Tuesday, May 26, 2009

"Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Changa la Macho"

Sheria ya maadili ya umma ilitungwa mwaka 1995 na bunge la Jamuhuri ya Tanzania kwa lengo la kuondoa migongano ya maslahi kwa watumishi wa umma wakati wanafanya maamuzi yao. Sheria hii ilitungwa kutokana na mambo matatu muhimu. Kwanza ilitokana na kuanguka kwa Azimio la Arusha lililokuwa likitekeleza sera za Ujamaa na kujitegemea. Azimio la Arusha lilikuwa na misingi ya maadili ya viongozi, kwahiyo baada ya kuanguka kwa Azimio hilo, ikabidi itafutwe njia mbadala. Pili, ni kutokana na mabadiliko kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi. Na tatu ni kuwepo kwa matukio mbali mbali katika kipindi hicho ya matumizi mabaya ya madaraka. Ndiyo maana hata Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha ‘Uongozi na hatima ya Tanzania’ alisema, “Ikulu imekuwa pango la walanguzi” akiwaonya viongozi wa umma kutotumia ofisi za umma kwa maslahi yao binafsi.

Soma zaidi mahojiano na Mwanasheria mwandamizi wa chama cha Wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) Tundu Lissu kuhusu mapungufu ya sheria hii kwa kubofya hapa.

No comments: