Wednesday, May 20, 2009

Salama: Jasiri Aliyetangaza Kuishi na Virusi vya UKIMWI

Maisha tunayoishi hapa duniani, yanahitaji uvumilivu, ujasiri pamoja na busara miongoni mwa jamii inayotuzunguka. Nashawishika kusema hayo baada ya kukutana na Salama Jumanne(Pichani), ambaye ana ujasiri wa kueleza kitu kinachomsibu pamoja na kupambana na misukosuko kwa jamii ambayo ilimcheka baada ya kuamua kujitangaza kuishi na Virusi vya Ukimwi (VVU). Nilipomwona mara ya kwanza, sikuamini kile alichokieleza kuwa anaishi na VVU, hali iliyonilazimu katika nafasi yangu ya uandishi wa habari, kuandika habari zake na kufuatilia kila tukio analokumbana nalo nami kuliandika ili watu mbalimbali waweze kumsaidia kutokana na matatizo anayokumbana nayo.

Nilihuzunika baada kunieleza historia ya maisha yake, pia nilijiuliza maswali mengi, je, ingekuwa mimi nakumbana na tatizo hili ningekaa kimya au ningewaeleza wenzangu? Je, marafiki, wazazi na jamii kwa ujumla wangelipokeaje tatizo langu ingawa mimi mwenyewe nimeshaamua kulitangaza ili nipate msaada? Binafsi sina uwezo mkubwa wa kumsaidia Salama lakini naamini watu mbalimbali pamoja na wahisani, wataguswa na habari hii na kumsaidia kwa kuwa licha ya kuwa anaishi na VVU, pia ana watoto watatu na mjukuu mmoja.

Salama ni mtu mwenye haiba, huwezi kuamini kuwa anaishi na VVU mpaka alipojitangaza kuwa na hali hiyo, umati uliokusanyika pale Mabibo katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Siku ya Maadhimisho ya Mwanamke Duniani, inayofanyika Machi 8 kila mwaka. Isome zaidi habari hii kwa kubofya hapa.

No comments: