katika mazogo, watu wengi wanapata tabu na kwamba wajumbe hao wana wajibu wa kujipanga upya ili kurejesha matumaini kwa wananchi. Rais Kikwete ambaye alikuwa akifungua kikao hicho ambacho ni cha kwanza tangu baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, alisema ni mkutano wa historia na kwamba baada ya majadiliano ya kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichofanyika Ijumaa na juzi ni lazima wajipange ili kusogeza chama hicho mbele. Katika kikao cha CC Sekretarieti nzima ya NEC chini ya mwenyekiti wake ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ilitangaza kujiuzulu pamoja na Kamati Kuu isipokuwa Rais Kikwete; Makamu wa Mwenyekiti Bara, Pius Msekwa; Makamu Mweyekiti Zanzibar, Amani Abeid Karume na wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao kama, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa; Spika wa Bunge, Anne Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ameir Pandu Kificho; Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Bilal; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seid Ali Iddi; na mjumbe wa kudumu wa CC, John Malecela. “Ninategemea ushirikiano tusome mazingira tuliyonayo tujipange ili kusogeza mbele chama chetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa anategemea ushirikiano kutoka kwa wajumbe wa NEC.

Friday, April 8, 2011

Maoni mchakato wa Katiba watawaliwa na vurugu

UTOAJI maoni juu ya uundwaji tume ya kuendesha mchakato wa Katiba mpya nchini umeingia dosari kwa mikutano ya Dodoma na Dar es Salaam kugubikwa na vurugu. Katika mikutano yote ya Alhamisi, polisi walilazimika kutumia nguvu za ziada kutuliza ghasia, huku Dodoma wakitumia risasi na mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) alikiri jana kusababisha vurugu za Dodoma katika eneo la ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa mjini hapa. Mbunge huyo alikiri mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Msekela kuhamasisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenda kwenye ukumbi huo kutoa maoni ya Katiba na kusababisha vurugu kubwa, iliyolazimu polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi nje ya jengo hilo. Lema alitoa kauli hiyo, muda mfupi baada ya Msekela kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu vurugu hizo na kueleza kuwa zilisababishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotumia vijana kuvuruga amani ya nchi na kwamba alipata taarifa ya kuwapo wanasiasa waliokwenda Udom kuhamasisha wanafunzi kuja bungeni Alhamisi. Baada ya kauli ya Msekela iliyoambatana na kupiga marufuku wanasiasa kufanya kampeni Udom kwa kuwa ni kinyume cha sheria, Lema alijitokeza papo hapo na kukiri kuwa yeye ndiye aliyekwenda Udom na alizungumza na wanafunzi nje ya chuo kwa mujibu wa sheria na hakuwahamasisha kurusha mawe. “ Jumamosi hii nakwenda tena, ni wajibu wangu nikiwa mbunge kufanya hayo, nisingependa kutishwa kabisa, huo ni wajibu wangu mbunge kuhakikisha watu wanauelewa muswada, napenda Mkuu wa Mkoa uelewe kuwa mimi nilikwenda na nitakwenda tena kufungua tawi la chama Jumamosi hii, sheria inaniruhusu,” alisema Lema ambaye baadaye aliwaambia waandishi kuwa atakwenda na Mkuu huyo akitaka kumkamata, amsubiri huko na haogopi, maana sheria anazijua. Lema alisema alikwenda kuhamasisha wasomi waje kutoa maoni kuhusu Katiba kwa kuwa wauza nyanya na wafanyabiashara wa magengeni, hawawezi kutoa maoni kwa sababu hawaelewi Kiingereza na masuala ya Katiba, ila wasomi. Katika eneo la Bunge, watu waliodhaniwa kuwa wananchi, lakini asilimia kubwa kujulikana kuwa ni wanafunzi wa Udom, walizuia njia huku wakiimba nyimbo za kudai Katiba mpya kwa uhuru, lakini baadaye vurugu zilipozidi, Lema aliyekuwa ndani ya ukumbi wa maoni, alitoka nje na kuwataka watu hao watulie ili utaratibu wa kwenda uwanja wa Jamhuri zifanyike, lakini walisikika wakisema, “Lema umetusaliti.” Baadhi yao, walifika eneo la Bunge mapema asubuhi na kulazimisha kuingia ukumbini bila kupekuliwa, tena kwa idadi kubwa, huku ukumbi huo ukiwa na uwezo wa watu 540 na walipoelezwa kusubiri utaratibu wa Kamati kwenda kupokea maoni yao ukumbi wa Chimwaga (Udom), walianza kurusha mawe na kusababisha Mkuu wa Mkoa kuamuru polisi waingie kazini. Hali ya tafrani iliyozuka katika milango ya kuingilia eneo la Bunge kuanzia asubuhi, ilisababisha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kutanda katika maeneo hayo, huku mchakato wa kupokea maoni kwa wananchi walioingia ukumbini ukiwa unaendelea, lakini vurugu zilipozidi, FFU wakiwa na gari lao waliingia kutoka nje ya uzio wa Bunge kwa kasi na kufyatua risasi walikokuwa wananchi na wanafunzi hao. Hata hivyo, Msekela alisema uongozi wa Bunge umekubali kwenda Chimwaga saa 10 jioni Alhamisi ili kupokea maoni ya wanafunzi hao kuhusu Mchakato wa Muswada wa Uundwaji wa Tume ya kukusanya maoni ya uanzishwaji wa Katiba Mpya, lakini kinachotokea ni kutoelewa kwa wanafunzi kuwa si kupokea Muswada wa Katiba Mpya. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Bunge kuhusu tukio hilo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, alisema tukio hilo ni la aibu na waliofanya fujo hawakutumia busara wala hekima, kwa kuwa uwezo wa ukumbi ni mdogo na kamati ndogo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyopo hapa ilisharidhia kwenda Chimwaga. “Ukumbi ni mdogo, tunapata shida, ni kwa namna gani mtu kama ana nia njema ya kutoa maoni anakuja na mawe mfukoni, maoni gani yanatolewa kwa mawe, si busara, tuliliona hilo la ukumbi na tukakubaliana awamu mbili za kupokea maoni, asubuhi mpaka saa nane na saa tisa kuendelea, tulipobaini wengi ni wanafunzi, tukasema kamati iende Chimwaga, lakini hawataki,” alisema Dk. Kashililah. Polisi walipoanza kufyatua risasi zaidi ya milio 20 ilisikika huku mabomu ya kutoa machozi nayo yakifuatia na kusababisha wanafunzi na maelfu ya watu waliokuwa nje ya jengo la Bunge kukimbia bila mpangilio na kusababisha kamera za wapiga picha kuharibika, watu kuanguka na wengine kupigwa mawe. Hata hivyo, hakuna taarifa za waliojeruhiwa kiasi cha kukimbizwa hospitalini kwa kuwa Polisi ilirejesha amani baada ya tafrani hiyo. Awali, wakizungumza kwa nyakati tofauti nje ya jengo la Bunge, wanafunzi wa Udom walisema hawataki kwenda Chimwaga kwa kuwa wanahisi ni ujanja wa kisiasa kwani walipata matangazo yakiwataka waje Msekwa na si Chimwaga na kama Kamati inataka waende Chimwaga, basi waambatane. “Hakuna anayeondoka hapa, tunataka twende Jamhuri ili kila mtu aseme, kama hawataki nasi hatuondoki hapa, kama ni Chimwaga twende mguu kwa mguu,” alisema Petro Karungamya, na kuungwa mkono na mwanafunzi mwenzake, Haruna Mikidadi. Kamati hiyo ndogo ya kupokea maoni Dodoma ilikuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Bora, Angela Kairuki. Kamati nyingine mbili ziko Dar es Salaam na Zanzibar na zitakusanya maoni kwa siku tatu, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi na ikibidi Jumapili. Naye Halima Mlacha anaripoti kuwa mkutano wa Dar es Salaam wa kukusanya maoni juu ya Muswada wa Uundwaji Tume ya Mapitio ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi wa mwaka 2011, ulivurugika na kulazimika kusitishwa hadi leo kutokana na kuzuka vurugu na mapigano wakati mkutano huo ukiendelea. Vurugu hizo zilianza baada ya Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda CCM, Tambwe Hizza, kutoa maoni kwa niaba ya chama hicho, na kujikuta akizomewa na kuitwa fisadi mara alipoanza kusifia jitihada za Serikali za kuanzisha mchakato huo wa kuunda Katiba mpya. “Muswada huu ni jitihada za Serikali za kuwasikiliza wananchi, yatakayoongelewa yatazingatiwa, lakini pia mikutano hii ya hadhara isitumike kumnyima Rais madaraka yake,” alisema Tambwe na kabla ya kumalizia hoja yake alizomea na vurugu kuibuka. 'Habarileo' lilishuhudia ukumbi wa Karimjee ambako mkutano huo ulikuwa ukifanyika ukichafuka ghafla, kwa washiriki, wengi wao wakiwa vijana, kutishia kumtoa mbele Tambwe huku waliokuwa wakimtetea, wakiambulia kupigwa nao bila kukubali na hivyo kuzuka mapigano. Hata hivyo, polisi waliokuwa eneo hilo na wengine kuongezeka walidhibiti tafrani hiyo ingawa mkutano huo ulishindwa kuendelea kutokana na Tambwe kugoma kukaa chini na badala yake kuimbwa kwa kebehi. “Aondoke, CCM ni aibu, fisadi,” ndiyo maneno ya nyimbo yaliyokuwa yakisika ukumbini hapo huku baadhi ya waliohudhuria wakishindwa kuvumilia na kuvamia eneo alilosimama Tambwe hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na mkutano huo kusitishwa. “Kamati ilikuja hapa kukusanya maoni ya wananchi juu ya muswada huu, lakini wote ni mashahidi wa mazingira yaliyojitokeza muda mfupi, hivyo Kamati imeridhia kusitisha mkutano huu hadi kesho (leo) ili kutengeneza mazingira mazuri ya kukusanya maoni haya,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Gosbert Blandes. Awali akiwasilisha maoni yake mbele ya baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, alisifu juhudi za Rais Jakaya Kikwete za kutengeneza muswada huo, lakini pia alishauri wananchi wapewe nafasi ya kutoa maoni juu ya masuala muhimu yanayowahusu na kipengele kinachowabana kirekebishwe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, alionesha kusikitishwa na vurugu zilizotokea na kusisitiza kuwa mkutano huo lengo lake ni kupokea maoni ya mwananchi yeyote yawe mabaya au mazuri na kuyafanyia kazi yatakayoonekana kuwa na tija kwa Watanzania. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alitaja baadhi ya vifungu katika muswada huo virekebishwe likiwamo suala la kupewa madaraka makubwa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupewa jukumu la kusimamia utaratibu wa kupigia kura Katiba hiyo. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema shinikizo na hamasa la kuundwa kwa Katiba mpya lilitoka kwa vyama vya upinzani, lakini kwa bahati mbaya muswada huo haujavitaja vyama hivyo. James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, alipendekeza muswada huo upelekwe bungeni na Ibara ya 98 ya Katiba ibadilishwe, ili kuwezesha kuundwa Baraza la Kutunga Katiba, ambalo litasimamia uteuzi wa makamishna wake na sekretarieti, kuliko kumwachia kazi hiyo Rais pekee kama muswada unavyosema. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, alisema kitendo cha baadhi ya washiriki katika mkutano huo kuanzisha vurugu ni cha kusikitisha, kwa kuwa kinawanyima wananchi wengine fursa na uhuru wa kutoa maoni yao juu ya muswada huo. Wakati huo huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani amesema mchakato wa kupokea maoni ya uundwaji wa Katiba Mpya utaigharimu Serikali zaidi ya Sh bilioni 27 kwa sasa na kiwango hicho kinaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya mchakato. Aidha, amelaani upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu hasa wanasiasa kuwa kinachofanyika Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar siku hizi nne ni utoaji maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Katiba Mpya, kitu ambacho si kweli kwa kuwa ni maoni ya Muswada wa Uundwaji wa Tume itakayopokea maoni ya wananchi. Waziri aliwaondoa hofu wananchi na wadau wote kuhusu suala hilo kwa kusema Bunge limeongeza Jumapili pia itumike itakapobidi na kwamba Serikali itazingatia na kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) na wananchi wengine kuhusu Tume hiyo kwa kuwa serikali ni sikivu wakati wote. Kombani alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha mwaka 2014 Katiba Mpya inapatikana na Muswada wa Uundwaji wa Tume, baada ya maoni, utafikishwa bungeni Aprili 18 ili upitishwe na ipatikane sheria itakayowezesha Tume kuanza kazi Juni mosi, 2011.

Wednesday, April 6, 2011

John Mnyika aihoji serikali kuhusu Kagoda

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika,(Chedema) amehoji uchunguzi dhidi ya kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuchota mabilioni ya fedha za Malipo ya Madeni ya Akaunti ya Nje (EPA), umefikia hatua gani. Katika swali lake la nyongeza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mathias Chikawe, Mnyika alitaka kujua serikali imechukua hatua gani katika uchunguzi wa suala hilo. Lakini katika majibu yake, Waziri Chikawe alisema kwa kifupi kuwa uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo bado unaendelea. “Serikali tunasema bado tunaendelea na uchunguzi na ukikamilika tutachukua hatua,” alisema. Hata hivyo, katika swali lake la nyongeza, Hamad Rashid (CUF Wawi) alisema kesi za uchunguzi zipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), na akaitaka serikali kuwasilisha bungeni taarifa za kesi zilizofanyiwa uchunguzi ambazo zipo kwa DPP. Akijibu Chikawe alikubaliana na mbunge na akasema serikali itawasilisha taarifa za kesi hizo bungeni. Katika swali lake la msingi, Pudenciana Kikwembe (Viti Maalum), alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba lengo la taifa katika kupambana na rushwa linafikiwa. Chikawe alisema katika kuhakikisha lengo hilo, linafikiwa. Serikali ilipitisha sheria mbalimbali ambazo hasa ndiyo msingi wa mapambano dhidi ya rushwa. Pia alisema kupitia mkakati wa taifa dhidi ya rushwa na utaratibu wa Public Expenditure Tracking System (PETS), serikali imeanzisha mafunzo dhidi ya rushwa na miundombinu ya maadili kwa watumishi wa serikali na taasisi zisizo za kiserikali, ili kuhakikisha kuwa watumishi wanazingatia maadili katika kutoa huduma kwa wananchi. Aliwaomba viongozi wote wa serikali, wa siasa, wa dini na wa jamii kwa ujumla, kukemea rushwa kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo kwani rushwa ni adui wa haki.

Dk. Migiro ashauri Ukimwi uwe ajenda ya kisiasa

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro amesema suala la kupambana na maambukizi ya Ukimwi linatakiwa liwe ajenda ya kisiasa ili kuwa na msukumo mpya wa kupunguza maambukizi hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk. Migiro alisema, kwa miongo mitatu sasa, kumekuwa na jitihada nyingi zinazofanywa duniani katika kupambana na maambukizi ya Ukimwi, lakini idadi ya wagonjwa katika kipindi hicho ilifikia milioni 60 huku milioni 25 kati ya hao walipoteza maisha.

Alisema jana kuwa, maambukizi mapya yalipungua kwa asilimia 20 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita na akaeleza kuwa licha ya kuwa hiyo ni hatua nzuri, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

“Kwa kila mtu anayeanza tiba ya maambukizi ya Ukimwi, wawili zaidi wanapata maambukizi mapya, hivyo rasilimali zinatumika zaidi na hivyo fedha zinazotengwa kutotosheleza kugharimia wagonjwa wote kupata tiba,” alisema Dk. Migiro aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania.

Alisema, ndiyo maana anaona suala hilo la kupambana na Ukimwi liwe sehemu ya ajenda za kisiasa na liwekwe zaidi katika mipango ya maendeleo ya kiafya. Pia alisema kunatakiwa juhudi zinazofanywa sasa za kupambana na Ukimwi ziwe endelevu na za muda mrefu.

Alisema, katika hali hiyo, UN imekuja na malengo ya kuwa na maambukizi sifuri, unyanyapaa sifuri na vifo sifuri ambavyo lengo lake ni kupunguza nusu ya maambukizi, vifo na unyanyapaa ifikapo mwaka 2015. “Sifuri tatu hizi zitakuwa na manufaa kwa walioambukizwa mtu mmoja mmoja na dunia nzima,” alisema.

Mkurugenzi wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS), Michel Sidibe alisema licha ya kuwapo juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kwa kuwapatia dawa za kupunguza makali wagonjwa, lakini sio wagonjwa wote wanaopata dawa hizo.

Alitoa mfano kuwa ni asilimia 70 tu ya wajawazito ambao wameambukizwa Virusi vya Ukimwi nchini ndio wanapata ARV’s na ni asilimia 52 ya wagonjwa wa Ukimwi ndio wanaopata dawa hizo kuanzia mwaka 2004.

“Tumepiga hatua, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya ya kuzuia, kutibu na kuwajali hawa ambao tayari wameambukiziwa,” alieleza Sidibe.

Tuesday, April 5, 2011

MSWAADA WA KATIBA NCHINI


SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO

UNAKARIBISHWA KATIKA MFULULIZO WA SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) KILA JUMATANO, AMBAPO WIKI HII TGNP WATAWASILISHA


MADA:MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA; NINI MAONI YA WANANCHI??

Lini: Jumatano Tarehe 06 April, 2011

Muda: Saa 09:00 – 11:00 Alasiri


MAHALI: Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo


WOTE MNAKARIBISHWA

Bunge kusikiliza maoni ya wakazi wa Dar, Dodoma kuhusu Katiba

Wakati Mkutano wa Tatu wa Bunge unanza leo, wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, watapata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Nchi kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi wiki hii. Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Mawasiliano ya Umma wa Bunge, Jossey Mwakasyuka, alisema jana mjini hapa na kuwataka wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao. “Huu ni muswada muhimu sana, wananchi wanatakiwa kutoa maoni yao kwa kadiri watakavyoweza kuijitokeza…tunatoa nafasi kwa watu wengi zaidi kutoa maoni yao,” alisema. Alisema kwa kuwa Alhamisi ni ya mapumziko, yaani ni Siku ya kumbukumbuku ya kifo cha Karume, imeamuliwa iwe ni siku ya kupokea maoni ya wananchi kuhusu muswada huo. Alisema kama wananchi wengi watakuwa bado kutoa maoni yao kwa siku hiyo ya Alhamisi, wataendelea tena kwa siku ya Ijumaa na Jumamosi. Alisema wajumbe wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Bunge watagawanyika makundi mawili ili kupokea maoni hayo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Mwakasyuka alisema Muswada huo wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Nchi unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Aprili 18 na kujadiliwa hadi kesho yake. Katika hatua nyingine alisema Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma wa Mwaka 2011 unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Aprili 15, mwaka huu baada ya kipindi cha maswali na majibu. Katika mkutano huu wa tatu, jumla ya maswali 145 yanatarajiwa kuulizwa na kupatiwa majibu.

Pinda: Kutahiri wanaume kunapunguza kasi ya Ukimwi

Kampeni ya kupambana na Ukimwi nchini imeendesha mpango wa majaribio wa kutahiri wanauwe watu wazima waliokuwa hawajawatahiriwa ikiwa ni njia ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo,.

Tayari jumla ya wanaume 31,432 wamekwishatahiriwa nchini chini ya mpango huo unaotarajiwa kuenezwa katika mikoa minane nchini yenye kiwango cha juu ya maambukizi, ifikapo mwaka 215.

Hayo yalisema na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizindua rasmi Mkakati wa Taifa wa Kinga ya Ukimwi (2009 - 2012) pamoja na Mpango Kazi kuhusu Jinsia na Uukimwi (2010 – 2012) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Uzinduzi huo ulishuhudiwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro ambaye anatembelea Tanzania na aliyefuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu mapambano ya Ukimwi (UNAIDS), Michel Sidibe, na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Alberic Kacou.

Nchini Tanzania baadhi ya wanaume hutahiriwa na wengine huwa hawatahiri kulingana na tamaduni mbalimbali na kwamba kitaalamu kutotahiri kunaongeza kasi ya maambukizi ya Ukimmwi.

Kwa mujibu wa utafiti, kasi ya maambukizi ya Ukimwi imepungua Tanzania kati ya mwaka 2003 na 2008, kutoka asilimia saba hadi asilimia 5.7, ambayo ni idadi ya watu karibu watu milioni moja, ambao asilimia 10 ni watoto wadogo.

Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Iringa ina kasi kubwa ya maambukizi ya zaidi ya asilimia tisa, kwa mujibu wa utafiti huo.

Waziri Mkuu alisema pia kwamba bado Tanzania ina maambukizi mapya kwa watu 90,00 kila mwaka na kwamba alipozindua Uchunguzi wa Hali ya ukimwi nchini mwaka 2009, alielekeza TACAIDS kufanyakazi na tawala za mikoa ili kutengeneza mipango ya uzuiaji wa ukimwi kulingana na mahitaji na hali ilivyo katika kila mkoa.

CHANZO: NIPASHE

Ajivunia kutimiza ndoto za kuwasaidia wanawake

HIVI karibuni Tanzania iliungana na nchi nyingi duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Tanzania iliadhimisha wiki hiyo, kwa kwa kufanya matukio mbalimbali kama vile midahalo, kongamano na maandamano.

Moja ya matukio yaliyofanyika siku hiyo ni utoaji wa Tuzo kwa wanawake waliofanya vema katika tasnia mbalimbali.

Tuzo hizo zinalenga kuwahamasisha akinamama hao kufanya mambo makubwa zaidi ili waweze kuisaidia jamii inayowazunguka.

Pia tuzo hiyo inaonesha ni kwa jinsi gani wanajamii wanatambua mchango wa akina mama katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Tuzo hizo zilianzishwa na Kampuni ya Uhusiano ya Fornt Line Management, ambapo Mkurugenzi Mtendaji, Hellen Kiwia, anasema kuwa mwaka huu tuzo hiyo imeshirikisha vipengele 10.

Akifafanua zaidi Hellen anasema huu ni mwaka wa pili mfululizo, kwa kampuni yake kutoa tuzo hizo na imeweza kuwanufaisha wanawake wengi zaidi.

Hellen anasema tuzo hiyo ilianzishwa, kutokana na nia yake ya muda mrefu ya kuwasaidia wanawake pindi atakapokuwa mwanasiasa.

Anasema ndoto hizo za kuwa mwanasiasa, zilififia baada ya kupata kazi ya utangazaji katika kituo cha East African TV kwa mwaka mmoja kuanzia 2002 hadi 2003.

Akiwa huko alipata mwanga kuwa kupitia vyombo vya habari, vinaweza kuwafikia wanawake nchi nzima.

Hellen baada ya kuacha kazi katika kituo hicho na kuhitimu shahada ya uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, alianzisha Kampuni ya Front Line Management na alijikuta akiwa tena karibu zaidi na vyombo vya habari kiutendaji.

Alitimiza ndoto hiyo ya kuwasaidia wanawake mwaka 2010 ambapo ndipo alitoa tuzo ya kwanza ya kutambua mchango wa mwanamke.

Mwaka huu amefanikisha ndoto hiyo kwa mara ya pili, ambapo kupitia kampuni hiyo ametoa tuzo kwa wanawake wengine katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumzia uamuzi wake wa kuwafikia wanawake kwa njia ya utoaji Tuzo, anasema Tuzo hizo zinawapa mwanga wanawake hao kujiinua zaidi katika shughuli wanazofanya.

Anasema kuwa Tuzo hizo, zina nia ya kutambua mchango wa mwanamke katika jamii, kulingana na nia na malengo ya shughuli yake.

Anasema kuwa wanawake walipata tuzo hizo, wanaweza kuzitumia kama njia ya kupata mafanikio zaidi, kwa kuwa wanadhihirisha ni kwa jinsi gani mchango wao unatambulika.

“ Mimi niliamua kuwafikia wanawake wengi kwa njia hii, ikiwa ni mkakati wangu wa kuhakikisha kuwa nawafikia na kuwainua wanawake nchini. Tuzo ni moja kati ya njia pekee ya kuwasaidia akina mama hawa”, anasema Hellen.

Anasema kuwa ili mwanamke kutunukiwa Tuzo hiyo, anatakiwa awe ana mchango katika jamii inayomzunguka. Mchango huo sio lazima uwe wa mamilioni ya fedha, lakini hata kwa kutoa chochote kile chenye manufaa kwa jamii inayomzunguka.

“Binafsi naamini kuwa msaada kwa mtu yeyote katika jamii, huwa sio lazima fedha peke yake, ila hata ujuzi wa kitu fulani unaweza kuwa msaada tosha”, anasema Hellen.

Anaongeza kuwa wapo watu wanaoweza kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuwapatia elimu au hata mazingira bora ya kujifunzia kitu fulani, nao huu ni msaada pia.

Wanawake waliopata tuzo mwaka huu ni pamoja na Oliver Lyamuya, aliyepewa Tuzo ya Multichoice Arts and Culture.

Pia kulikuwa na Tuzo ya Kilimo ya RBP, ambayo alishinda Asia Kipande Tuzo ya mwanamke chipukizi mwenye mafanikio, iliyotolewa na American People ilienda kwa Modesta Mahiga huku Mwamvita Makamba, akipata tuzo ya taaluma kutoka kwa kinywaji cha Bailey.

Tuzo ya mwanamke mwenye mchango katika michezo, ilienda kwa Rahma Al Kharoos, huku tuzo ya Sayansi na Teknolojia iliyotolewa na Kampuni ya Songas, ilienda kwa Mary Mwanukuzi.

Hellen anasema akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayotoa tuzo hizo, hahusiki kwa namna yoyote ile na uchaguzi wa wanaozipata, kwa kuwa zinaratibiwa na Kampuni ya Delloite, ambayo ina wajumbe maalumu wa kufuatilia tuzo hizo.

Kwa mwaka huu, mwanamke wa mwaka ambaye amepata tuzo bora kuliko wengine ni – Marina Njelekela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Wanawake Nchini (Mewata). Yeye alishinda kupitia Tuzo ya Afya, iliyotolewa na Deloitte.

Mwanaharakati na mwanahabari wa muda mrefu nchini, Ananilea Nkya, alipata Tuzo ya Teknolojia na Mawasiliano, iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pia, kulikuwa na tuzo nyingi kama utumishi wa umma, aliyopata Margareta Chacha, Tuzo ya Biashara aliyopata Zainab Ansell, Tuzo ya Home Shopping Center aliyopata Khadija Mwanamboka na Tuzo ya Kutambua Mchango wa Mwanamke wa Muda Mrefu, aliyotunukiwa Dk. Maria Kamm.