Friday, January 30, 2009

MREJESHO WA SEMINA (GDSS) YA TAREHE 28/1/2009

UTANGULIZI:
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umejiwekea utaratibu wa kufanya muendelezo wa semina za jinsia na maendeleo kwa kila siku za jumatano (GDSS),ambazo hufanyika makao makuu ya ofisi za mtandao huo zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam.
Semina hizi zina lengo la kupeana taarifa, kujengeana uwezo na kuibua mijadala ya masuala mbalimbali katika jamii ni kwa watu wote bila kujali jinsia, umri, rika, kabila, kiwango cha elimu au utafiti kwa mshiriki.

TAREHE:-
Semina hii ilifanyika jumatano ya tarehe 28/1/2009.

MADA:-
Tathmini miaka kumi (10) ya sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) 1998-2008.

MWEZESHAJI:- Kaka Venant William, kutoka TGNP.

MAHUDHURIO:-
Washiriki waliohudhuria GDSS hii walikuwa kama ifuatavyo:-
Wanawake: 50
Wanaume: 38
Jumla: 88

KUHUSU WASHIRIKI:-
Washiriki wa semina hii walikuwa ni wanachama wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS), wafanyakazi wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) na wananchi kwa ujumla.

MJADALA KWA UFUPI:-
Baada ya mrejesho kutoka kwa washiriki wa semina kuhusu kumbukumbu ya mada zilizotolewa juma lililopita na watoa mada Bi. Ananilea Nkya kutoka (TAMWA) na Bi. Scholastika Jullu kutoka (WLAC) kuhusu historia fupi iliyopelekea msukumo wa kutaka kutungwa kwa sheria ya makosa ya kujamiiana, mafanikio pamoja na changamoto kuhusu (SOSPA) mwanzoni mwa miaka ya tisini 1990.
Washiriki waliyataja baadhi ya mambo yaliyopelekea msukumo wa kutaka sheria hii kutungwa kuwa pamoja na:-

•Athari za utandawazi kuanza kuibuka.
•Madhara ya ukimwi kuanza kuonekana wazi zaidi.
•Kushamiri kwa vitendo vya kishirikina (Ramli).
•Ukosefu wa haki hasa kwa wanawake na watoto.
•Mgawanyo mbaya wa rasilimali katika jamii.

MJADALA KWA UREFU:-
Mjadala ulilenga zaidi katika changamoto na nini kifanyike kuhusiana na sheria hii ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) hasa baada ya waziri wa sheria na mambo ya katiba kutoa tamko kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa wanaharakati walishinikiza sheria mbaya ya makosa ya kujamiiana mwaka 1998 na kusema kuwa inapingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kutamka azma ya serikali kuifanyia mabadiliko haraka iwezekanavyo.
Washiriki walisema pamoja na sheria kuonyesha makali yake, lakini hali imezidi kuwa mbaya sana kwa sasa maana vimezuka vitendo vingine vingi zaidi vyenye kumdhalilisha zaidi mwanamke na mtoto.Waliyataja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na:-
•Kutiwa hatiani kwa wahalifu wengi wa makosa ya kujamiiana toka kuanzishwa kwa sheria hii miaka kumi (10) iliyopita, takriban robo tatu (¾) ya wahalifu wanatumikia adhabu katika magerezani mbalimbali nchini.
•Sheria imewezesha ulinzi kupatikana kwa wanawake wengi zaidi na watoto nchini.
•Kupungua kwa vitendo vya ukeketaji. Takwimu zimeonesha kuwa mwaka 2006 vitendo hivyo viliripotiwa kupungua kwa zaidi ya asilimia ishirini (20).
•Kupungua kwa vitendo vya kidhalilishaji/bughudha dhidi ya wanawake.

CHANGAMOTO;
Kwa miaka kumi iliyopita ya utekelezaji wa sheria hii changamoto kadhaa zilizo orodheshwa, nazo ni pamoja na:-

•Ukali wa sheria bado haujawa tiba ya matatizo kwa wote wanaoshiriki katika vitendo vya ubakaji/udhalilishaji.
•Kumekuwapo na tabia ya kutokuwajibika kwa wana jamii na hususan katika jeshi la polisi linapokuja suala la utekelezaji wa sheria hii (SOSPA).
•Kukosekana kwa utu miongoni mwetu kunakopelekea msukumo mdogo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
•Mila,desturi na tamaduni zetu bado ni tatizo katia utekelezaji wa sheria hii.
•Miongozo ya dini katika masuala ya ndoa itazamwe upya kwa maana katika baadhi ya dini humnyima mwanamke.

NINI KIFANYIKE?;
Baada ya mjadala wa kina mapendekezo kadhaa yalitolewa na wana GDSS pamoja na wana jamii kwa ujumla kuhusu nini kifanyike kwa mustakabali wa sheria hii na kutaka;

•Tamko la kumtaka waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia na watoto Mh. Magreth S. Sitta kwa umma kuhusu mfanikio ya sheria ya makosa ya kujamiiana SOSPA ya mwaka (1998).
•Waziri wa sheria na mambo ya katiba Mh. Mathias Chikawe aombe radhi kwa tamko alilolitoa kuhusu SOSPA.
•Wana GDSS kuandaa tamko na kulitoa rasmi jumatatu tarehe 2/2/2009 kwa umma kupinga kauli iliyotolewa na waziri wa sheria na mambo ya katiba kuhusu SOSPA.
Na katika kutoa tamko hili, timu ya watu wa nane (8) iliundwa na washiriki wa semina ili kuwawakilisha wenzao.
Washiriki hao ni:-

1. Esther Jackson.
2. Nuru Ruksan
3. Eva Nganda
4. Subira Kibiga
5. Eliab Maganga
6. Badi Darussi
7. Pius Manyama
8. Titus Ntanga

HITIMISHO:-
Wakati wa kufanya hitimisho la semina ilikubaliwa na wote kuwa yote yalioazimiwa yafanyiwe kazi kikamilifu na ifikapo jumanne ya tarehe 3/2/2009 kuwe na jibu kamili la maazimo ili kabla ya kuanza GDSS ya wiki ijayo utolewe mrejesho wa yote tuliyokubaliana.

Thursday, January 29, 2009

Ujumbe katika Picha


Piga ngoma sio Mwanamke

Richmond sasa ifikie mwisho


TANGU Bunge litoe mapendekezo yake kuhusu hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wahusika katika kashfa ya zabuni ya kampuni ya Richmond Development, mwaka sasa unaelekea kutimia.

Katika mwaka huo mmoja, Bunge limekutana katika mikutano yake takriban mara tatu. Wabunge walikutana Aprili, mwaka jana, wakakutana katika Bunge la Bajeti na baadaye wakakutana katika mkutano wa Novemba, mwaka jana.

Kwa mara nyingine, Bunge limeanza mkutano wake mjini Dodoma. Huu ni mkutano wa 14 wa Bunge. Lakini pia ni mkutano wa nne wa Bunge, tangu Serikali iahidi kutekeleza mapendekezo kuhusu Richmond.

Tunatambua kuwa mbele ya Watanzania, Serikali na Bunge ni vyombo muhimu na ambavyo umma unaviheshimu sana. Ni vyombo vinavyogusa maisha ya kila siku ya raia wa Tanzania.

Pamoja na hayo tunadhani ni hatari kwa baadhi ya Watanzania kuamini kuwa Bunge au Serikali vinafanya mchezo wa kuigiza kuhusu Richmond kama ambavyo hisia miongoni mwa wanajamii zinavyoanza kujionyesha sasa.

Na hisia hizi si bure. Kwamba Richmond imegusa taasisi nyeti nchini kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni sababu tosha ya kuibuka kwa hisia hizi miongoni mwa umma.

Sisi tungependa kuona Bunge na Serikali vikitimiza majukumu yao barabara katika suala hili la Richmond ili wanaodhani ahadi ya Serikali kutekeleza mapendekezo ya Bunge ni mchezo wa kuigiza, wanatoka katika ulimwengu wa dhahania.

Ni busara sasa ahadi ya Serikali kuhusu Richmond ifikie mwisho ili mikutano ijayo ya Bunge iendelee na masuala na changamoto nyingine nyeti zilizoko mbele.

Hivyo ni imani yetu ya kuwa katika mkutano huu wa 14 wa Bunge, Serikali itawasilisha taarifa kamili bungeni, hasa ikizingatiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwisha kuunda timu maalumu kufanikisha suala hili.

Hiyo ikifanyika itatoa nafasi kwa busara, raslimali, nguvu kazi na muda sasa kuwekezwa katika masuala mengine ndani ya mikutano ijayo ya Bunge huku Richmond ikiwekwa katika kaburi la sahau.

Source: Raia Mwema Januari 28,2009

Wednesday, January 28, 2009

SKENDO YA MAJENGO MAPYA BoT WAHUSIKA KORTINI


Twin Towers

MAOFISA wa ngazi za juu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Deogratius Kweka, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka matatu ya kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 200.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Hadija Msongo jana, Wakili wa Serikali John Lwabuhanga alidai kuwa Liyumba ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT na Kweka ambaye ni Meneja Miradi wa BoT, wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka wakiwa watumishi wa umma.
Akiwasomea mashitaka, wakili huyo alidai katika mashitaka ya kwanza dhidi ya Liyumba kuwa, katika siku tofauti kati ya mwaka 2001 na 2006, akiwa mtumishi wa umma BoT, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuchukua uamuzi wa kuandaa ujenzi wa jengo la BoT bila kufanya makubaliano na Bodi ya Uongozi wa BoT.

Tuesday, January 27, 2009

Semina (GDSS) wiki hii

UNAKARIBISHWA KATIKA MFULULIZO WA SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) KILA JUMATANO AMBAPO WIKI HII WANAGDDS WATAJADILI KUHUSU:

NINI KIFANYIKE KUTOKANA NA MJADALA WA WIKI ILIYOPITA KUHUSU MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA: 1998-2008


LINI: Jumatano Tarehe 28 Januari 2009

Muda:
Saa 9:00 – 11:00 Jioni


MAHALI: Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni


WOTE MNAKARIBISHWA!!

MUHTASARI WA SEMINA KUHUSU TATHMINI YA MIAKA 10 YA SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA (SOSPA) YA MWAKA 1998

Tathmini ya miaka kumi (10) ya sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) 1998.

WATOA MADA:
Marie Shaba – (FemACT).
Ananilea Nkya – (TAMWA).
Scolastica Jullu – Kituo cha msaada wa sheria (WLAC).

MWEZESHAJI:- TGNP

MAHUDHURIO:-
Washiriki waliohudhuria GDSS hii walikuwa kama ifuatavyo:-
Wanawake 144
Wanaume 90
Jumla 234
KUHUSU WASHIRIKI:-
Washiriki wa semina hii walikuwa ni wanachama wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS), vikundi shirikishi , wafanyakazi wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) na wananchi kwa jumla.

MJADALA KWA UFUPI:-
Baada ya salam,ufunguzi wa semina na kutakiana heri ya mwaka mpya kuliko fanywa na bi Marie Shaba, historia fupi ya msukumo wa kutaka kutungwa kwa sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) ilitolewa.
Mtoa mada bi Ananilea Nkya kutoka (TAMWA) alianza kwa kusema “Mfumo ama sera za nchi zilikuwa mbaya na kuwakandamiza watu wengi hasa katika nyanja za uchumi,siasa na uchangiaji huduma zilizopelekea watu wengi kukosa ajira na kupelekea kuibuka kwa matatizo mengi zaidi ya kijamii mwanzoni mwa miaka ya tisini (1990) .”

Aliyataja baadhi ya mambo yaliyopelekea msukumo wa kutaka sheria hii kutungwa kuwa ni:-

• Athari za utandawazi kuanza kuibuka.
• Madhara ya ukimwi kuanza kuonekana wazi zaidi.
• Kushamiri kwa vitendo vya kishirikina (Ramli).
• Kufichuka kwa vitendo vingi viovu katika jamii kama vile ubakaji,kunajisi n.k kupitia vyombo vya habari.
• Ukosefu wa haki hasa kwa wanawake na watoto.
• Mgawanyo mbaya wa rasilimali katika jamii.

Baada ya kubainisha hayo mtoa mada aliwataka washiriki wajiulize kama kitendo cha waziri kusema sheria hii imelenga kuwakandamiza wanaume zaidi…
Je mambo yaliopelekea kutungwa kwa sheria hii yamebadilika?

Aliendelea kwa kusema “tunaihitaji zaidi sheria hii kwa sasa zaidi kuliko wakati mwigine wowote, maana katika jamii yetu sasa kumezuka tabia mbaya zaidi za vitendo vya ubakaji katika ndoa na bado watu wameendelea kukosa ajira, hivyo kufikiria ,kupunguza ama kufuta sheria hii ni kuwaweka wanawake na watoto katika wakati mgumu zaidi”.

MJADALA KWA UREFU:-
Mafanikio na changamoto za sheria hii ndio yalijadiliwa katika hatua hii kuhusu sheria hii ya makosa ya kujamiina . Washiriki wakiongozwa na mtoa mada bi Scholastica Jullu kutoka kituo cha msaada wa sheria (WLAC).

Mafanikio ya sheria;
• Kutiwa hatiani kwa wahalifu wengi wa makosa ya kujamiiana toka kuanzishwa kwa sheria hii miaka kumi (10) iliyopita, ilielezwa karibu robo tatu (¾) ya wahalifu wanatumikia adhabu katika magerezani mbalimbali nchini.
• Sheria imetoa ulinzi kwa wanawake wengi zaidi na watoto nchini.
• Kupungua kwa vitendo vya ukeketaji. Ilielezwa kuwa mwaka 2006 vitendo hivyo viliripotiwa kupungua kwa asilimia ishirini (20).
• Kupungua kwa vitendo vya kidhalilishaji/bughudha dhidi ya wanawake.

Changamoto;
Kwa miaka kumi iliyopita ya utekelezaji wa sheria hii changamoto kadhaa zilibainishwa,miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na:-

• Kutokufahamika vizuri kwa sheria hii katika jamii.
• Kutokupelekwa/kuripotiwa kwa kesi nyingi za ubakaji katika vituo vya polisi kwa hofu ya aibu ya kutokuolewa na kwa wale wadogo mara nyingi maamuzi ya usuluhishi yanafanywa majumbani.
• Mara nyingi katika kesi za namna hii watoa ushahidi na wapelelezi huwa tofauti,kitu kinachopelekea kukosekana ushahidi madhubuti wa kuwatia hatiani wahalifu.
• Kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji ndani ya ndoa.
• Mkinzano wa kisheria kwenye ndoa, elimu na uchaguzi.Inatamkwa kuwa mtu mzia mwenye haki ya kushiriki uchaguzi lazime awe na miaka kunzia kumi na nane (18), lakini mtu huyo huyo anaruhusiwa kuingia katika ndoa akiwa na miaka kumi na tano (15) na kumnyima fursa ya kupata elimu.

Kifanyike nini;
• Elimu iendelee kutolewa kwa jamii ili kurahisisha uelewa na utekelezaji wa sheria hii.
• Kuwepo na utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja katika kufatilia mambo ili kupata ufanisi mapema.
• Kuondolewa kwa mfumo dume ambao tayari umeonekana kuwa ni tatizo.
• Tuwe na mbinu mpya za jando na unyago.
• Sheria ya makosa ya kujamiiana ifundishwe kuanzia ngazi za shule ya msingi kwa kuzingatia mtaala utakaokubaliwa.
• Kuongezwe kipengele cha ubakaji ndani ya ndoa katika sheria hii.
• Serikali ianzishe mahakama maalum,wanasheria na vifaa maalum kwa maswala ya ubakaji.

HITIMISHO:-
Wakati wa kufanya hitimisho la semina, mambo matano (5) yaliazimiwa:-

• Kabla ya muswada wa marekebisho ya sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) kupelekwa bungeni,rasimu ya mabadiliko ipitiwe kikamilifu na wadau wote au kuwe na mjadala wa kitaifa kuhusu mabadiliko hayo.
• Itolewe elimu ya kutosha kwa vyombo vya dola na jamii kwa ujumla kuhusu utekelezaji madhubuti wa sheria hii.
• Kutaka maboresho zaidi na kuzuia ufutwaji au kupunguzaji wa adhabu katika sheria hii.
• Kuwepo kwa shinikizo la kumtaka waziri mwenye dhamana ya sheria ajiuzulu.
• TGNP na wanaharakati wengine waendeleze vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi kwa kuunganisha nguvu.

Mwisho ilikubaliwa kuwepo na muendelezo wa mjadala katika muendelezo wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) siku ya jumatano tarehe 28/1 kuhusu sheria hii ya makosa ya kujamiiana (SOSPA)-1998 ili kutoa fursa zaidi kwa washiriki kujadili kwa kina na kutoa maoni yao.

Friday, January 23, 2009

Uchumi wamtikisa Kikwete

HALI ya uchumi nchini hivi sasa si nzuri, na inaelekea imeanza kumtikisa Rais Jakaya Kikwete ambaye sasa ameanza kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu utendaji wa sekta muhimu kiuchumi, Raia Mwema imebaini.

Kuanzia wiki iliyopita, Rais Kikwete amekuwa na vikao vyenye mwelekeo wa kuwabana watendaji na wafanyabiashara wa sekta zinazogusa uchumi, ikiwa ni pamoja na sekta ya miundombinu na fedha.

Katika kikao na sekta ya miundombinu, Rais Kikwete aliwahusisha pia watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao walibanwa kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka na unakwenda sambamba na ushirikiano na wadau wengine wakiwamo wafanyabiashara na kampuni binafsi.

Katika kikao hicho alitoa maelekezo kwa wadau wa sekta ya reli na bandari ambao walitakiwa kuboresha huduma zao ili kuwezesha waagizaji bidhaa nchini kutokimbilia kutumia bandari ya nchi jirani.

Mara baada ya kukutana na wadau wa sekta ya miundombinu, Rais Kikwete, wiki hii, alikutana na watendaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi, na asasi zake, ikiwamo BoT.

Katika kikao hicho, Gavana Beno Ndullu alinukuriwa akisema kwamba mfumuko wa bei ulipanda ghafla mwaka jana, kwa sababu ya kupanda mno kwa bei za mafuta na vyakula (nafaka) katika soko la dunia, na kwamba utaanza kushuka katika siku za karibuni, na hivyo kuteremsha gharama za maisha.

Mfumuko wa bei nchini ulikuwa asilimia 13.5 kwa mwezi uliopita wa Desemba kutoka asilimia 8.6, kabla ya kuanza kupanda ghafla na kwa kiasi kikubwa kwa bei ya mafuta duniani na ile ya chakula.

Taarifa ya Ikulu ilieleza kwamba, BOT inabashiri kuwa lengo la ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.5 bado linaweza kufikiwa.

Tofauti na mikutano aliyoifanya mwanzoni mwa utawala wake ambako Rais alitembelea kila wizara na kutoa maelekezo yake, mikutano ya sasa inafanyika Ikulu kati ya Rais na viongozi wa juu wa wizara mbalimbali na asasi za wizara hizo.

Gavana Ndullu pia alieleza kuwa hazina ya fedha za kigeni katika BOT, hadi kufikia Desemba mwaka jana, ilikuwa ni dola za Marekani bilioni 2,894.42 ambazo zinatosha kuweza kuagiza bidhaa kutoka nje kwa kipindi cha miezi minne.

Kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba hali ya uchumi imekuwa mbaya; kiasi cha kuilazimu Serikali kuharakisha kuchapisha noti mpya, lakini Gavana Ndullu alisema kuwa hatua hiyo itakayochukuliwa mara baada ya kumpata mzabuni, haina uhusiano na hali hiyo.

Kwa sasa Serikali inamtafuta mzabuni wa kuchapisha fedha, baada ya wa awali kutoka nchini Ujerumani, kukamilisha mkataba wake, ingawa pia naye anakaribishwa kupigania zabuni hiyo.

Akizungumza na Raia Mwema jijini Dar es Salaaam, ingawa Profesa Ndullu amekiri kuwapo kwa mfumuko wa bei nchini, lakini akasisitiza kuwa hali si mbaya sana na kwamba kuchapwa kwa noti mpya ni utaratibu wa kawaida

“Kuna mambo mawili katika kuchapa noti mpya. Kwanza ni kuondoa noti zilizochakaa, lakini pia ni kukidhi mahitaji ya kibiashara na hasa hali ya biashara inapokua kwa kasi,”

“Nasi tunafikiria kubadili noti kwa malengo mbalimbali ambayo ni pamoja na kuziboresha lakini hii ni hatua ya baadaye, baada ya kumpata mzabuni.

“Tuliwahi kuwa na senti tano, senti 10 lakini tukaziacha…ni kweli kuna suala la mfumuko wa bei lakini hali si ya kutisha kama ilivyo Zimbabwe ,” alisema.

Alipoulizwa kama ni mambo gani yatazingatiwa katika noti mpya, Profesa Ndullu alisema kikao rasmi bado hakijafanyika cha uamuzi lakini mambo kadhaa yatazingatiwa, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa noti za sasa, hususan za Sh 10,000.

Na alipoulizwa kuhusu noti zitakazoondolewa katika mzunguko, Profesa Ndullu hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wakati wake haujafika.

Katika miaka ya nyuma, uchapishaji wa noti mpya umekuwa ukihusisha mchakato wa kufuta katika matumizi baadhi ya noti.

Noti ambazo zimewahi kufutwa katika mchakato wa kutumika ni pamoja na za shilingi 10 na shilingi 200. Noti ya shilingi 200 ilianzishwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mtaalamu bingwa wa uchumi alisema kwamba kama Serikali inakusudia kuchapa noti mpya kwa ajili ya kuondoa zilizochakaa katika mzunguko, ni sahihi.

Hata hivyo, alionya kuwa kama Serikali inakusudia kuchapa noti mpya kwa lengo la kufidia matumizi yake hayo ni makosa makubwa yenye athari ya moja kwa moja kwa raia wa kawaida nchini. Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, athari hizo ni pamoja na ongezeko la mfumuko wa bei.

“Kwanza ni utaratibu wa kawaida kwa Benki Kuu kuchapisha fedha na hasa kama inakusudia kuondoa fedha chakavu katika mzunguko,” alisema na kuongeza kuwa kama lengo la sasa la hatua ya Serikali ni kuingiza fedha mpya na kuondoa za sasa basi athari pia zinaweza kuwa kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kupoteza imani na sarafu ya Tanzania.

Lakini pia alisema hatua hiyo inaweza kuwa na mantiki kama Serikali inakusudia kuanzisha noti mpya ya kiwango cha juu baada ya kubaini kuwa noti ya sasa ambayo ni Shilingi 10,000 haikidhi mahitaji kwa kulinganisha na sarafu za kimataifa na hususan dola ya Marekani.

Kwa upande wake, mtaalamu na mtafiti wa masuala ya uchumi kutoka Taasisi ya Utafiti katika masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Oswald Mashindano, aliiambia Raia Mwema kuwa uamuzi wa kuchapisha fedha mpya una athari mbaya kwa Taifa.

“Unapochapisha noti mpya maana yake ni kwamba kuna matatizo katika vyanzo vya mapato au mfumo wa uchumi umekubwa na mtikisiko.

“Huko nyuma nafikiri katika miaka ya sabini tuliwahi kuchapisha noti. Lakini unapochapisha noti maana yake unaongeza fedha nyingine nje ya mfumo wa kawaida wa uzalishaji.

“Unaongeza fedha hizo katika mzunguko wa fedha na hapo utakuwa hauna mizania sawa na unaweza kufungulia mfumuko wa bei zaidi,” anasema.

Anazungumzia kauli ya Gavana Ndullu akisema; “Kama ni kweli kuna ukuaji wa shughuli za biashara kiasi cha kuhitajika kuongezwa kwa fedha zaidi hiyo ni ishara kwamba ujasiriamali na wajasiriamali wameongezeka.

Katika hali kama hiyo, fursa bora zaidi si kuchapisha fedha mpya na kuziingiza katika mzunguko bali ni kukopa fedha katika taasisi za kimataifa na kuwakopesha wajasiriamali.

Alitoa mfano wa uamuzi uliofanywa hivi karibuni na Serikali ya Marekani wa kukopesha fedha makampuni ya nchi hiyo yaliyoathiriwa na kuyumba kwa uchumi wa taifa hilo kubwa duniani.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu ugumu wa kupata mkopo katika asasi hizo kutokana na asasi hizo nazo kuathiriwa na anguko la uchumi duniani, Dk. Mashindano alisema kama mkopo unashindikana ipo njia nyingine ya tahadhari.

Alibainisha tahadhari hiyo kuwa ni kuchapisha fedha mpya na wakati huo huo kuwa makini zaidi katika matumizi hususan katika sekta kiongozi katika kuimarisha uchumi.

Raia Mwema, januari 21,2009

Thursday, January 22, 2009

Sakata la Richmond kulipuka upya

-Wabunge wamsubiri Pinda
-Wataka wahusika washitakiwe kama kina Mramba

BAADHI ya wabunge, wanasiasa na wataalamu wa sheria wanautazama uamuzi wa kumburuza mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Richmond, Naeem Gire, kwa tahadhari kubwa wakiamini kuwa kuna malengo yaliyojificha.

Richmond Development LLC ni kampuni iliyopewa zabuni ya kuagiza mitambo ya kufua umeme wa dharura, mwaka juzi, na ndiyo chanzo cha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.

Itakumbukwa kuwa katika taarifa ya Kamati Teule iliyochunguza Richmond , ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harisson Mwakyembe, mapendekezo 23, yakiwamo ya kuwachukulia hatua waliohusika kuibebea kampuni hiyo kinyume cha taratibu na hata sheria za nchini, yalitolewa.

Wakizungumza na Raia Mwema, jijini Dar es Salaam ambako wabunge wanakutana kwa ajili ya maandalizi ya mkutano ujao wa Bunge utakaoanza Januari 27, mwaka huu, wabunge na watalaamu hao walidai kuwa msingi wa wasiwasi wao ni aina ya mashitaka yanayomkabili Naeem Gire.

Kwa mujibu wa hati za mahakamani, Gire anakabiliwa na mashitaka ya kusema uongo pamoja na kughushi nyaraka.

Anakabiliwa na mashitaka matano, baadhi yakiwa ni kuwasilisha taarifa za uongo katika Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na katika Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT), iliyoundwa na baadhi ya makatibu wakuu wa wizara, akiwamo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja.

“Gire ni mtu mdogo sana katika sakata hii nzima ya Richmond , ni kweli kwamba naye ana makosa na anastahili kuchukuliwa hatua za kufikishwa mahakamani.

“Lakini sisi wabunge hatupaswi kugota hapo kimtazamo. Upeo wetu unapaswa kwenda mbali zaidi na hasa katika kutafakari uwezekano wa kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu wote waliohusika katika sakata la Richmond ,” anasema mmoja wa wabunge, mwenye taaluma ya sheria.

Anasisitiza kuwa kwa kuzingatia aina ya mashitaka dhidi ya Gire, kuna uwezekano kuwa watendaji wengine wote na wanasiasa katika kashfa hiyo, wakaonekana hawana hatia wala makosa.

Kwa mujibu wa mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, mashitaka dhidi ya Gire ya kusema uongo na kuwasilisha nyaraka zisizofaa, kisiasa inaweza kutafsiriwa kuwa mawaziri na timu ya watalaamu wa Serikali walikuwa na nia njema katika mchakato mzima wa Richmond, na hawastahili lawama kwa kuwa walipewa taarifa za uongo na nyaraka za kughushi.

Mbunge mwingine ambaye pia hakutaka kutajwa jina kwa madai kuwa wanaisubiri taarifa ya Serikali bungeni, alisema; “Issue mama katika Richmond ni watendaji wa Serikali waliohusika kuitia hasara nchi, huyo Gire achukuliwe hatua lakini si kipaumbele cha mapendekezo ya Bunge.

“Kamati Teule ya Bunge imefanya kazi kubwa na yenye ushahidi wa kutosha namna ambavyo watendaji na wanasiasa walivyoibeba Richmond , licha ya kuonywa na baadhi ya watalaamu wa TANESCO na wengineo,” alisema.

Itakumbukwa kuwa katika taarifa yake ya kurasa 165 kuhusu Richmond , Kamati Teule ya Bunge iliwahoji mashahidi 75, kwa kuwauliza maswali 2,717.

Kamati hiyo pia ilipitia nyaraka 104, zilizotajwa bungeni na Dk. Mwakyembe kuwa zimebeba ushahidi usio na shaka kwamba Wizara ya Nishati na Madini, iliibeba Richmond Development Company LLC kutoka
mwanzo wa mchakato wa zabuni hadi mwisho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema pamoja na kufunguliwa kwa kesi dhidi ya Gire, wahusika wengine waliosalia katika sakata la Richmond hawana mwanya wa kusafishwa.

“Ni kweli kwamba huyo Gire amefikishwa mahakamani, lakini yeye anakabiliwa na makosa ya jinai na kughushi, wapo watendaji Serikali wanaostahili kuchukuliwa hatua zaidi,” alisema Shelukindo akiongeza:

“Kama watendaji na viongozi wa kisiasa walikubali kudanganywa na Richmond tangu awali, maana yake ni wazembe…ni dhahiri kuwa wamefanya kazi kizembe na hii ni hatari kama kiongozi unadanganywa kirahisi tu…eeh! Unaweza kuangusha nchi kiuchumi…tutazidi kufuatilia hadi mwisho wake.”

Alisema wanasubiri taarifa ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge.

Kwa mujibu wa Shelukindo, wanataraji Waziri Mkuu atawasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo katika mkutano ujao wa Bunge.

Waziri Mkuu Pinda alikwishawahi kuwasilisha taarifa yake ya awali bungeni kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo na kuahidi kukamilisha utekelezaji huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema waliohusika na sakata la Richmond walitumia vibaya madaraka sawa na wanasiasa waliofikishwa mahakamani kuhusiana na suala la kampuni ya Alex Stewarts.

“Makosa ya Mramba (Basil) na Yona (Daniel) , ya kutumia vibaya madaraka yanafanana na watendaji waliohusika katika mkataba wa Richmond, hivyo wanatakiwa nao wafikishwe mahakamani,” alisema Lipumba.

Lakini kwa upande mwingine watalaamu wengine wa sheria wanabainisha kuwa hatua ya kumfikisha Gire mahakamani haiwezi kulifunga mdomo Bunge kuzungumzia kadhia ya Richmond .

Wanasema Bunge lina mwanya mkubwa kisheria na kikatiba kuhoji hatua iliyofikiwa na Serikali katika utekelezaji wa maazimio ya Bunge, bila kuingilia uhuru wa Mahakama (kesi ya Gire).

“Bunge linaweza kuendelea kujadili suala la Richmond bila kuingilia uhuru wa Mahakama. Suala la Gire ni la kijinai pekee. Lakini wapo watendaji waliozembea serikalini na yapo mapendekezo ya Bunge. Haya yote yanaweza kuhojiwa au kujadiliwa bila hata kuingilia Mahakama,” anafafanua mmoja wa wabunge wa muda mrefu bungeni.

Kamati Teule ya Bunge ililalamika kuwa katika kile kilichoelezwa kukidhi maslahi binafsi, Wizara ya Nishati na Madini ilikataa kuiruhusu kuona majalada ya wizara yenye mawasiliano kuhusu zabuni hiyo ya Richmond.

Ilibainika pia kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilipindisha uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kusitisha mpango uliokuwa umekaribia utekelezaji wa kuzalisha umeme kupitia mitambo ya kukodi ya kampuni ya CDC Globeleq.

Inadaiwa upuuziaji huo ulifanywa bila kuufikisha ujumbe wa Serikali kwa kampuni hiyo wa kurekebisha masharti yao ili mradi huo utekelezwe.

Inadaiwa pia kwamba hayo yalifanyika siku hiyo hiyo ambayo Baraza la Mawaziri lilitoa maagizo na siku nne baada ya kuanza mgawo wa umeme kwa mikoa yote ya Tanzania Bara inayounganishwa na Gridi ya Taifa.

Kamati Teule ya Bunge ilibaini pia kukiukwa kwa makusudi Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004, na Kanuni zake za mwaka 2005, licha ya Baraza la Mawaziri kusisitiza Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake izingatiwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Teule, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pia lilishinikizwa kutoheshimu ushauri wa kitaalamu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Kutokana na shinikizo hilo , Bodi ya Zabuni ya TANESCO iliwekwa pembeni na TANESCO ikaagizwa kuvunja sheria kwa kuwabadilisha wajumbe wa Bodi yake ya Zabuni.

Wizara ya Nishati na Madini pia ikafanya uamuzi wa
ununuzi kwa niaba ya TANESCO na kuulazimisha uongozi wake kusaini mkataba na kampuni ( Richmond ) ambayo TANESCO waliikataa mara tatu kwa vigezo vya kitaalamu kuwa haifai kwa kazi hiyo.

Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za Bunge zilizonukuu taarifa ya Mwakyembe “Huo ulikuwa udhalilishaji mkubwa wa viongozi na watendaji ndani ya TANESCO”.

Jambo jingine la kutilia shaka ni taarifa kwamba mwezi mmoja kabla ya zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura, Wizara ya Nishati na Madini iliiandikia Richmond Development Company LLC kuitaarifu kuwa imeshindwa kutekeleza mkataba baina yake na Wizara kuhusu mradi wa bomba la mafuta.

Kutokana na hali hiyo, kimya cha Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC, kuliipa Kamati Teule shaka kuhusu uadilifu wa viongozi wa Wizara.

Source: Raia Mwema 21, Januari 2009

Wednesday, January 21, 2009

OBAMA INAUGURATION SPEECH


My fellow citizens:
I stand here today humbled by the task before us, grateful for the trust you have bestowed, mindful of the sacrifices borne by our ancestors. I thank President Bush for his service to our nation, as well as the generosity and cooperation he has shown throughout this transition.
Forty-four Americans have now taken the presidential oath. The words have been spoken during rising tides of prosperity and the still waters of peace. Yet, every so often the oath is taken amidst gathering clouds and raging storms. At these moments, America has carried on not simply because of the skill or vision of those in high office, but because We the People have remained faithful to the ideals of our forbearers, and true to our founding documents.
So it has been. So it must be with this generation of Americans.
That we are in the midst of crisis is now well understood. Our nation is at war, against a far-reaching network of violence and hatred. Our economy is badly weakened, a consequence of greed and irresponsibility on the part of some, but also our collective failure to make hard choices and prepare the nation for a new age. Homes have been lost; jobs shed; businesses shuttered. Our health care is too costly; our schools fail too many; and each day brings further evidence that the ways we use energy strengthen our adversaries and threaten our planet.
These are the indicators of crisis, subject to data and statistics. Less measurable but no less profound is a sapping of confidence across our land - a nagging fear that America's decline is inevitable, and that the next generation must lower its sights.
Today I say to you that the challenges we face are real. They are serious and they are many.
They will not be met easily or in a short span of time. But know this, America - they will be met. On this day, we gather because we have chosen hope over fear, unity of purpose over conflict and discord.
On this day, we come to proclaim an end to the petty grievances and false promises, the recriminations and worn out dogmas, that for far too long have strangled our politics.
We remain a young nation, but in the words of Scripture, the time has come to set aside childish things. The time has come to reaffirm our enduring spirit; to choose our better history; to carry forward that precious gift, that noble idea, passed on from generation to generation: the God-given promise that all are equal, all are free, and all deserve a chance to pursue their full measure of happiness.
In reaffirming the greatness of our nation, we understand that greatness is never a given. It must be earned. Our journey has never been one of short-cuts or settling for less. It has not been the path for the faint-hearted - for those who prefer leisure over work, or seek only the pleasures of riches and fame. Rather, it has been the risk-takers, the doers, the makers of things - some celebrated but more often men and women obscure in their labor, who have carried us up the long, rugged path towards prosperity and freedom.
For us, they packed up their few worldly possessions and traveled across oceans in search of a new life.
For us, they toiled in sweatshops and settled the West; endured the lash of the whip and plowed the hard earth.
For us, they fought and died, in places like Concord and Gettysburg; Normandy and Khe Sahn. Time and again these men and women struggled and sacrificed and worked till their hands were raw so that we might live a better life. They saw America as bigger than the sum of our individual ambitions; greater than all the differences of birth or wealth or faction.
This is the journey we continue today. We remain the most prosperous, powerful nation on Earth. Our workers are no less productive than when this crisis began. Our minds are no less inventive, our goods and services no less needed than they were last week or last month or last year. Our capacity remains undiminished. But our time of standing pat, of protecting narrow interests and putting off unpleasant decisions - that time has surely passed. Starting today, we must pick ourselves up, dust ourselves off, and begin again the work of remaking America.
For everywhere we look, there is work to be done. The state of the economy calls for action, bold and swift, and we will act - not only to create new jobs, but to lay a new foundation for growth. We will build the roads and bridges, the electric grids and digital lines that feed our commerce and bind us together. We will restore science to its rightful place, and wield technology's wonders to raise health care's quality and lower its cost. We will harness the sun and the winds and the soil to fuel our cars and run our factories. And we will transform our schools and colleges and universities to meet the demands of a new age. All this we can do. And all this we will do.
Now, there are some who question the scale of our ambitions - who suggest that our system cannot tolerate too many big plans. Their memories are short. For they have forgotten what this country has already done; what free men and women can achieve when imagination is joined to common purpose, and necessity to courage.
What the cynics fail to understand is that the ground has shifted beneath them - that the stale political arguments that have consumed us for so long no longer apply. The question we ask today is not whether our government is too big or too small, but whether it works - whether it helps families find jobs at a decent wage, care they can afford, a retirement that is dignified. Where the answer is yes, we intend to move forward. Where the answer is no, programs will end. And those of us who manage the public's dollars will be held to account - to spend wisely, reform bad habits, and do our business in the light of day - because only then can we restore the vital trust between a people and their government.
Nor is the question before us whether the market is a force for good or ill. Its power to generate wealth and expand freedom is unmatched, but this crisis has reminded us that without a watchful eye, the market can spin out of control - and that a nation cannot prosper long when it favors only the prosperous. The success of our economy has always depended not just on the size of our Gross Domestic Product, but on the reach of our prosperity; on our ability to extend opportunity to every willing heart - not out of charity, but because it is the surest route to our common good.
As for our common defense, we reject as false the choice between our safety and our ideals. Our Founding Fathers, faced with perils we can scarcely imagine, drafted a charter to assure the rule of law and the rights of man, a charter expanded by the blood of generations. Those ideals still light the world, and we will not give them up for expedience's sake. And so to all other peoples and governments who are watching today, from the grandest capitals to the small village where my father was born: know that America is a friend of each nation and every man, woman, and child who seeks a future of peace and dignity, and that we are ready to lead once more.
Recall that earlier generations faced down fascism and communism not just with missiles and tanks, but with sturdy alliances and enduring convictions. They understood that our power alone cannot protect us, nor does it entitle us to do as we please. Instead, they knew that our power grows through its prudent use; our security emanates from the justness of our cause, the force of our example, the tempering qualities of humility and restraint.
We are the keepers of this legacy. Guided by these principles once more, we can meet those new threats that demand even greater effort - even greater cooperation and understanding between nations. We will begin to responsibly leave Iraq to its people, and forge a hard-earned peace in Afghanistan. With old friends and former foes, we will work tirelessly to lessen the nuclear threat, and roll back the specter of a warming planet. We will not apologize for our way of life, nor will we waver in its defense, and for those who seek to advance their aims by inducing terror and slaughtering innocents, we say to you now that our spirit is stronger and cannot be broken; you cannot outlast us, and we will defeat you.
For we know that our patchwork heritage is a strength, not a weakness. We are a nation of Christians and Muslims, Jews and Hindus - and non-believers. We are shaped by every language and culture, drawn from every end of this Earth; and because we have tasted the bitter swill of civil war and segregation, and emerged from that dark chapter stronger and more united, we cannot help but believe that the old hatreds shall someday pass; that the lines of tribe shall soon dissolve; that as the world grows smaller, our common humanity shall reveal itself; and that America must play its role in ushering in a new era of peace.
To the Muslim world, we seek a new way forward, based on mutual interest and mutual respect.
To those leaders around the globe who seek to sow conflict, or blame their society's ills on the West - know that your people will judge you on what you can build, not what you destroy. To those who cling to power through corruption and deceit and the silencing of dissent, know that you are on the wrong side of history; but that we will extend a hand if you are willing to unclench your fist.
To the people of poor nations, we pledge to work alongside you to make your farms flourish and let clean waters flow; to nourish starved bodies and feed hungry minds. And to those nations like ours that enjoy relative plenty, we say we can no longer afford indifference to suffering outside our borders; nor can we consume the world's resources without regard to effect. For the world has changed, and we must change with it.
As we consider the road that unfolds before us, we remember with humble gratitude those brave Americans who, at this very hour, patrol far-off deserts and distant mountains. They have something to tell us today, just as the fallen heroes who lie in Arlington whisper through the ages.
We honor them not only because they are guardians of our liberty, but because they embody the spirit of service; a willingness to find meaning in something greater than themselves. And yet, at this moment - a moment that will define a generation - it is precisely this spirit that must inhabit us all.
For as much as government can do and must do, it is ultimately the faith and determination of the American people upon which this nation relies. It is the kindness to take in a stranger when the levees break, the selflessness of workers who would rather cut their hours than see a friend lose their job which sees us through our darkest hours. It is the firefighter's courage to storm a stairway filled with smoke, but also a parent's willingness to nurture a child, that finally decides our fate.
Our challenges may be new. The instruments with which we meet them may be new. But those values upon which our success depends - hard work and honesty, courage and fair play, tolerance and curiosity, loyalty and patriotism - these things are old. These things are true. They have been the quiet force of progress throughout our history. What is demanded then is a return to these truths. What is required of us now is a new era of responsibility - a recognition, on the part of every American, that we have duties to ourselves, our nation, and the world, duties that we do not grudgingly accept but rather seize gladly, firm in the knowledge that there is nothing so satisfying to the spirit, so defining of our character, than giving our all to a difficult task.
This is the price and the promise of citizenship.
This is the source of our confidence - the knowledge that God calls on us to shape an uncertain destiny.
This is the meaning of our liberty and our creed - why men and women and children of every race and every faith can join in celebration across this magnificent mall, and why a man whose father less than sixty years ago might not have been served at a local restaurant can now stand before you to take a most sacred oath.
So let us mark this day with remembrance, of who we are and how far we have traveled. In the year of America's birth, in the coldest of months, a small band of patriots huddled by dying campfires on the shores of an icy river. The capital was abandoned. The enemy was advancing. The snow was stained with blood. At a moment when the outcome of our revolution was most in doubt, the father of our nation ordered these words be read to the people:
"Let it be told to the future world...that in the depth of winter, when nothing but hope and virtue could survive...that the city and the country, alarmed at one common danger, came forth to meet [it]."
America. In the face of our common dangers, in this winter of our hardship, let us remember these timeless words. With hope and virtue, let us brave once more the icy currents, and endure what storms may come. Let it be said by our children's children that when we were tested we refused to let this journey end, that we did not turn back nor did we falter; and with eyes fixed on the horizon and God's grace upon us, we carried forth that great gift of freedom and delivered it safely to future generations.

Tuesday, January 20, 2009

Mwaka mpya bila mabadiliko!

WIKI tatu zilizopita, tulifurahia mwaka mpya wa 2009. Furaha yetu iliambatana na matumaini mapya.

Wenye mipango iliyokwama mwaka uliopita, walifurahia mwaka mpya huku wakitafakari namna ya kukamilisha mipango hiyo.

Hakuna aliyejitabiria matatizo, wala aliyepanga kumsababishia mwenzake matatizo. Tulitakiana heri ya mwaka mpya kwa dhati. Tuliamini kuwa uzembe unaogharimu maisha yetu, hususan ajali zisizo za lazima, utapungua au kwisha.

Lakini dalili za awali mwanzoni mwa mwaka huu zinabainisha bado hatujawekeza vya kutosha katika matarajio yetu. Hususan matarajio ya kupunguza au kutokomeza ajali za barabarani.

Ndani ya wiki hizi takriban tatu, tumepoteza ndugu, jamaa na rafiki zetu ambao tulipeana heri ya Mwaka Mpya kwa furaha.

Tumewapoteza katika vifo vya wakina mama wajawazito na watoto,mauaji ya albino, ajali za barabarani, mkoani Tanga na katika maeneo mengine ya nchi. Wamekufa wakati wakiwa safarini kufanikisha juhudi zao za kusaka maendeleo binafsi na ya taifa.

Kutokana na hali hiyo, kikubwa tunachokiona sisi ni mauaji yameongezeka hasa ya albino na vikongwe, tumeingia mwaka mpya wakati fikra zetu katika kudhibiti ajali za barabarani tu peke yake.

Tupo ndani ya mwaka mpya bila kuwa na fikra mpya katika kujiepusha na mauaji ya albino na vikongwe pamoja na ajali za barabarani. Abiria na madereva wameendelea kuwa chanzo cha ajali za barabarani.

Sehemu kubwa ya ajali hizo chanzo chake ni mwendo kasi. Hii ni sababu iliyo ndani ya uwezo wa dereva pamoja na abiria.

Tunahimiza jamii, abiria, madereva na watendaji katika vyombo vya dola kukumbuka kuwa Taifa bila watu ni sifuri. Wakumbuke kuwa Taifa lenye maombelezo mfululilizo hususan yasiyo ya lazima, si taifa la kujivunia.

Katika mwaka 2009, abiria, madereva na vyombo vya dola tujitahidi kuhakikisha tunakuwa Taifa lenye kukomesha mauaji ya albino na vikongwe na pia kuwa na idadi ndogo ya ajali za barabarani Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika na hata barani Afrika.

Pamoja Tunaweza!

Mkakati wa GDSS 2009 kwa mtazamo wa ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

MUHTASARI WA SEMINA.
(GDSS)

TAREHE:- Semina hii ilifanyika jumatano ya tarehe 14/1/2009.

MADA:- Mkakati wa GDSS 2009 kwa mtazamo wa ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

WATOA MADA:
Anna Mushi - mtoa mada mkuu (TGNP
Lilian Liundi – mtoa mada mshiriki (TGNP).

MWEZESHAJI:- TGNP
MJADALA KWA UFUPI:-
Baada ya salamu na kutakiana heri ya mwaka mpya, utambulisho wa mada ulifuata na fursa kwa washiriki kuelezea mikakati yao kwa mwaka 2009 kuhusiana na namna watakavyo shiriki katika kuendeleza vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapindizi.

MALENGO KUTOKA KWA WASHIRIKI:-
• Kufanya ushawishi kwa wanawake wengi zaidi kuja kuhudhuria katika semina za GDSS ili kupanua wigo wa harakati za kumkomboa mwanamke.
• Kuhakikisha tekinolojia inamkomboa mwanamke.
• Kufanya maandalizi madhubuti katika kuhakikisha ufanisi wa tamasha la jinsia mwezi wa tisa (GF).
• Kutoa elimu zaidi kuhusu VVU na UKIMWI katika mikoa ya Singida na Dodoma.
• Kuhakikisha kilio cha yatima na wajane kinasikika vilivyo katika jamii.
• Kuandika habari/ makala nyingi zaidi zitakazowezesha ukombozi wa mwanamke.
• Kufanya ufuatiliaji wa kina kuhusiana na masuala ya huduma ya afya.

MJADALA KWA UREFU:-
Baada ya kumalizika kwa zoezi hilo, mtoa mada aliwataka washiriki kujigawa katika makundi matatu (3) na kujadili nini kifanyike ili kuboresha (GDSS) kwa mtazamo wa kumkomboa mwanamke kimapinduzi na kutoa mapendekezo matatu(3) yatakayojadiliwa kwa kina na kupata mapendekezo ya pamoja kwa utekelezaji zaidi.

MREJESHO:-
Baada ya mjadala wa kina kutoka kwa washiriki, yafuatayo yalikubaliwa kwa utekelezaji ili kukamilisha malengo ya washiriki katika kusukuma mbele vuguvugula ukombozi wa mwanamke kimapinduzi kwa mwaka 2009.


• Utunzaji wa kumbukumbu.
• Kutoa elimu ya nini maana ya ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.
• Kujitolea.
• Kuanzisha semina za maendeleo na jinsia (GDSS) katika maeneo yetu.
• Kufanya tathmini ya mara kwa mara kuhusu shughuli zetu.

HITIMISHO:-
Wakati wa kufanya hitimisho la semina, mambo matatu (3) yalijiri;
• Hitaji la kuwepo kwa kauli mbiu itakayo tumika kama utambulisho na kichochea hamasa kwa wana GDSS katika shughuli zote za kiharakati.
• Ushiriki wa watoto katika semina za maendeleo na jinsia (GDSS) na shughuli nyingine za kiharakati, maana uzoefu umeonyesha kuwapo na mkanganyiko ambao kwa hakika unahitaji ufumbuzi wa haraka.
• Hitaji la matumizi ya vyombo vya habari hasa television katika kuongeza hamasa kama ilivyokuwa awali ambapo (AGAPE TV) ilitumika kufanya hivyo mwaka 2007.

Mwisho washiriki walikumbushwa kuhusu faida za kufanya kazi kwa ushirikiano ambapo walielezwa kuwa kutawaletea tija haraka na baadaye kusisitizwa kualika watu wengi zaidi kushiriki katika semina zetu.

Thursday, January 15, 2009

Hatumchunguzi Mkapa - TAKUKURU


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kwamba haimchunguzi rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwa “ tuhuma yoyote ya kijinai”.

Taarifa ya TAKUKURU kwa vyombo vya habari, iliyosambazwa jana Jumanne, ilisema: “Katika siku za hivi karibuni kumekuwapo na uvumi ambao umekuwa ukitolewa katika baadhi ya vyombo vya habari mbalimbali vya habari ukibeba ujumbe kwamba rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, anachunguzwa na vyombo vya dola ikiwamo TAKUKURU.

“TAKUKURU inawafahamisha wananchi kwamba uvumi huu hauna ukweli wowote. TAKUKURU haimchunguzi kiongozi huyu kwa kosa au tuhuma yoyote ya kijinai kama inavyodaiwa”.

Taarifa hiyo ya TAKUKURU ilisema kwamba kwa mujibu wa Ibara ya 46 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 haiwezi kumchunguza Mkapa.

Iliongeza taarifa hiyo ikinukuu Katiba: “Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ia ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilolifanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba hii.”

Ilisema kwa msingi huo wa Katiba, TAKUKURU “imeona ni vyema kuwafahamisha wananchi ukweli dhidi ya uvumi huu. Tukumbuke wakati wote kwamba Taifa letu lina Katiba ya nchi ambayo imeweka misingi mikuu ya kuendesha nchi, haki na wajibu wa kila Mtanzania”.

Raia Mwema Disemba 24, 2008

Wednesday, January 14, 2009

Bosi wa Richmond apandishwa kizimbani


NAEEM ADAM GIRE

MFANYABIASHARA NAEEM ADAM GIRE AMEFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU JIJINI DAR LEO AKIKABILIWA NA MAKOSA YA KUGUSHI, KUTOA HATI ZA UWONGO NA KUTOA TAARIFA ZA UWONGO KUHUSU UWEZO WA KAMPUNI YA RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY KUWA NA UWEZO WA KUZALISHA 100MW ZA UMEME TANZANIA.

MBELE YA HAKIMU MKAZI MH. WARIARWANDWE LEMA, MSHTAKIWA AMEKANA MASHITAKA NA AMEPELEKWA RUMANDE HADI KESHO WAKATI OMBI LAKE LA DHAMANA LITASIKILIZWA.

HII IMEKAAJE WANAHARAKATI WENZANGU?

Tuesday, January 13, 2009

Mtaalam: Anguko la uchumi limeanza kututafuna

WAKATI anguko la uchumi duniani likiwakutanisha nchini mawaziri na magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika pamoja na viongozi wengine wa kimataifa, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, mtaalamu wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja, amesema tayari Tanzania imeanza kuathirika mapema zaidi na anguko hilo kuliko ilivyotarajiwa.

Kauli hiyo ya Dk. Semboja inakuja wakati mkutano huo wa siku mbili ulionza jana (Machi 10) ukilenga kujadili jinsi ya kuliepusha Bara la Afrika na madhara ya mtikisiko wa uchumi unaondelea kutikisa nchi nyingi zikiwamo zile ambazo ni wafadhili wakuu wa Bajeti ya Tanzania.

Kwa mujibu wa gwiji huyo wa uchumi, athari za kiuchumi dhidi ya Tanzania zimeanza kujitokeza wazi wazi katika nyanja za uwekezaji, ajira, biashara na hata katika siasa na zaidi, athari hizo zinaonyesha dalili za kuzidi kumomonyoa maadili ya jamii.

Katika maelezo yake, yatakayochapishwa katika toleo la wiki ijayo la gazeti hili, Dk. Semboja anabainisha baadhi ya athari za mapema dhidi ya Tanzania kuwa ni pamoja na kupunguza wafanyakazi, viwango vya mishahara kwa watumishi wanaobaki na hata kupunguza gharama za uzalishaji.

Anasema athari za wazi zimeanza kujitokeza mwanzoni mwa mwaka huu ambazo zinajumuisha kupungua kwa ajira na kupungua kwa vipato.

Mbali na hali hiyo, anasema ya kuwa kutokana na mtikisiko huo wa kiuchumi duniani,

sekta isiyo rasmi nchini itaendelea kubabaika hasa ikizingatiwa kuwa watu wengi hukimbilia kuwekeza mitaji katika sekta isiyo rasmi, kama kinga au njia ya kujikwamua kiuchumi na kujinusuru katika migogoro hii.

Kwa mujibu wa Dk. Semboja, ingawa kuna dalili ya ukuaji wa sekta isiyo rasmi katika maeneo mengi ya mijini na vijijini, sekta ambayo kila mara ni wastaafu, wanawake na vijana ndiyo wanaothubutu kushiriki katika sekta, tatizo linalojidhihirisha ni kuwa waliomo katika sekta hiyo wengi wao hawana takwimu na taarifa kuhusu masoko yao, hawana ujuzi wala uzoefu wa mwenendo wa sekta hiyo na hali hiyo inawaweka katika hatari ya kushindwa na hatimaye kuanguka mara tu wanapoingia.

Kwa upande wa athari za kisiasa, mtaalamu huyo anasema mtikisiko wa uchumi duniani umeanza kuonyesha athari, ambazo zinaweza kuvuruga amani na usalama wa raia na Taifa.

Ndani ya hoja ya mtikisiko wa uchumi, Dk. Semboja anaamini kuwa yapo mambo kadhaa yanayoweza kuisukuma jamii ya Watanzania katika athari zaidi.

“Tuhuma za viongozi mafisadi, mauaji ya jamii ya albino, ongezeko la watu wasioajiriwa, umasikini na ufukara uliokithiri katika jamii ni dalili mojawapo zinazoashiria kuwa usalama wa raia na Taifa uko hatarini,” anasema Dk. Semboja akiongeza: “Dalili nyinginezo ni pamoja kuongezeka kwa kashfa kwa viongozi wa kisiasa katika rushwa.”

Lakini anaamini kuwa dalili nyingine ni udhaifu wa Serikali katika kutatua matatizo ya kikatiba na kimsingi, kama vile huduma duni za afya, elimu, maji, nishati na matusi, kejeli na chuki binafsi kati ya viongozi.

Anaonya Dk. Semboja: “Hali inaweza kutumika kama sababu za kimsingi za kidemokrasia kutaka mabadiliko ya utawala wa kisiasa katika mchakato wa upigaji kura wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwakani.”

Kwa mujibu wa Dk. Semboja, athari nyingine zitajitafsiri katika kuendelea kubomoka kwa maadili ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea zaidi umalaya, uhalifu, na tabia mbaya za ulevi na utamaduni wa kisasa.

Anasema pia kwamba kuongezeka kwa demokrasia, taarifa na takwimu, maarifa, na maendeleo ya Teknohama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) kumebadilisha mwono, mila na desturi za jamii. Jamii zinatambua haki zao za kimsingi na uhuru wao kisheria.

Hata hivyo, Dk. Semboja anasema kwa bahati mbaya wapo wengi ambao hawajui mipaka na wajibu wao, hivyo kufanya tabia na maadili kuporomoka.

“Kwa mfano imekuwa hakuna tofauti kati ya wazee na vijana katika masuala ya ngono zembe, ulevi, uvivu, na nia za kutaka kupata utajiri wa haraka haraka kwa taratibu zisizo za kisheria. Mitikisiko, migogoro na athari za kijamii na uchumi wa utandawazi huu unaweza kuchochea au kukuza athari hizi mbaya za kijamii,” anasema.

Lakini anasema wakati kwa upande wa kijamii na kisiasa hali ikiwa hivyo, athari kwa upande wa sekta nyeti za uchumi wa nchi kama kilimo, utalii na madini zimezidi kuwa kubwa tofauti na ilivyotarajiwa na watalaamu wa uchumi mwishoni mwa mwaka jana.

Katika kilimo, taarifa zinaonyesha kuwa bei ya kahawa aina ya arabika na kokoa zimeshuka katika soko la dunia. Arabika imeshuka kwa asilimia 24 wakati kokoa ikiporomoka kwa asilimia 27, kati ya Julai mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu.

“Inaonekana kuwa bidhaa muhimu za kilimo cha biashara zitashuka katika kipindi cha mwaka 2009. Kushuka kwa bei za bidhaa hizi muhimu kutasababisha athari ya kushuka kwa mapato ya biashara za nje,” anasema Dk. Semboja.

Anasema kutokana na kushuka kwa bei na wingi wa uzalishaji wa bidhaa za kilimo cha biashara za nje ya nchi, ni wazi kuwa mapato ya Serikali, Pato la Taifa (GDP), kupungua kwa ajira na kuongezeka kwa umasikini ni mambo yatakayoiumiza Tanzania.

Anasema katika utafiti wake huo ya kuwa katika kipindi cha mwanzo wa mwaka huu, mtikisiko wa kiuchumi umepunguza kasi ya mahitaji ya watu wa nchi zilizoendelea kupanga safari na utalii Tanzania.

Hapa, Dk. Semboja anasema: “Ni vema kutambua kuwa pamoja na kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii, kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama nyingi, pwani nzuri, kisiwa cha Zanzibar na Pemba, utalii wetu uko chini, mdogo na ukuaji wake ni dhaifu ukilinganisha na nchi kama vile Kenya na Afrika Kusini.

“Sababu kubwa ya utalii duni hapa nchini ni pamoja na kuwa na miundombinu mibaya, kodi kubwa, huduma na bei mbaya za hoteli na usafiri na gharama kubwa kwa watalii.

“Hivyo, mtikisiko wa kiuchumi utaweza kuwa na athari kubwa katika maeneo ambayo watalii wataona kuwa fedha zao hazitapata huduma bora wanazohitaji.”

Anasema katika sekta ya madini, hali si tofauti na katika sekta ya kilimo na utalii. Mtikisiko kiuchumi duniani umeshusha bei za madini na kupunguka kwa mahitaji ya madini katika masoko katika nchi zilizoendelea.

Hali ya kushuka kwa bei za madini na kupunguka kwa mahitaji vimeathiri shughuli za uchimbaji, biashara na uwekezaji katika sekta ya madini.

Hapa nchini, tayari baadhi ya kampuni za uchimbaji wa dhahabu zimeanza kupunguza shughuli na ajira kama mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji.

Inaelezwa kuwa hali ikiwa mbaya zaidi, Marekani, Ulaya, China na India zinaweza kusitisha uwekezaji wa moja kwa moja nchini kwa kuhofia kupotea kwa mitaji na kupata hasara, hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania haina mazingara endelevu ya uzalishaji na kibiashara.

Anasema hatari kubwa zaidi katika Bajeti ijayo ya Serikali ni kwamba misaada kutoka kwa wahisani inaweza kupungua na kwamba mambo yakiendelea kuharibika zaidi, wahisani wenye nia njema watakuwa na kipato kidogo cha kutoa kama msaada.

Anasema Dk. Semboja: “Imekuwa rahisi kwa nchi zilizoendelea kukata matumizi ya serikali zao kwa kupunguza misaada inayokwenda nchi zinazoendelea.

“Kuna wahisani wa aina nyingi. Wapo wale wanaosadia katika kutoa misaada na mikopo bila masharti na riba kubwa. Wako wale ambao wapo tayari kutoa misaada ya mikopo kwa masharti ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na kibiashara na riba kubwa. Hili kundi la pili, ndilo lilovuna katika migogoro na kuneemeka.”

Anasema kwa Watanzania wa kawaida, hasa wajasiriamali, hali inaweza kwenda kombo kwa upande wao na hasa kutokana na onyo lilitolewa kwa benki za biashara nchini.

“Mabenki ya biashara ya kigeni yaliyomo nchini yameanza kupata joto la kutakiwa kuwa makini katika kutoa mikopo midogo kwa ajili ya shughuli za biashara ndogondogo hapa Tanzania.

“Hapa awali walikuwa wepesi kutoa mikopo aina ya msaada kwa ajili ya sekta binafsi inayoendeshwa na wazalendo, tofauti na sasa. Hii itachangia kusimamisha uwekezaji wa wazalendo kwa ajili ya maendeleo yao.

Raia Mwema,Machi 11,2009.

Hii ni demokrasia inayopanuka

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepitisha uamuzi kuwa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani sasa watakuwa wakipigiwa kura za maoni na kila mwanachama, badala ya utaratibu wa zamani uliokuwa ukiwaruhusu wajumbe wachache kushiriki kupitia mikutano mikuu ya majimbo.

Kwamba, utaratibu mpya unatoa nafasi kwa kila mwanachama wa chama hicho kupiga kura katika tawi lake na hivyo kuwa vigumu kwa wagombea kuwahonga wanachama katika matawi yote katika jimbo husika.

Sambamba na uamuzi huo, CCM pia imepitisha uamuzi wa kuongeza uwakilishi wa wanawake katika Bunge na Baraza la Wawakilishi, ili idadi ya wanawake katika vyombo hivyo iwe asilimia 50 ya wabunge au wawakilishi wote wanaochaguliwa.

Tunachukua fursa hii kupongeza uamuzi huo uliofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kwa sababu ni njia mojawapo ya kuziba mianya ya rushwa ambayo ilikuwa ikitumiwa na baadhi ya wagombea kuwarubuni wapiga kura, kwa kuwa walikuwa wachache na walikuwa wakipatikana kwenye eneo mmoja.

Kitendo cha kuwakutanisha wanachama wachache wa CCM kwenye mkutano mmoja wa jimbo kilikuwa kinatoa fursa miongoni mwa wagombea kutoa fedha kwa urahisi na hivyo kuifinya demokrasia ya kupata viongozi bora na waadilifu.

Utaratibu huo mpya pia unapanua demokrasia kwa kuwashirikisha watu wengi zaidi katika kupiga kura za maoni na hivyo kupanua nafasi ya kila mwanachama kumchagua kiongozi anayemtaka, badala ya utaratibu wa kuwakilishwa kwenye mikutano ya majimbo, ambako wanachama wenye uchu na fedha walirubuniwa kwa urahisi.

Lakini pia tunachukua fursa hii kupongeza juhudi za kuongeza idadi ya uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya kutunga sheria kufikia asilimia 50 ya wabunge, wawakilishi na madiwani. Hii pia ni hatua nzuri ya kupanua demokrasia na kuongeza sauti za wanawake katika vyombo hivyo vya wananchi.

Jambo la msingi ni kwa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupokea mapendekezo ya CCM ili kurekebisha katiba za pande hizo mbili na sheria zake za uchaguzi, mapema iwezekanavyo, ili mabadiliko hayo yaweze kutumika katika uchaguzi mkuu ujao, tupate safu nzuri za viongozi.

Tunachukua nafasi hii pia kuvishauri vyama vingine vya siasa kuwa na taratibu za wazi za kupanua demokrasia kwa kushirikisha wanachama wao wengi zaidi katika michakato ya kupata viongozi wa vyama na hata wabunge, wawakilishi na madiwani.

Ni kwa njia hii sisi kama nchi tutakuwa na haki ya kujivunia mifumo yetu ya kupata wawakilishi wa wananchi na hata viongozi katika ngazi mbali mbali nchini.

Siri ya Zitto na Ngeleja yavuja

WAKATI hali ya umeme nchini ikiwa bado tete, barua ya siri kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuhusiana na sakata la umeme na hali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imevuja.

Barua hiyo inagusia ushauri wa kamati ya POAC kwa Serikali kuhusiana na kukabiliana na hali ya umeme, ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali kuingilia kati na kuinusuru Tanesco kifedha, bila kugusia mitambo ya Dowans ambayo imekua gumzo kwa sasa.

Ndani ya barua hiyo ya mwishoni mwa mwezi uliopita, ambayo Raia Mwema imeiona, Zitto, kwa niaba ya kamati yake, ameishauri Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwapo msaada wa dharura kwa Tanesco ili ijikwamue katika tatizo kubwa la kifedha na kuisaidia kununua mitambo ya kuzalishia umeme inayofaa bila kukiuka sheria za nchi.

“Kamati inawasilisha kwako ushauri wa kuiomba Serikali iiwezeshe Tanesco kununua mitambo ya umeme inayoona inafaa kulingana na mahitaji yake na bila kukiuka sheria za nchi ili kuliokoa Taifa kuingia kwenye giza na hivyo kuathiri uchumi wa taifa letu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo kutoka kwa Zitto.

Zitto, ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa shughuli za chama chake, alikataa jana kuzungumzia kuhusiana na kuvuja kwa barua hiyo akisema: “…nilikuwa nje ya nchi na nimekuja moja kwa moja huku Machame kwa shughuli za chama.”

Kuvuja kwa barua hiyo kunakuja wakati Zitto anatajwa kama mmoja wa wanasiasa wanaoiunga mkono Tanesco katika mpango wake wa kununua mitambo ya Dowans, msimamo ambao umezua utata na kumuweka pabaya kisiasa, lakini alipoulizwa kuhusiana na msimamo wake kwa sasa alisema: “Msimamo wangu ni kuona nchi haipati giza na Watanzania wajifunze kuwa na viongozi ambao wana mawazo tofauti na wengi.”

Ndani ya barua hiyo, ambayo nakala yake imepelekwa kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, kuna maelezo yanayoonyesha jinsi shirika hilo la umeme lilivyo na hali mbaya kifedha kutokana na sehemu kubwa ya mapato kutumika kununua umeme kutoka kampuni binafsi zinazozalisha umeme nchini.

Kuhusiana na ushauri wa serikali juu ya ununuzi wa mitambo barua hiyo inaeleza: “Kamati inapenda kuikumbusha Serikali kuwa maamuzi ya kununua mitambo ni maamuzi ya Serikali na si ya Kamati ya Bunge. Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali na si utendaji wa kila siku. Kamati yangu imetoa ushauri huu kuisaidia Tanesco kupunguza gharama za kununua umeme na kuongeza mapato yake kwa kutekeleza mpango wake wa wateja 100,000 kwa mwaka. Tanesco hawataweza kuunganisha umeme kwa wateja 100,000 kwa mwaka kama hakuna umeme wa kuwapatia.”

Habari zaidi kutoka ndani ya Kamati ya Zitto zinaeleza kwamba baadhi ya wajumbe wameonyesha kuchanganywa na taarifa za vyombo vya habari zilizomnukuu Mwenyekiti wao akizungumzia Dowans wakati kamati haikuwa na maamuzi kuhusiana na kampuni hiyo.

Miongoni mwao ni Makamu Mwenyekiti wa Zitto, Mbunge wa Mbarali, Esterina Kilasi, ambaye alinukuliwa wiki hii akisema kwamba kamati haikuwa na maamuzi yoyote kuhusiana na Dowans.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo aliliambia Raia Mwema kwamba wajumbe wengi waliozungumzia suala la mitambo walibainisha kwamba Tanesco ni lazima inunue mitambo mipya na izingatie sheria.

“Baada ya Tanesco kuzungumzia dhamira yake ya kutaka kununua mitambo ya Dowans, tuliwaambia kwamba suala la kununua ama kutonunua ni suala la kiutendaji linalotakiwa kuzingatia sheria, ubora wa kitu kinachotakiwa kununuliwa na taratibu zifuatwe na tuliwasisitizia kwamba kazi ya Kamati na Bunge ni kusimamia,” alisema Mbunge huyo.

Mbunge huyo ambaye alikataa kutajwa jina kwa kuwa si msemaji wa Kamati, alisema waliwaeleza Tanesco waziwazi kwamba kitendo chao cha kufika katika Kamati kutaka mpango wao wa kununua mitambo upate baraka, hakikua sahihi.

“Tulisikiliza nia ya shirika dhidi ya mitambo hiyo lakini hatukubariki ununuzi huo. Uamuzi wa kamati ni kuishauri Serikali kununua mitambo mipya kwa ajili ya tahadhari na kukabiliana na tatizo la umeme linaloweza kujitokeza kama Tanesco walivyoonya, lakini kwa kuzingatia ubora, sheria, kanuni na taratibu za manunuzi,” alisema.

Mbali ya Zitto na Kilasi, wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Felister Bura, Diana Chilolo, Raphael Chegeni, Bahati Abeid, Emmanuel Luhahula, James Musalika, Peter Serukamba, Juma Njwayo, Tatu Ntimizi, Hafidh Ali Tahir, Elisa Mollel, Zaynab Vullu, Mwanawetu Zarafi, Mwadini Abass Jecha na Shally Raymond.

Mbali ya kutoa ushauri kwa Serikali, Kamati ya Zitto ilipendekeza kuwapo kwa kikao cha pamoja na kamati ya Nishati na Madini, maombi ambayo yalikataliwa na Spika Sitta, ambaye alibainisha wazi kwamba hakukuwa na sababu ya kikao hicho baada ya Kamati ya Nishati na Madini, inayoshughulikia sekta hiyo, uamuzi ambao unaelezwa kukubalika na kamati zote.

Tayari Tanesco wamekwishasitisha mpango wao wa kununua mitambo ya Dowans, lakini kwa taarifa ambayo ilitoa kitisho kwa wananchi kwamba kutakuwa na tatizo kubwa la umeme litakaloathiri sekta nyingi za huduma na uzalishaji.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa na Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Idris Rashid iliibua mjadala mpya wa kumtaka ajiuzulu kutokana na kutowajibika na kuutisha umma.

Katika tamko lake Dk. Rashid alisema: “Tanesco inatangaza rasmi kujitoa kwenye nia yake ya kununua mitambo hii. Ni imani yetu kwamba tumekwisha kujieleza na kujenga hoja za kutosha, na wananchi wa Tanzania, watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, hospitali hazitoi huduma, viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu tulishindwa kufanya maamuzi".

Sakata la Dowans limeibua mjadala mkali nap engine mgawanyiko wa wazi uliotokana na kauli za kukinzana kati ya wabunge wa kamati mbili ya POAC na ile ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM), William Shellukindo, anayesaidiwa na mwanasiasa machachari, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe tofauti ambazo zimejitokeza zaidi katika vyombo vya habari.

Shellukindo na Mwakyembe wote walionyesha kushitushwa kwao na taarifa za kamati ya Zitto kujihusisha na masuala ya kisera badala ya kupitia hesabu huku wakihusisha hatua hiyo na mikakati ya kisiasa.

Dk. Mwakyembe ndiye aliyesema kwamba upo uwezekano wa suala hilo kutumika kama sehemu ya kampeni za kisiasa za Chadema ambako Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wake, lakini Zitto akanukuliwa akisema suala hilo halina chembe ya siasa mbali ya maslahi ya Taifa.

Baada ya kauli za wabunge hao, Spika Sitta alifunga mjadala kwa kuishauri serikali kuachana na ununuzi wa mitambo ya Dowans kwa kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Raia Mwema, Machi 11,2009.

Dokezo: Rais amedhalilishwa sakata la Dowans

HAKUNA haja kwa Watanzania kusubiri nchi iingie gizani ndipo waamue kama alivyosema Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dk. Idris Rashid. Kwa nini tusubiri giza ili tuamue wakati tunaweza kuamua sasa? Tufanye uamuzi mmojawapo kati ya mambo mawili.

Mosi, awajibishwe Dk. Rashid na wenzake kwa sababu walikwenda likizo (uzembe) na waliporejea ofisini ghafla wakabaini ni lazima wanunue mitambo ya Dowans. Pili, kama Rais Jakaya Kikwete hatawawajibisha hawa ambao wamepuuza ahadi yake ya Mei 9, 2006 kwa Watanzania, basi tuanze kujutia kura zetu zilizompa ushindi aongoze Ikulu.

Ni aibu kiongozi tuliyempa jukumu la kiutendaji kuratibu sekta ya umeme, akakosa kuwa na kile kinachoweza kuitwa “plan B.”

Tutakuwa watu wa ajabu kama tutakumbatia ushauri wa Dk. Rashid, wa kusubiri maisha ya giza, hospitali kukosa umeme, viwanda kushindwa kuzalisha na wanafunzi kushindwa kusoma.

Yapo maswali mengi yanayoibuka katika sakata la Dowans. Mosi, kwa nini Dk. Rashid na wenzake katika Tanesco wakose mbinu mbadala licha ya kuongoza shirika hilo kwa miaka kadhaa?

Kwa nini leo hii aibuke na kuonya kuwa kuna dharura ya umeme, na lazima inunuliwe mitambo ya Dowans?

Natambua kuwa Dk. Rashid ametoa sababu za kwa nini lazima anunue mitambo ya Dowans akisema ni kutokana na ufinyu wa muda na dharura.

Binafsi naamini kuwa sababu hii ni sehemu ya mpango wa kuhalalisha malengo ya muda mrefu ya kununua mitambo ya Dowans. Imani yangu hiyo inatokana na ukweli kwamba Tanesco imekuwa na wanasheria wake au ina uwezo wa kukodi wanasheria kama ilivyofanya wakati wa kuvunja mkataba kati yake na Dowans, Agosti mosi, mwaka 2008.

Je, Dk. Rashid alishindwa kuomba ushauri wa kisheria tangu mwaka jana kwamba anaweza au hawezi kununua mitambo ya Dowans bila kuvunja sheria za nchi?

Je, hakujua kuwa kuna zuio la Mahakama lililowekwa na Tanesco dhidi ya mitambo ya Dowans? Lakini pia je, hakujua kuwa Dowans imeshitaki katika Mahakama ya Usuluhishi, jijini Paris, Ufaransa?

Kubwa zaidi, tujiulize na kutafakari, je, Dk. Rashid na wenzake walikuwa katika likizo ya muda mrefu kiasi gani ? Likizo ambayo mara baada ya kwisha waliporejea ofisini ghafla wakabaini hakuna njia yoyote mbadala zaidi ya ununuzi wa mitambo ya Dowans hata kama ni kuvunja sheria, ikiwamo Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004?

Nyuma ya uamuzi wa Rais


NJAA ya wadokozi ambao siku hizi ni maarufu kwa jina la mafisadi, imegharimu kwa kiasi kikubwa maisha ya raia wa kawaida nchini.

Kodi anayolipa raia huyo kwa mfano, wakati anaponunua chumvi au sukari dukani imekuwa ikidokolewa na mafisadi kwa kipindi kirefu sasa.

Kodi hiyo imekuwa ikidokolewa na kwa kutumia mbinu za kifisadi, imekuwa ikigharimia miradi ambayo mwishowe hunufaisha mafisadi.

Miradi kama ya kuzalisha umeme wa dharura, ununuzi wa rada ya kijeshi kwa bei ya juu na hata ununuzi wa ndege ya Rais.

Fedha za malipo kwa miradi au ununuzi wa mali hizo zimekuwa zikitoka katika fuko (hazina) lililokusanya kodi ya raia.

Raia huyo ni pamoja na mkulima aliyenunua kiberiti na mafuta ya taa dukani, kwa ajili ya kuwashia kibatari chake kijijini.

Ndiyo! Hapa nchini kila mmoja ni mlipa kodi hata mtoto mchanga. Mzazi analazimika kumlipia mtoto wake mchanga kodi, na hasa anaponunua mahitaji ya mtoto huyo.

Ukweli ni kwamba karibu kila bidhaa inayouzwa dukani nchini inatozwa kodi kabla ya kumfikia mlaji. Iwe bidhaa inayozalishwa nchini au inayoingizwa kutoka nje ya nchi.

Na bidhaa inapomfikia mlaji, kiwango cha awali cha kodi kilichotozwa humwangukia mlaji huyo. Hivyo unaweza kusema karibu kila mtu nchini ni mlipa kodi.

Na kwa maana hiyo kila mtu nchini anapaswa kuchukizwa na ufisadi wa aina yoyote. Huzuni au hasira ya raia wa Tanzania dhidi ya ufisadi haiwezi kutulizwa kwa nadharia bali kwa vitendo.

Matukio ya ufisadi yaliyokwisha kutokea awali ni majereha yanayoweza kuponywa lakini yakaacha makovu. Tunaweza kuyaponya majeraha hayo kwa kurejesha kilichoibwa na kuwachukulia hatua wahusika, lakini hatuwezi kusahau tabia yao hiyo ya udokozi katika historia ya nchi.

Tafakari yangu kuhusu safari ya vita dhidi ya ufisadi ililazimika kuingia katika ukurasa mpya baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya salamu za mwaka mpya.

Kati ya mambo aliyozungumzia Rais Kikwete katika hotuba yake ya Desemba 31, mwaka jana, ni kuhusu majukumu mapya kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Kwa mujibu wa Rais, Katibu Mkuu Kiongozi sasa atakuwa na majukumu mapya. Atakuwa akisikiliza malalamiko ya wawekezaji (bila shaka wale wa ughaibuni).

Rais ameeleza sababu za kufanya uamuzi huo. Akasema ni kutokana na kuwapo kwa dalili za wazi kuwa Tanzania imeanza kupoteza imani kwa wawekezaji.Uamuzi huo ni wa busara lakini pia umenifanya nijiulize maswali. Msingi wa kujiuliza maswali hayo ni kutokana na ukweli kwamba nchini kuna Kituo cha Uwekezaji (TIC). Kituo ambacho kimewahi kupewa tuzo kutokana na kile kilichowahi kuelezwa kuwa kufanya kazi yake kwa ufanisi, iweje basi leo hii Rais ambebeshe majukumu ya ziada Katibu Mkuu Kiongozi? Majukumu ambayo bila shaka yangeweza kubaki chini ya TIC?

Ni lazima kuna jambo halipo sawa, kuna kasoro. Lakini ni jambo gani hilo? Je, mambo si swari TIC? Au uaminifu umeota mbawa katika chombo hicho cha kuratibu uwekezaji na wawekezaji nchini? Je, chombo hiki hakina uwezo tena wa kusikiliza malalamiko ya wawekezaji? Katika hali ya kawaida na kama TIC ingekuwa na ufanisi usiotia shaka ni wazi kuwa Rais angeagiza jukumu la kusikiliza malalamiko ya wawekezaji kufanywa na chombo hicho, nilimsikiliza vizuri Rais Kikwete, alikuwa wazi zaidi katika hotuba yake, akasema wawekezaji wamekuwa na malalamiko mengi. Na kwa kuzingatia kukiri huko kwa Rais kuwa wawekezaji wamekuwa na malalamiko mengi ni wazi kuwa TIC imezembea kiutendaji,na kama si kuzembea basi ushauri wake kwa baadhi ya watendaji serikalini umekuwa ukipuuzwa. Lakini kama hali ni hiyo, ni nani hao wapuuzaji ndani ya Serikali? Ni makatibu wa wizara zipi, au mawaziri wa wizara gani?

Kwa nini malalamiko yawe mengi wakati chombo hicho (TIC) kikiendelea kuishi, tena kikiwa na watalaamu waliobobea? Watalaamu walioshiriki mafunzo mbalimbali kuhusu masuala ya uwezekazaji? Kwa nini malalamiko ya wawekezaji yawe mengi wakati mbali na kuwapo kwa TIC, kuna wizara mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya kisekta yanayogusa wawekezaji?

Kama utafanya tafakari ya kina utabaini kuwa uamuzi huu wa Rais unathibitisha kuwa kuna tatizo la msingi ndani ya mfumo wa kuratibu shughuli za wawekezaji,utabaini kuwa kuna tatizo ndani ya mfumo mzima wa kiutendaji serikalini. Na inawezekana hakuna mawasiliano mazuri ya kitaalamu kati ya baadhi ya taasisi na wizara.

Ni dhahiri kuwa kuna nguvu zinazopingana kimalengo ndani ya Serikali. Kwa mfano, ni wazi kuwa mantiki ya uwezekezaji nchini imeibua kambi mbili zenye mgongano, kuna kambi inayotumia mchakato wa kukaribisha wawekezaji nchini kwa maslahi binafsi, lakini pia kuna kambi inayohakikisha Taifa linanufaika wawekezaji kwa kiwango cha juu.

Na ukweli ni kwamba matokeo ya kambi hizi ni uamuzi wa Rais kutaka malalamiko ya wawekezaji yasikilizwe na Katibu Mkuu Kiongozi. Hakika uamuzi huu ni ishara kwamba kuna kasoro kubwa katika mfumo wa utendaji serikalini. Ni dhahiri kuwa uadilifu umekuwa bidhaa adimu serikalini.

Uamuzi huu wa Rais ni unazua maswali mengi zaidi kwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi sasa atakuwa akisikiliza malalamiko ya awali ya wawekezaji, na si rufaa za malalamiko ya wawekezaji.

Ningemwelewa zaidi Rais Kikwete kuhusu uamuzi wake huu kama angetangaza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi atasikiliza rufaa za malalamiko ya wawekezaji.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Na Godfrey Dilunga
Raia Mwema, 9 Januari 2009

Mgongano wa kimaslahi na ufisadi unaoitesa nchi yetu

MARA kadhaa tumesikia viongozi wetu waandamizi na hata mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete akielezea dhamira ya Serikali yake kupeleka mswada bungeni unaozuia kuchanganya siasa na biashara.

Hili pengine linaweza kuwa ni jibu muafaka kwa matatizo yanayolitesa Taifa; ulaji wa rushwa, matumizi mabaya ya ofisi za umma na ufisadi unaotishia amani, umoja na utulivu wa nchi.

Mara kadhaa mimi na wengine pia hupenda kusema nchi yetu ipo njia panda; yale yanayotokea sasa hayajawahi kushuhudiwa kwa muda mrefu au hayajawahi kutokea kabisa katika historia ya nchi. Ni njia panda, kabla hatujafika huko tunapotaka kufika katika Tanzania ile yenye neema na maisha bora kwa watu wake.

Kitafsiri mgongano wa kimaslahi ni ile hali inayojitokeza pale mtu aliye katika nafasi fulani ya kuaminiwa (mfano; mwanasiasa, mwanasheria, mhandisi n.k) anapokuwa na maslahi yanayokinzana, baina ya maslahi yake binafsi na nafasi aliyokuwa nayo.

Kukinzana huko kwa maslahi kunamuweka katika nafasi ngumu ya kufanya maamuzi bila ya kufanya upendeleo unaosukumwa na maslahi ya kibinafsi. Ikumbukwe mgongano wa kimaslahi unaweza kujitokeza hata pale ambapo hakuna uvunjwaji wa sheria au hata kukiukwa kwa maadili.

Mgongano wa kimaslahi unaweza kutengeneza picha ya upendeleo hata pale mhusika pengine hakuwa na nia ya upendeleo na hivyo basi kuiweka taaluma yake au cheo chake katika hali ya kutiliwa shaka.

Njia bora kabisa ya kupambana na mgongano wa kimaslahi ni kuuepuka moja kwa moja kwa kuepuka kujihusisha kabisa na biashara yoyote au taaluma yoyote baada ya kuteuliwa kushika ofisi ya umma.

Mfano, mwanasiasa aliyeteuliwa au kuchaguliwa kushika wadhifa fulani anaweza kuuza hisa zake zote katika mashirika au kampuni alizokuwa akishiriki. Au kwa namna nyigine anaweza kuzihamisha hisa hizo kwenda katika chombo cha udhamini kitakachokuwa kinaendelea na biashara bila ya ufahamu wake au yeye kuwa na ushawishi wa namna yeyote.

Wale wanaoona kwamba panaweza kutokea mgongano wa kimaslahi kwa wao kuwapo katika nafasi ya kimaamuzi au ushawishi inashauriwa ni bora wakakaa pembeni, na mtumishi muadilifu na mkweli ni yule ambaye pia atakuwa tayari kusema kwa uwazi kwa wenzake kuwa anajitoa katika kujadili suala husika kwa sababu kutakuwa na mgongano wa kimaslahi.

WANAHARAKATI WENZANGU MNALIONAJE HILI?

Friday, January 9, 2009

Waziri Chikawe awavaa wanaharakati


-Asema walishinikiza sheria mbaya ya kujamiiana mwaka 2002
-Afafanua kuwa inapingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1970
-Atamka serikali kuifanyia mabadiliko haraka iwezekanavyo

Serikali inapitia sheria ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) ya mwaka 2002 ili kupunguza adhabu kali zinazotolewa kwa watuhumiwa wanaotiwa hatiani kwa makosa ya kujamiiana, Rai limeelezwa.

Waziri wa katiba na sheria, Mathias Chikawe amesema pamoja na adhabu ya makosa hayo kuwa kali kwa adhabu ya chini kuwa kifungo cha chini ni miaka 30 na adhabu ya juu kuwa kifungo cha maisha gerezani, sheria hiyo pia inapingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1970.

Alisema wakati sheria ya ndoa ya mwaka 1970 inaruhusu binti wa miaka 15 kuolewa, sheria ya makosa ya kujamiiana inatamka kuwa msichana wa miaka 18 na chini ya umri huo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hiari au lazima ni kitendo cha kubakwa.

Waziri Chikawe alisema; "tunazitazama adhabu zinazotolewa kwa makosa ya ubakaji chini ya sheria ya makosa ya ubakaji ya mwaka 2002 ambazo ni mbaya kutokanana kutoa vifungo virefu na wakati huo ikipingana na sheria zingine halali za nchi".

Waziri Chikawe ambaye kitaaluma ni mwanasheria alisema sheria ya makosa ya kujamiiana ilipitishwa kwa shinikizo kubwa la wanaharakati waliokwenda kuweka kambi mjini Dodoma wakati muswada huo unawasilishwa imedhihirika kuwa na makosa mengi.

"Sheria ya SOSPA ilipitishwa wakati huo kukiwa kwenye wakati mgumu, wanaharakati walishinikiza ana kupitishwa kwa sheria hiyo na hali hiyo iliyofanya hata adhabu kuwa kali kutokana na mazingira yaliyotanda wakati huo lengo likiwa kulinda hadhi ya wanawake na watoto wa kike", anasema waziri Chikawe na kuongeza;

"Kutokana na upungufu huo, serikali sasa inapitia upya sheria hiyo kwa lengo la kurekebisha adhabu kwani zimebainika ni kali sana na hata mimi nakubaliana na wanaolia kwa adhabu hizo ambayo ni kifungo cha miaka 30 jela au kifungo cha maisha jela".

Kwa habari zaidi,
Gazeti la Rai, Januari 8-14, 2009
Ukurasa wa 1-3

Rais Kikwete aahidi kuzifanyia kazi sheria kandamizi


Hii ni sehemu tu ya hotuba ya Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa uchaguzi wa UWT

Ndugu Mwenyekiti;
Pamoja na kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi, yapo mambo ambayo yanahusu maendeleo ya wanawake ambayo inabidi yaendelee kufanywa sasa.
Sisi katika Serikali tumeweka vipaumbele katika mambo matano yahusuyo maendeleo ya mwanamke nchini:
La kwanza, ni lile nililolisemea hapo awali: la kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi. Katika kufanikisha jambo hili muhimu, kuna mambo yanayohitaji mabadiliko ya sheria. Na kuna yale ambayo tunaweza kuyafanya kwa maamuzi yetu sisi tuliyo madarakani sasa. Mimi nimekuwa nafanya hivyo kwa nafasi zinazoangukia katika mamlaka yangu ya uteuzi. Ndio maana leo tunao wanawake wengi katika nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi Watendaji, Majaji, na kadhalika. Naahidi kuendelea kufanya hivyo kadri fursa zinapojitokeza. Nasema hivyo kwa sababu wale tuliowapa nafasi wanawawakilisha vizuri.
Kwa upande wa nafasi za kuchaguliwa, ni muhimu wanawake nao wakajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi pindi fursa zinapopatikana. Kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi pia kutegemee ni kwa kiasi gani kinamama nao wanajitokeza kuomba nafasi hizo. Chama, na hasa UWT, mnalo jukumu kubwa la kuhamasisha wanawake kujitokeza.

Ndugu Mwenyekiti,
Sisi katika Chama cha Mapinduzi tuliwaahidi wanawake wa Tanzania, kupitia Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2005, kwamba tutaanza kwa kuongeza uwakilishi wa wanawake Bungeni, ili angalau tufikie asilimia 50-50.
Mchakato wa kuelekea huko umeanza na unaenda vizuri. Si shughuli rahisi sana ndiyo maana imechukua muda. Hata hivyo, tumedhamiria kutimiza ahadi yetu.
Tulikwishaamua kuelekea huko na hakuna kitakachoturudisha nyuma katika kuanza mpango huo. Mawazo ya msingi yatakapokamilika yatawekwa hadharani kwa wadau wote kutoa maoni yao. UWT inao mchango na wajibu mkubwa katika kufanikisha azma hii. Uongozi wenu na mawazo yenu yatakuwa muhimu katika kusaidia kupatikana kwa utaratibu mzuri utakaopanua na kuimarisha demokrasia nchini kwa haraka.

Ndugu Mwenyekiti,
La pili katika kuhakikisha maendeleo na ustawi wa mwanamke wa Tanzania ni kuhakikisha mwanamke hanyimwi haki zake. Kuna msemo kwamba “haki za mwanamke ni haki za binadamu”. Nami nakubali. Kwa maana hiyo, sisi katika Serikali tumeendelea na mchakato wa kuzitazama upya Sheria zihusuzo ndoa, mirathi na watoto, sheria ambazo zinahusu haki na ustawi wa wanawake wa nchi yetu. Kwa kuwa Sheria hizi zinagusa kwa karibu maisha ya jamii nzima, tumeamua tutengeneze White Paper ili wananchi washiriki kwenye mjadala wa mabadiliko ya Sheria hizi. White Paper hii italetwa kwenye Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa. Na tutaweka utaratibu wa wananchi kujadili mapendekezo hayo. Dhamira yetu ni kuzirekebisha sheria hizo ili wanawake wasizidi kukandamizwa na kunyimwa haki zao za msingi. Ni matarajio yangu kuwa UWT itashiriki kwa ukamilifu kama mdau kiongozi katika mijadala itayohusu Sheria hizi. Sauti yenu lazima isikike na uongozi wenu lazima uonekane kwenye jambo hili muhimu.
Jambo la tatu tulilolipa msisitizo katika ukombozi wa mwanamke wa Tanzania ni elimu ya mtoto wa kike. Kama wengi mjuavyo, tunalo tatizo kubwa katika baadhi ya jamii zetu juu ya kutotiliwa maanani au hata kupuuzwa kabisa haki ya mtoto wa kike kupata elimu. Kwa maana hiyo, kwa miaka mingi sasa idadi ya wanafunzi wa kike kwenye mashule yetu, na hasa idadi ya wanafunzi wa kike wanaomaliza elimu katika ngazi zote, imekuwa ndogo kuliko ya wavulana.
Tumejitahidi sana kwa miaka ya hivi karibuni kubadilisha hali hii kwa upande wa elimu ya msingi na sekondari. Siku hizi idadi ya watoto wa kike wanaoingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza, inalingana na wavulana. Lakini, bado kuna tatizo la watoto wa kike kutokumaliza shule kwa idadi inayolingana na wenzao wavulana. Jambo hili linarudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike wa Kitanzania. Tunaendelea kukabiliana nalo, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua madhubuti za kupunguza tatizo la mimba za wanafunzi.
Ni muhimu kwa UWT nayo kuwa mstari mbele na inaonekana iko mstari wa mbele katika harakati za kukabiliana na tatizo la watoto wa kike kutokumaliza masomo kwa sababu za kuolewa au kupata mimba na mambo mengine yanayofanya watoto wa kike wasimalize masomo.
Jambo la nne ambalo tumelipa uzito mkubwa na tutaendelea kulipa umuhimu mkubwa ni uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake. Kama nilivyosema hapo awali, Watanzania ni maskini lakini wanawake ni maskini zaidi. Kwa maana hiyo, wanahitaji kuwekewa mazingira maalum na mahsusi kwa ajili ya kujikwamua katika hali duni za maisha. Serikali inatambua kuwa wanawake ni wajasiriamali wazuri, waaminifu na ni watu wenye bidii kubwa. Wanachohitaji ni umoja, mtaji na elimu ya ujasiriamali na biashara.

Chanzo cha habari,
mawasilianoikulu.blogspot.com

Sofia Simba Atarajiwa Kutangazwa Mshindi


Wakati wowote asubuhi au mchana wa leo. Ni katika uchaguzi wa UWT Taifa. Hii ni kwa mujibu wa chanzo changu cha kuaminika ndani ya Chama Tawala,CCM.

Chagueni uongozi, si fedha

HAKIKA inashangaza jinsi ambavyo Taifa hili linazidi kudidimia katika mambo ya hovyo ambayo huko nyuma hayakupata si tu kutendwa bali kusikika.

Na inaelekea huu ni ugonjwa unaotukeketa katika kila pembe ya maisha yetu na mbaya zaidi, sasa umeingia hadi kwenye siasa, ambako tunaona kila aina ya kituko.

Ni kana kwamba watu hawa wameagana. Tuanze na Mbeya. Kabla na baada ya kutangazwa kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini tulikuwa tukishuhudia kila aina uchafu kwa maana ya maneno yanayosemwa na wanasiasa wetu.

Bado tunashuhudia uchafu huo wakati huu wa kampeni. Bado badala ya kutuambia nini watakachofanya cha kuufanya umma uvutiwe nao, wengi wa wagombea wanalalamika. Lakini umma hauhitaji malalako haya.

Unaweza kusema labda haya yanayotokea yamekuwa hivyo kwa kuwa huu wa Mbeya Vijijini ni ushindani wa vyama na kila chama kinajitahidi kurubuni wapiga kura, ndiyo maana ahadi nyingine zinazotangazwa ni kichekesho.

Lakini yanapotokea katika chama hichohicho, katika kundi la watu wanaotakiwa kuwa na imani moja na mwelekeo mmoja, inatia shaka.

Wiki hii ni wiki ya uchaguzi katika moja ya jumuiya za Chama cha Mapinduzi (CCM). Umoja wa Wanawake (UWT) unafanya uchaguzi, kumpata, pamoja na wengine, Mwenyekiti.

Tumesikia tambo zisizoisha kutoka kambi zote zinazowania nafasi ya Mwenyekiti. Tambo hizi, mara kadhaa, zimetoka nje ya utaratibu wa kawaida wa kujinadi katika uchaguzi, zikawa matusi na kashfa kubwa!

Kuna habari za matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi huu kiasi kwamba mtu atajiuliza, kama alivyopata kujiuliza Baba wa Taifa, Julius Nyerere; kama mtu alikopa fedha hizi atazirudishaje?

Sisi bado ni waumini wa uchaguzi unaomtafuta mtu mwenye uwezo wa uongozi, si mwenye uwezo wa kugawa fedha nyingi kuliko mpinzani wake. Ikitokea wote ni wagawa fedha, hiyo ni bahati mbaya sana! Pamoja na hayo tuwaombe wajumbe UWT wajitahidi kuchagua uongozi badala ya fedha.

John Bwire
Raia Mwema, Januari 7, 2009

Thursday, January 8, 2009

Wajumbe UWT wamfitinisha JK na Sophia Simba



WAKATI Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) ukitarajia kupata mwenyekiti wake mpya wiki hii, kumekuwapo na hujuma dhidi ya demokrasia itakayofanikisha mchakato wa kumpata mwenyekiti huyo, Raia Mwema imebaini.

Miongoni mwa mambo yaliyoibuka ni kutajwa kwa Rais Jakaya Kikwete kumuunga mkono mmoja wa wagombea wa naasi hiyo, Waziri wake wa Utawala Bora, Sophia Simba, madai ambayo yameshindwa kuthibitishwa na uongozi wa juu wa CCM uliopelekewa.

Pamoja na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sophia Simba ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, nafasi ambayo inatafsiriwa kuwa imetokana na kuwa kwake karibu na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Mbali ya kutajwa kwa Rais Kikwete ambaye ndiye atakayefungua rasmi mkutano wa UWT leo Jumatano, tuhuma za rushwa na kuchafuana kwa wagombea ni mambo yaliyotawala kampeni za kuelekea uchaguzi wa jumuiya hiyo yenye nguvu ndani ya chama tawala.

Baadhi ya wapambe wamefikia hatua ya kusambaza ujumbe wa maneno kupitia simu za mkononi za baadhi ya wajumbe wakitumia ugonjwa wa mmoja wa wagombea kama sababu ya kutaka asichaguliwe kushika nafasi hiyo ya uongozi wa UWT. Nafasi hiyo inawaniwa pia na wabunge wa Viti Maalumu Janet Bina Kahama na Joyce Masunga.

Wagombea kupitia wapambe wao inadaiwa wanahujumu mkondo wa demokrasia ya mmojawao kuchaguliwa kumrithi mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Abdallah.

Inadaiwa kuwa baadhi ya washiriki wa kampeni za wagombea hao walilazimika kusafiri na baadhi ya wajumbe kuelekea Dodoma katika kile kilichoelezwa kuwa kuwathibiti wasibadili mawazo ya kumchagua mgombea wa kundi wanalounga mkono.

Wajumbe waliojikuta wakisafiri na wapambe wa wagombea hao ni pamoja na wanaotoka katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Wajumbe wengine kutoka mikoa ya Kusini walijikuta wakizuiwa kwa muda jijini Dar es Salaam katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni “kuwekwa sawa.”

Baadhi ya wajumbe wamejikuta wakigharimiwa huduma za malazi jijini Dar es Salaam, kabla ya kuelekea mjini Dodoma kupiga kura.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wajumbe hao wamekuwa hodari katika kutoa ushirikiano ili kupewa rushwa na wapambe wa wagombea hao.

Habari kutoka mjini Dodoma zinaeleza kuwa wapambe wa baadhi ya wagombea waliwasili mjini hapo siku kadhaa, baadhi ya wagombea waliwasili mjini hapo siku kadhaa kwa ajili ya kuwapokea wajumbe wapiga kura.

Lakini wakati wapambe hao wakiwa wamewasili Dodoma kabla ya wajumbe kuwasili, washindani wao walilazimika kusafiri hadi katika mikoa wanakotoka wajumbe hao na kusafiri nao kuelekea Dodoma.

Kilele cha uchaguzi huo kinafikiwa wakati wagombea Sophia Simba na Mbunge wa Viti Maalumu, Janet Kahama wakiwa katika mvutano na mchuano mkali.

Kumekuwapo na malalamiko kutoka katika kila upande kuhusiana na kuchezeana ‘rafu’ na zaidi ni kambi mbili za Janet Kahama na ile ya Waziri Simba.

Janet Kahama kama ilivyo kwa Joyce Masunga ni wabunge wa Viti-Maalumu na ukweli ni kwamba mchakato wa kupata wabunge wa aina hiyo huhusisha ushindani ikiwa ni pamoja na kupigiwa kura na wajumbe maalumu katika mikoa wanakogombea.

Hata hivyo, madai kwamba Waziri Simba ametumwa na mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kugombea nafasi hiyo yamekwishakanushwa.

Madai hayo si mara ya kwanza kutajwa, yamewahi kujitokeza katika kinyang’anyiro cha viongozi wa juu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pia.

Mara kadhaa, Rais Kikwete mwenyewe amesikika akikanusha madai hayo. Lakini wakati Waziri Simba akiwa katika mazingira hayo, mgombea Janet Kahama naye anadaiwa kuungwa mkono na mwenyekiti anayemaliza muda wake, Anna Abdallah.

Haijafahamika ni kwa nini Anna Abdallah amuunge mkono mgombea huyo, lakini inawezekana ni imani yake kuwa mama huyo aliyepishana naye miaka mitatu kiumri (Anna akiwa mkubwa zaidi) ataweza kuongoza umoja huo kwa tija zaidi.

Lakini licha ya kuwapo kwa madai hayo, Anna Abdallah hakuwahi kusikika hadharani akiyapinga, lakini pia hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa anamuunga mkono Janet Kahama.

Wakati wagombea hao wakiwa na mazingira hayo, mgombea mwingine Joyce Masunga naye anatajwa kuwa na kigogo anayemuunga mkono.

Baadhi ya wajumbe wa UWT wanadai kuwa anaungwa mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Tofauti na wenzake hao wawili, Masunga amekuwa akiendesha kampeni za kimya kimya, na kwa wanasiasa wengine waliozoea mikikimiki ya kampeni wanadai kuwa mwenendo wa kampeni za mgombea huyo zinaweza kumwangusha.

Anna Abdallah anaondoka madarakani baada ya kuongoza UWT kwa miaka 14. Aliingia madarakani mwaka 1994, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sophia Kawawa, aliyefariki dunia.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, endapo mmojawapo kati ya Sophia au Kahama atashinda kiti hicho, uongozi wake huenda ukakabiliwa na changamoto nyingine ndani ya umoja huo.

Kuna uwezekano mkubwa changamoto hizo zikawa zinaibuliwa na kundi la mshindani atakayeshindwa ili hatimaye kuthibitisha kuwa ilikuwa ni makosa kwa mhusika kuchaguliwa kutokana na uwezo duni kiutendaji.

Hali hiyo inatabiriwa kwa kuwa wito wa kuvunja makundi ndani ya CCM umekuwa ukipuuzwa licha ya wito huo kutolewa na viongozi wa juu, akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Rais Kikwete.

Nafasi ya Uenyekiti wa UWT kama ilivyo kwa jumuiya nyingine za chama hicho, ina umuhimu wa pekee kutokana na anayeshika nafasi hiyo kuingia moja kwa moja katika vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.

Kuwa mjumbe wa Kamati Kuu CCM mwaka mmoja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kuna umuhimu mkubwa kisiasa, si tu kwa mjumbe husika bali pia kwa wanasiasa wengine wakiwamo wagombea wa nafasi za kisiasa katika dola ikiwamo Urais na Ubunge.

Ni kwa ajili hii wanasiasa wengi makini wametupa karata zao katika uchaguzi wa UWT kama walivyofanya katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) uliokuwa na makeke mengi na ule wa Jumuiya ya Wazazi, ambao umeshindwa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo makundi ndani ya chama hicho tawala.

Uchaguzi huo umetanguliwa na mkutano wa Baraza Kuu la UWT lililoketi Jumanne, wiki hii.

Miongoni mwa mambo yaliyopitiwa katika mkutano huo wa Baraza Kuu ni pamoja na kupitia ripoti ya utendaji ya umoja huo katika kipindi kilichopita.