Wednesday, May 13, 2009

Mengi, Rostam wamweka Kikwete njia panda

-Iddi Simba ampinga Rostam kuhusu NICO
KUNA maoni kuwa ombwe la uongozi ndilo ambalo linachangia katika malumbano, ambayo yameigawa nchi, kati ya wafanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambao kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa kuhujumu Taifa.

Baadhi ya wanazuoni, wanasiasa wastaafu na raia wa kawaida, wameiambia Raia Mwema wiki hii kwamba malumbano hayo hayawezi kuachwa yaendelee, na kwamba sasa lazima Serikali ionyeshe njia katika kuyamaliza kwa kuwatosa, japo wote wawili wanaelezwa kuwa watu wa karibu na Rais Jakaya Kikwete.

Mmoja wa wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amesema kinachojulikana kwa Watanzania wote ni kwamba hakuna Serikali ya Rostam Aziz au Reginald Mengi, na kwamba ukimya wa Serikali unaweza kuchochea wananchi kujichukulia sheria mikononi.

Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Profesa Mwesiga Baregu, ameiambia Raia Mwema kwamba Serikali ina wajibu wa kuchunguza tuhuma zinazorushwa kutoka kila upande na kwamba kilichofanywa na kila mmoja kati ya Mengi na Rostam ni kila mtu kutoa vidokezo tu na sasa Serikali ichukue hatua.

“Kama Serikali ikiendelea kukaa kimya italeta mguno miongoni mwa wananchi na hiyo ni hatari, wanaweza (wananchi) kuamua kuanza kujichukulia sheria mkononi,” alisema Profesa Baregu na kuongeza:

“Katika maelekezo yake au hatua itakazochukua, Serikali inapaswa kulinda haki za raia kwa mujibu wa sheria zilizopo lakini kwa maslahi ya Taifa.”

Soma zaidi

2 comments:

Anonymous said...

mi nadhani sisi sote tunatambua kwamba wale waliotajwa na Bw Mengi inawezekana wakawa wanahusika katika hili, ingwa yeye mwenyewe mengi alimtaja rais wa jamuhuri yupo mstari wa mbele lakini inavyoonekana si kweli kwani ingekuwa yupo mstari wa mbele asingeacha kuwachukulia hatua wale waliotajwa. Halafu Polisi Jamii niliwategemea wangechukua hatua katika sakata hili, au polisi jamii ipo kudhibiti wahalifu maskini pekee?

Anonymous said...

serikali inajua sana nani fisadi na nani siye, hata sisi tunafahamu. wananchi wataamka siku moja na kudai haki zao zilizochukuliwa na mafisadi, kila la kheri wanaharakati wote wapinga ufisadi!