Friday, May 15, 2009

Wabunge Kuongezewa Mishahara; Hii Imekaaje Wadau?

Katika miezi ya hivi karibuni Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa katika malumbano makali baina yao, baadhi wakipinga hoja ya kutaka kuongezewa mishahara, marupurupu na posho, na wengine wakidai nyongeza hiyo. Kwa wananchi walio wengi katu hawawezi kukubaliana na hoja hii ya kuongezwa mishahara ya wabunge, ambayo kama mapendekezo hayo yakiridhiwa, wabunge wetu watalipwa jumla ya shilingi za kitanzania Milioni Kumi na mbili kwa mwezi. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa kwa hali yoyote ile. Katika Tanzania kama hii ya sasa ambayo Huduma za Afya zimedirora sana, Miundombinu ya barabara, maji, umeme, ni hafifu, Elimu inayodidimia kila ukicha, Ukosefu wa Ajira kwa vijana, Ukosefu wa Masoko kwa bidhaa za Wakulima, na changamoto nyingine kibao ambazo nchi yetu inazikabili sidhani kama wabunge wetu kuongezewa mishahara katika kipindi hiki ni busara na haki. Wanaharakati na waandishi wengi wamejaribu kutoa mawazo yao juu swala hili na kuonyesha wazi nia ya kupinga muswada huu kupitishwa,lakini wabunge wanaong'ang'ania muswada huu ni wengi na wamekuwa wakiongezewa nguvu na spika wa bunge, waziri mkuu na wabunge kadhaa wa chama Tawala.

Je, Wadau mna maoni gani juu ya mswada huu?

Kwa kusoma zaidi juu ya mjadala huu bofya katika linki hapa chini.

Sipendi tena sitaki wabunge wajiongezee mishahara

Pinda atetea wabunge

Dk. Slaa apita kipindi kigumu bungeni

No comments: