Wateja wa Benki ya Standard Chartered wenye akaunti ya Diva Club ambayo ni kwa ajili ya wanawake, sasa watapata punguzo la bei za bidhaa au huduma katika maduka maalumu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Jeremy Awori alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe ya Siku ya Mama ambayo benki hiyo iliandaa kwa ajili ya wateja wake wa akaunti ya Diva.
Awori alitaja baadhi ya maduka ambayo wateja wanaweza kupata punguzo kuwa ni pamoja na Living Room, Game, Night Support na DT Dobie. Katika sherehe hizo zilizofanyika Hoteli ya Kempinski, Benki hiyo ilitoa zawadi kwa wanawake waliohudhuria katika sherehe hiyo kwa kutambua mchango wao katika kutunza fedha katika benki hiyo kupitia akaunti hiyo.
No comments:
Post a Comment