Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa TGNP Lilian Liundi aliwakaribisha warembo hao kwa mchezo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Usu Mallya akizungumza na warembo wanaowania taji la Miss Universe 2012 walipotembelea Mtandao wa Jinsia Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita. |
Warembo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TGNP |
Warembo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TGNP |
Warembo wanaowania taji la Miss Universe 2012 |
“Wasichana wanatumika vibaya, wanatendewa ukatili mkubwa, hakuna usawa katika mgawanyo wa rasilimali hasa malipo, suala kubwa ni kuhakikisha tunanufaika sawa katika rasilimali zetu kuanzia ngazi ya familia, hadi Taifa na kuunganisha nguvu ya pamoja’ amesema Mallya.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilaino TGNP, Lilian Liundi, amesema kuwa warembo na wasanii hata wanamitindo wanapaswa kujitambua kwa kujiwekea viwango vya malipo kwa kazi zao. Amesema kuwa watatakiwa kutambua fursa na hadhi yao na kudai kupatiwa malipo stahiki na yanayoendana na hali halisi ya maisha endeleu wanapohitaji kutengeneza matangazo ya kibiashara, sinema au kupanda majukwani. “Hili ni eneo muhimu sana, kuna tatizo kubwa la mfumo wa kinyonyaji unaoendelea wa kuwaumiza wasanii, warembo na wanamitindo, hii ni ajira, lazima iwe endelevu na imsadie muhusika.
Tunapozungumzia haki ya uchumi tunagusa moja kwa moja juhudi za mtu kujiendeleza kutokukwamishwa au kunyonywa na kundi lingine,”alisema Lilian na kuongeza: “Tujiwekee viwango, kabla ya kuwa na mikataba na makampuni, muweke viwango kuwa mnapoonekana kwenye jukwaa milipwe shingi ngazpi?” Liundi aliitaka kampuni inayoratibu mashindano hayo ya Compas Communication, kuangalia aina ya zawadi zinazotolewa kwa washindi hao kuwa za kuwasaidia zaidi badala ya fedha kidogo ambazo haziwasaidii kujiendeleza wala kufanya mradi wowote.
Warembo hao wamesema kuwa baadhi yao wanalipwa fedha kidogo kwani kwani mmoja wao aliyewania ‘Miss Dar’ ambapo ambao hawakushinda lakini waliingia 10 bora walilipwa shilingi 100,000. Liundi alisema kuwa ni lazima zawadi za warembo ziwe endelevu, ziwasaidie warembo kubadilisha maisha yao na sio lazima fedha kwani inaweza kuwa masaada wa kusoma ili mrembo apate ujuzi au maarifa.
Mkuu wa Chuo cha Jinsia, Dk. Diana Mwiru, aliwataka warembo hao kujikita katika utaalam zaidi ya urembo ili kujiandaa na maisha baada ya urembo na kuwa na soko la ajira zaidi. “Mnaweza kuwa wataalam wa masuala ya jinsia, uchumi, au kilimo, lakini ukawa mrembo, ukipata ajira katika utaalam huo unaenda na unapata fursa ya kutangaza taaluma yako, pia usikubali maisha yako yategemee kitu kimoja, maisha yanahitaji uelewa mpana wa masuala muhimu,”alisema Dk. Mwiru. Dk. Mwiru amewataka warembo hao kusoma Chuo cha GTI ili kubobea katika masuala ya Jinsia na maendeleo.
No comments:
Post a Comment