Wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu, Dar es salaam, wakiwa darasani wakifanya mitihani yao ya kila mwisho wa mwezi.
Katika hali kama hii ni aibu kwa wabunge wetu kudai nyongeza ya mishahara na marurupu. Huduma za jamii kama Elimu, afya, na miundombinu ikiendelea kudorora kila siku, huku gharama za maisha zikipanda kwa wananchi wa kawaida. Picha hii inawakilisha maelfu ya wanafunzi ambao wanakaa chini na wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati, walimu, vitabu, vyumba vya madarasa, chakula, madawa na nk. Je, upo umuhimu wowote kwa waheshimiwa wabunge kudai nyongeza ya mishahara katika kipindi hiki?
No comments:
Post a Comment