Pale wilayani kuna ujanjaujanja unatumika kwa sababu mimi nina binti ambaye alikuwa anasoma shule ya sekondari Mwaneromango, nilimkamata mtuhumiwa kwa mkono wangu, nikampeleka Kisarawe, lakini mpaka leo tangu mwaka 2002 naambiwa upelelezi unaendelea, mtuhumiwa yuko uraiani na binti yangu alishajifungu
Taratibu zote muhimu alizotakiwa kufuata kufungua kesi alitimiza na sheria iko upande wake, lakini hadi leo hajapata haki. Juma Mwagala hasononeshwi na kitu kingine chochote zaidi isipokuwa umaskini wake anaona ndio chanzo cha kushindwa kwake kupata haki kortini dhidi ya kijana aliyempa mimba binti yake.
"Umaskini huu!" anapiga makofi na kunyanyua juu mikono yake kwa ishara ya kumuomba Mungu. Na pale anapogeuka nyuma na kumwona mtu akisogelea alipoketi, anajikusanya na kumkaribisha.
Kusoma makala nzima bofya hapa.
No comments:
Post a Comment