Monday, May 11, 2009

Ma-DC wapya Wanawake


Wakuu wa Wilaya wapya, sita wanawake kati ya 15 walioteuliwa na Rais hivi karibuni wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza semina elekezi mjini Morogoro, majina na Wilaya zao kwenye mabano , kutoka kulia ni Fatma Mwassa ( Mvomero), Queen Mlozi ( Ukerewe), Fatma Ally ( Nanyumbu), Mery Silla (Arumeru), Dk Rehema Nchimbi ( Newala) na Angelina Mabula ( Mulemba)., mafunzo hayo ya awali yalifanyika kuanzia Mei 5,hadi 8, mwaka huu.
Picha na mdau wa Morogoro John Nditi.

Idadi hii ya uwakilishi wa akina mama inatosha jamani?

2 comments:

Anonymous said...

Rais Kikwete kwa kweli anajitahidi sana kuwainua wanawake katika ngazi mbalimbali za uwakilishi serikalini ila bado hii haitoshi, wakuu wa mikoa wakina mama ni wachache.

Kapitu

Anonymous said...

kila la kheri katika kutetea wanyonge na kufanya kazi kwa uadilifu, wananchi wote wanawategemea nyinyi baada ya muda mrefu wa kupewa ahadi kemkem na viongozi waliotangulia. wanaharakati wote tunawategemea labda mtaleta jipya lolote.

mdau