Friday, May 8, 2009
Minjingu haikubaliki au tunakimbia majukumu?
Wiki mbili zilizopita, kuliibuka mjadala bungeni kuhusu ubora wa mbolea ya Minjingu inayozalishwa na Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu kilichoko Babati mkoani Manyara, Kaskazini mwa Tanzania. Baadhi ya watunga sheria nchini, wakiwa katika mjadala wa Muswada wa Mbolea wa mwaka 2008, walidai mbolea hiyo haifai na wakaenda mbali zaidi kuitaka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, isiwapelekee pembejeo hiyo katika maeneo yao.
Miongoni mwao walikuwa ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi wa chama tawala, CCM na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo wa United Democratic Party (UDP).
Pamoja na mambo mengi katika mchango wake, Zambi alisema yafuatayo wakati akijadili muswada huo, “…mwaka huu kule Mbozi na mahali pengi, tumepelekewa mbolea ya Minjingu ambayo imewaharibia uzalishaji sana wananchi wa Wilaya ya Mbozi na inawezekana na mahali pengine.
“Wananchi wale wanasema mbolea hii kama haitarekebishwa, naomba niseme kwa niaba yao, nina hakika kwa sababu ni wengi wananiona na wananisikiliza, wamesema serikali isituletee mbolea hiyo.”
Mbunge huyo wa Mbozi Mashariki aliendelea na mchango wake bungeni Aprili 22, mwaka huu na kueleza, “Nalisema hili kwa sababu ndio ujumbe wao, naweza nikawa nawakwaza wengine, lakini naungana na wananchi wa Wilaya ya Mbozi na mimi nimeona mashamba ya wananchi yameharibika sana kwa wale wote waliotumia mbolea ya Minjingu.”
Kwa upande wake, Cheyo naye alikataa mbolea hiyo ya Minjingu na kueleza kwamba ni bora wananchi wa kwao (Usukumani) waachwe waendelee kutumia mbolea za samadi na mboji, akidai mbolea ya Minjingu inaharibu ardhi na mazao hayapatikani.
Soma zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment