Friday, May 29, 2009

Afrika Itaweza Kuwa na Serikali Moja?

Tangu bara la Afrika lipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni, viongozi wa afrika wamejaribu mara kadhaa kuunda serikali moja ambayo itasimamia mambo ya Afrika na kuifanya Afrika iwe na sauti katika anga za kimataifa lakini jambo hilo bado halijafanikiwa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba kazi yao ilikuwa ni kuleta Uhuru na Umoja, na wamefanikiwa kuleta uhuru, lakini umoja bado haujafanikiwa. Kazi ya kuiunganisha Afrika moja waliachiwa viongozi na wasomi wetu wa sasa. Katika siku za karibuni, viongozi na wasomi wa Afrika wamekuwa wakikutana na kujadili juu ya kuwa ana Afrika moja, lakini baadhi ya wasomi wanasema, Afrika kuwa na serikali moja ni ndoto za alinacha. Je, ni kweli kwamba Afrika haiwezi kuwa na serikali moja? Hapa chini kuna mahojiano na Dr. Benson Bana wa Chuo kikuu cha Dar es salam juu ya Umoja wa Afrika.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dk Bana:Afrika kuunda Serikali moja ni ndoto za Alinacha

Mhadhiri wa Chuo cha Fani na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Cass) Dk Benson Bana. Maswali na majibu ya mahojiano kati ya Mwananchi na Mhadhiri wa Chuo cha Fani na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Cass) Dk Benson Bana.

Unafikiria nchi za Afrika zinaweza kuunda serikali moja?

Kwa kweli ni ndoto za Ali Nacha kwa sasa kusema Bara la Afrika liwe na serikali ya pamoja. Hii ni kwa sababu tuna udhaifu wa aina nyingi ambao unatukwamisha na kutusuta katika azma ya kutaka kuungana na kuunda serikali moja.

Kwanza tujenge Asasi za Shirikisho la bara la Afrika na kuziimarisha, ikiwa ni pamoja na ushuru wa forodha, soko la pamoja kwa sababu Afrika hadi sasa bado ni 'heterogonous' kwa mfano Somalia ina matatizo yake, Misri ni Afrika lakini wanathamini zaidi Shirikisho la nchi za kiarabu, Comoro wanajifanya Wafaransa, Afrika ya Kusini wanajifanya wazungu.


Unafikiria ni kwa nini miungano mingi ya nchi za Afrika inavunjika?

Miungano hii inakufa kwa sababu waafrika wengi wanafikiria na kujali zaidi utaifa na 'vijikabila' vyao kuliko Jumuiya zao au miungano yao.

Pia ujenzi wa utaifa katika nchi nyingi za bara la Afrika bado unaendelea, ni Tanzania tu ambao tumefanikiwa lakini pia tuna muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao pia bado unatupelekesha kwa kutawaliwa na kero kuntu.

Mathalan wenzetu wakenya karibu kila kabila linataka kuwa na jeshi lake, Uganda kuna matatizo kibao ya kikabila, Burundi na Rwanda ndio usiseme kwa matatizo ya kikabila sasa utakuta yote haya yanatusuta kufanikisha azma ya kuunda serikali moja ya Shirikisho la Afrika.

Soma zaidi mahojiano haya kwa kubofya hapa.

3 comments:

Anonymous said...

You actually make it appear so easy with your presentation but I
find this topic to be actually one thing which I think
I might never understand. It seems too complicated and extremely large for me.

I am looking forward in your next post, I will try to get the
dangle of it!

Feel free to surf to my webpage manslaughter

Anonymous said...

Hello! I know this is kind of off topic but I
was wondering if you knew where I could get a captcha plugin
for my comment form? I'm using the same blog platform as yours and I'm having difficulty finding one?
Thanks a lot!

Here is my blog - role-play
Also see my page - sme-community.com

Anonymous said...

My brother suggested I might like this website. He was
totally right. This put up truly made my day. You cann't believe just how so much time I had spent for this info! Thanks!

Feel free to visit my homepage; nuptials