SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake
cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi
ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo
wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi
wakiwa watumishi wa umma.
Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job
Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru)
ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na
kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.
Zitto
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya
Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika
ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya
chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika
maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho
kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na
kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula
rushwa.
“Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama
kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa
Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua
zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.
Lissu ataja wengine
Kwa
upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge
wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini),
Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles
Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai
hayo.
Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.
Katika
orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu
alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini
huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo
kujinufaisha.
“Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito
wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na
kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na
Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama
hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea:
“Ila uchunguzi wetu
umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na
mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”
Lissu
alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema
wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.
Alisema
Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni
ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu
mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50.
“Nasir
Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa
namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi
kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema
na kuendelea;
"....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa
moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa
akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na
Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo.
Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na
kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”
“Hawa ndiyo
wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani
tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi.
Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana
taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”
Lissu alisema
kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za
umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995
na ni kinyume na maadili ya kibunge.
Katika hatua nyingine Lissu
amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za
Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema
nazo zina madudu mengi.
“Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya
Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe,
uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia
watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili
haki itendeke,” alisema.
Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi
ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri
kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke
kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge
yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”
“Katika hili
tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi
wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”
Majibu ya tuhuma
Alipotakiwa
kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta
lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi.
“Nimekuja
bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya
Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na
mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika
shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema).”
Kwa
upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya
Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya
kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo.
"Siyo
kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango
wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla.
Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10
kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema
Aliishauri kambi hiyo ya
upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu
ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza
kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.
Awali,
Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo
kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu
baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu.
Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki
vituo vya mafuta.
Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati
maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa
yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli
mtaujua, haraka ya nini?.
Mjadala Bungeni
Mjadala huo wa
wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni
jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru
Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali
Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili
kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria.
"Mheshimiwa Naibu
Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala
la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika
akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini
Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?” alihoji
Nassari na kuendelea:
“Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma
(POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati
zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia
kamati zenye mikataba.”
Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya
wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati
ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... “Tumeambiwa
Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge
gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe.”
“Mimi
naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge
tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,’ alisema
Kessy.
Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya
Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo
na baadaye apelekewe taarifa.
“Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo
humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili
suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi,” alisema.
Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui.
Alisema
Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike
uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba
ikibainika Bunge litawaanika hadharani.
“Kamati imerejea
kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya
jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe
kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale
itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,’’ alisema Ndugai.
Naibu
Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa
kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi
ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo.
Aliwatahadharisha
wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola
ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya
wabunge.
Tuesday, July 31, 2012
Monday, July 30, 2012
Maganzo: Mji wenye utajiri wa almasi usio na huduma ya maji
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Masagala nje kidogo ya Mji mdogo wa Maganzo akitoka kuchota maji bwawani bwawa hili lilichimbwa na mkandarasi huyo. |
Binti akichota maji katika moja ya mabwawa ambayo si salama kwa matumizi anuai bwawa hili lilichibwa na mkandarasi aliyekuwa akitengeneza barabara. |
Mabinti wakitoka kusaka maji kwa matumizi anuai. |
Na Joachim Mushi, Kishapu
KWA mtazamo wa kawaida ni kitendo cha
kawaida kwa mji wowote kuendelea kutokana na rasilimali zake zinaouzunguka mji
huo. Maeneo mengi nje ya nchi na hata Tanzania yamekuwa yakipata maendeleo ya
jamii na mazingira yake kutokana na rasilimali na shughuli za kijamii
zinazolizunguka eneo lenyewe.
Hali hii ni tofauti na ilivyo katika Mji
mdogo wa Maganzo uliopo wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga, ambao umefanikiwa
kuwa na rasilimali ghali yenye thamani kubwa ulimwenguni. Mji huu una madini ya
almasi yanayopatikana karibia sehemu kubwa ya eneo la Maganzo.
Kihistoria Mji wa Maganzo unachimbwa
madini ya almasi tangu kitambo kidogo. Wananchi wanachimba madini hayo katika
mashamba, viwanja na maeneo mengine ambayo yanaaminika kuwa na almasi. Huu ni
utajiri mkubwa ambao Mji mdogo wa Maganzo umefanikiwa kuwa nao.
Baadhi ya wananchi wamefanikiwa kunufaika
na utajiri huu. Nasema hivyo maana ukifika katika eneo hilo utashuhudia nyumba
za thamani na za kisasa na hata magari ya kifahari ambayo baadhi ya wakazi wa
eneo hilo wameyapata kutokana na almasi.
Mji huo unahuduma ya umeme, afya (japokuwa
kunachangamoto kadhaa), mawasiliano (mtandao wa simu) na pia umefanikiwa
kupitiwa na barabara kuu ya lami inayotoka Shinyanga mjini kuelekea Mkoa wa
Mwanza. Kwa kiasi fulani mji unavutia.
Wapo wawekezaji kadhaa wa madini akiwemo
Kampuni ya Williamson Diamonds ambayo licha ya kumiliki eneo kubwa la machimbo
ya almasi inamiliki maeneo mengine kadhaa ya ndani ya mji huo. Wachimbaji hawa
wanaendesha shughuli za uchimbaji madini eneo hilo.
Lakini pamoja na rasilimali hii ya Mji
Mdogo wa Maganzo hauna huduma ya maji safi na salama ya uhakika. Mji mzima
hauna maji ya bomba na badala yake hutegemea maji ya kuletwa kwa madumu kwa
baiskeli kutoka mjini Mwadui ambapo ni kilometa kadhaa kutoka katika mji huo.
Wachuuzi wa maji kwa kutumia baiskeli ndio
wanaotoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mji wa Maganzo. Wachuzi
hawa zaidi ya 100 ndio wanaotegemewa kuupatia mji huu maji kibiashara. Dumu
moja la maji huuzwa kati ya sh. 400 hadi 500 kulingana na umbali alipo
mwananchi anayeitaji maji hayo.
Benard Lucas ni mmoja wa wachuuzi (wauzaji
wa maji kwa kutumia baiskeli) Maganzo, anasema alianza kufanya biashara hiyo ya
uuzaji wa maji tangu mwaka 2009 baada ya kupata mtaji. Anasema uuzaji wa maji
eneo hilo unaitaji muhusika awe na baiskeli pamoja na madumu ya kubebea maji
pekee.
“Sehemu ambayo huyachota maji haya sisi
hatulipii...huyachota bure kazi yako ni kusafirisha kwa kutumia baiskeli na
kuwatafuta wateja walipo. Dumu moja la maji tunauza kati ya shilingi 400 na 500
kulingana na umbali anapopatikana mteja,” anasema Lucas.
Anasema kwa upande wake huuza madumu 14
hadi 16 kwa siku kulingana na uchakarikaji wa siku hiyo. Mwanambelembe Machia
ni muuzaji mwingine wa maji katika Mji mdogo wa Maganzo, anasema amekuwa
akifanya biashara hiyo kwa muda mrefu sasa na inalipa.
“Mimi nina watu wangu maalumu ambao
tumekubaliana kupeleka maji kiasi fulani kwa kila siku. Huwa napata wastani wa
shilingi 5,000 kwa siku kama kukiwa na biashara mbaya lakini kiasi hiki
kinanitosha kabisa kwa matumizi yangu,” anasema Machia.
Kwa upande wake Frank Simba mchuuzi wa
maji eneo hilo anasema alimaliza elimu ya msingi mwishoni mwa 2011, lakini
baada ya kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari alinunuliwa baiskeli na
wazazi wake na kuanza biashara hiyo ya uuzaji maji ili aweze kujitegemea.
Anasema msimu mbaya wa biashara hiyo ni
kipindi cha masika ambacho wananchi hutegemea maji ya mvua ili kukwepa gharama.
“Kutokana na wingi wetu kipindi hiki huwa kibaya kwa biashara maana wateja
huadimika kabisa,” anasema kijana huyu anaeomba shida ya maji isitoweke
Maganzo.
Hata hivyo Sera ya Maji ya nchi ya mwaka
2002 inaeleza kuwa madhumuni ya jumla ya sera kuhusu utoaji wa huduma ya maji
vijijini ni kuboresha afya ya jamii na kusaidia kuondoa umaskini vijijini ikiwa
ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa maji safi, salama na ya kutosha.
Madhumuni mahsusi ya sera hiyo ni
kuhakikisha upatikanaji wa huduma endelevu ya maji safi, salama na ya kutosha,
kwa gharama iliyo ndani ya uwezo wa wananchi vijijini. Pia kuweka bayana
majukumu na wajibu wa wadau mbalimbali. Lakini kama hiyo haitoshi sera pia
imesisitiza kuhusu wananchi kulipia sehemu ya gharama za ujenzi wa miradi, na
pia kulipia gharama zote za uendeshaji na matengenezo ya miradi yao, tofauti na
dhana iliyokuwepo ya kuchangia tu sehemu ya gharama za uendeshaji na matengenezo.
Hii haipingwi kuwa maji ni hitaji la
msingi na haki ya kila mtu. Na kwa kutambua kuwa upatikanaji wa maji safi na
salama ni hitaji la msingi na haki ya kila mtu, utoaji wa huduma ya maji
vijijini utaimarishwa. Hata hivyo haki kama hii haipo kwa wakazi wa Mji mdogo
wa Maganzo ambao unautajiri mkubwa wa almasi. Wakazi wa eneo hili kutokana na
shida ya maji wamekuwa wakitumia maji kutoka kwenye madimbwi kukwepa gharama za
kununua maji kila kukicha, huku wakihatarisha maisha yao kiafya.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Maganzo, Lwinzi Kidiga anakiri huduma ya maji ni kero kubwa kwa wakazi wa
vijiji vyote vinavyo zunguka eneo hilo. Anabainisha kuwa zipo juhudi ambazo
yeye na viongozi wenzake wanazifanya kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo.
Anasema kwa sasa tayari uongozi wa kijiji
umefanya mazungumzo na mwekezaji wa madini ya almasi eneo hilo, ambaye pia ni
mmiliki wa mgodi wa Williamson unaochimba almasi eneo hilo na mwekezaji huyo
amekubalia kuwaletea maji wananchi kwenye moja ya tanki kubwa ambalo lipo
jirani na soko kubwa eneo hilo. Anaongeza kuwa mradi huo unatarajia kuanza kati
ya mwezi Julai, 2012.
Lakini huenda miaka kadhaa ijayo kero hiyo
ya maji ikatoweka kwani, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Lucas Said akizungumzia kero hiyo anasema kwa sasa wataalamu wanafanya utafiti
katika vijiji kadhaa kuhakikisha vinapatiwa huduma ya maji pale mpango wa
kuleta maji kutoka Ziwa Victoria kwa matumizi eneo hilo utakapo kamilika.
Friday, July 27, 2012
Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka
MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja
katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo
familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi.
Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika.
Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu.
Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete.
Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi.
Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF)
Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mng’ong’o na Mwanakhamis Kassim Said.
Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu.
Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwang’onda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga.
Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM).
Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe.
Wananchi waja juu
Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni.
Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao.
“Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine,” alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa).
Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha.
“Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida,” aliongeza.
Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge.
Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake.
“Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi,” alisema.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo.

Wednesday, July 25, 2012
Sheria mpya mifuko ya jamii yazua mtafaruku nchini
Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya 2012 yaliyofanywa
na Bunge yamezua mtafaruku na sintofahamu, huku wafanyakazi wa sekta
mbalimbali wakiyapinga kwa maelezo kwamba ni kandamizi na yanalenga
kuwanyima haki ya fedha wanazokatwa kwa mujibu wa sheria kuchangia
mifuko hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicolaus Mgaya aliliambia gazeti hili jana kuwa, watafungua kesi katika Mahakama ya Kazi nchini, kupinga hatua ya Serikali kubadili Sheria ya muda wa lazima wa kuchukua mafao hayo ambao ni kati ya miaka 55 na 60.
Tangu juzi watu kutoka sehemu mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakipiga simu katika chumba cha habari cha Mwananchi kwa lengo la kupata ufafanuzi wa mabadiliko hayo ya sheria yaliyopitishwa na mkutano wa saba wa Bunge, Aprili 13 mwaka huu.
Kadhalika sheria hiyo inayozuia mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii kuchukua mafao kabla ya umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55, lilichukua nafasi kubwa katika mijadala ya mitandao ya kijamii ambako wengi wa wanaliochangia, wameiponda sheria hiyo na kuiita kuwa ni ya ‘kinyonyaji’.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka alisema jana kuwa: “Hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi, maana sheria hii itafuatiwa na kanuni na miogozo mingine ambayo ninaamini kwamba itaondoa wasiwasi uliopo”.
Isaka alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika miongozo hiyo ni iwapo mwanachama atafukuzwa au kuachishwa kazi, wanachama ambao wako kwenye kazi za mikataba na wale wanaopata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini.
“Kimsingi ni kwamba suala la mafao ya kuacha kazi kabla ya umri wa kisheria wa kustaafu limefutwa kwa mifuko yote, isipokuwa katika mazingira hayo niliyoyaeleza litawekewa miongozo, na hii ni kwa faida ya wachangiaji,”alisema Isaka.
Alisema baada ya sheria hiyo kuwa imepitishwa na Bunge, kisha kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi Juni mwaka huu, SSRA ilianza mchakato wa kuweka miongozo na baada ya hapo kinachofuatia ni kutoa elimu kwa umma na baadaye kuanza kutumika kwake rasmi.
“Lakini sasa tumelazimika kuanza kutekeleza sheria hiyo mapema kuliko tulivyopanga hasa baada ya kutokea kwa suala hili kwenye public (umma) kabla ya muda tuliokuwa tumekusudia,”alisema mkurugenzi huyo.
Isaka aliongeza kuwa chimbuko la sintofahamu iliyojitokeza ni baadhi ya mifuko kuchezeana rafu kwa lengo la kupata wanachama wapya kwenye migodi na kwamba wao kama wadhibiti tayari wametoa onyo kwa mifuko iliyohusika.
“Kwanza hakuna mfuko wowote ambao una mamlaka ya kutangaza kuanza kutumika kwa sheria, ni SSRA tu wenye mamlaka hayo, kwa hiyo tumewapa onyo, kama wanajitangaza wajitangaze kwa kueleza uzuri wa mfuko wao ni siyo kuchafuana au kuchafua wengine,” alisisitiza.
Wasemavyo wafanyakazi
Mgaya alisema sheria hiyo ni kandamizi kwani inamnyima fursa mfanyakazi aliyestaafu au kufukuzwa kazi kupata malipo yake ambayo ni halali.
“Sheria hii sisi hatuikubali na tunaipinga kwa nguvu zote na tutakwenda Mahakama ya Kazi kufungua kesi ya kupinga kutumika,” alisema Mgaya na kuongeza:
“Tutafanya mawasiliano na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuwaeleza kuhusu sheria hii ili watusaidie na ikishindikana azma yetu ni kwenda mahakamani.”
Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba haiwezekani mtu anafukuzwa kazi akiwa na miaka 45 na baadhi yao hawataki tena kuajiriwa wanataka kufanyabiashara halafu unamnyima mafao yake hadi afikishe miaka 55, kitu ambacho kitamfanya mtu huyo aishi maisha magumu.
“Sheria hiyo ingekuwa na usawa ingetumika kwa wafanyakazi wote wa Serikali na kutowabagua kama inavyojieleza kwamba, Mbunge akimaliza miaka yake mitano anachukua mafao yake. Sasa kwa nini iwe kwao tu na si kwetu pia?,” alihoji Mgaya.
Kwa upande wao Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (Tamico) Wilaya ya Geita, kimesema kitapeleka maombi maalumu kwa Rais Kikwete kupinga marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Katibu wa Tamico Wilaya ya Geita, Benjamin Dotto alisema wameamua kupiga kura ya maoni juu ya mabadiliko ya sheria hiyo, ili wanachama wao waamue wenyewe kama wanaitaka au la.
”Tunamwomba Rais aagize kupelekwa muswada wa marekebisho bungeni, kwa ajili ya kipengele ambacho kimeleta mtafaruku,” alisema Dotto.
Alisema kipengele cha kuzuia mfanyakazi kuchukua mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 55, kinakandamiza masilahi ya mfanyakazi mnyonge ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akichangia mapato ya nchi kupitia kodi anayokatwa.
Chimbuko la sheria
Mabadiliko ya sheria hizo za mifuko ya hifadhi ya jamii yalifanywa na Bunge Aprili 13 mwaka huu, baada ya muswada husika kuwa umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni Februari 1, 2012.
Ibara ya 107 ya muswada huo ndiyo ilipendekezwa kufutwa kwa Ibara za 37 na 44 za Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) ambavyo vilikuwa vikiruhusu mafao ya kujitoa.
Meneja uhusiano wa SSRA Sara Mssika alisema jana kuwa kufutwa kwa ibara hizo kulimaanisha kwamba hakuna mfuko wowote unaoruhusiwa kutoa tena mafao ya aina hiyo hadi hapo miongozo mipya itakapotolewa.
“Hakuna sheria ya mfuko mwingine iliyokuwa ikiruhusu mafao ya kujitoa, na kama wapo waliokuwa wakifanya hivyo, basi walikuwa wanafanya hivyo pengine kwa taratibu nyingine ambazo ni nje ya sheria za kuanzishwa kwa mifuko yao,”alisema Mssika.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni alisema lengo la marekebisho katika Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuiwezesha SSRA kufanya kazi yake kikamilifu na kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Alisema muswada huo uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, wakiwamo wafanyakazi, waajiri na Serikali, pia
mifuko yenyewe kupitia vikao vya wadau na Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi Jamii na Uchumi.
“Kimsingi, wadau wote waliunga mkono mapendekezo yaliyomo katika muswada huu,” alisema Kabaka na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yatawezesha kupanuliwa kwa wigo wa wanachama kwenye mfuko kwa kuruhusu wafanyakazi wanaoingia kwenye ajira kwa mara ya kwanza ama kujiajiri wenyewe ili waweze kujiunga.

Tuesday, July 24, 2012
Asilimia 30 ya watoto hufanyiwa ukatili nchini
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba amesema ripoti ya
utafiti wa ukatili dhidi ya watoto nchini, imeonyesha takribani wanawake
watatu kati ya 10 na mwanaume mmoja kati ya saba, walifanyiwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia na watu wazima walipokuwa watoto chini ya umri
wa miaka 18.
Alisema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na kukabiliana na tatizo hilo.
Aidha, Simba, alisema matokeo hayo yatasaidia katika kuanzisha taratibu za kuboresha huduma kwa waathirika wa ukatili na kuandaa miongozo na kanuni za utekelezaji wa Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009.
“Katika mwaka huu wa fedha wizara itasambaza kanuni na miongozo hiyo katika halmashauri zote nchini, ili wananchi waweze kuzielewa na kuzizingatia…pia itatayarisha mwongozo wa kukusanya takwimu za watoto wanaonyanyaswa,” alisema.
Simba alieleza hayo bungeni jana alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Wizara hiyo imeomba bajeti ya Sh. bilioni 15.6 ambapo kati ya hizo Sh. bilioni 12.1 ni matumizi ya kawaida.
Wakati huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemshambulia Waziri Simba, kwa kumhadaa, kumdanganya na kumteleza Nasra Mohamed ambaye alifariki dunia baada kufanyiwa unyama na mumewe.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Conjesta Rwamlaza, alitoa kauli hiyo alipokuwa akisoma maoni ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto kwa mwaka 2012/13.
“Waziri Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa alieleze Bunge hili ni kwanini alimhadaa, kumdanganya na kumtelekeza Nasra Mohamed bila msaada wowote wakati aliahidi kwa kinywa chake mwenyewe kuwa angemsaidia?” alisema na kuongeza:
“Kambi ya Upinzani inataka kujua Waziri anawasaidiaje watoto walioachwa na marehemu na pia hatua gani zitachukuliwa dhidi ya aliyetenda ukatili huu?”
Alisema wanasikitishwa kuona kwamba Serikali haiko mstari wa mbele katika kupigania haki kwa wanawake wanaonyanyaswa.
Rwamlaza alisema tukio hilo lilitokea Februari 19 mwaka huu, katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, ambako Nasra Mohamed, alifanyiwa unyama na mumewe Elisha Mkumbati ambaye alimgonga kwa makusudi na gari na baadaye kumburuza na gari hilo jambo lililomsababishia maumivu makali na hatimaye umauti.

CHANZO:
NIPASHE
Wednesday, July 18, 2012
Hoja Za Kambi Ya Upinzani Mambo Ya Ndani Yazuiwa Bungeni
HOTUBA
YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA VINCENT JOSEPHAT
NYERERE (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA
2012/2013 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Kwa
niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, napenda kuchukua fursa hii
kuwasilisha maoni yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya nchi kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Aidha, napenda
kuwashukuru askari wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza wanaoishi
Kambi iliyoko katika Kata ya Mkendo kwa kunichagua kuwa Diwani wao. Vile
vile, nawashukuru wananchi wote wa vyama vyote na dini zote Jimbo la
Musoma Mjini kwa kunichagua kuwa Mbunge na mtetezi wao. Pia napenda
kumshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa imani yake
kubwa kwangu kwa kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi katika Wizara hii.
Kwa upekee kabisa, Mheshimiwa Spika, kwa wanaoeneza propaganda kwamba
CHADEMA inachukia au kudharau askari polisi wetu, naomba nitoe shukrani
zangu kwa mke wangu Helen V. Nyerere ambaye pia ni askari wa Jeshi la
Polisi.
UTEKELEZAJI WA AHADI ZA SERIKALI
Mheshimiwa Spika,
Katika
mwaka uliopita wa fedha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilihoji
matukio mbali mbali ya mauaji ya raia yaliyowahusisha askari wa Jeshi la
Polisi pamoja na wa vyombo vingine vya dola. Aidha, tulihoji matukio
mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu za wananchi wetu hasa katika
maeneo yenye migodi mikubwa ya dhahabu kama vile Nyamongo, Arusha na
kwingineko katika nchi yetu. Vile vile, tulihoji sababu za Serikali
kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria na za kiutendaji watuhumiwa wa
makosa haya makubwa.
Mheshimiwa Spika,
Wakati
anatoa hoja yake ya kuahirisha Mkutano wa Bunge la Bajeti la mwaka
jana, Waziri Mkuu aliahidi kwamba Serikali ingefanya uchunguzi wa
matukio yote ya mauaji kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (The
Inquests Act), Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania. Kwa maneno yake
mwenyewe, Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema: “vifo ... ambavyo vimetokea
katika mazingira ya kutatanisha chini ya mikono ya Vyombo vya Dola, ni
lazima vichunguzwe.” Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, hadi wakati
tunaandika maoni haya, hakuna Mahakama ya Korona hata moja ambayo
imeitishwa kwa lengo la kuchunguza vifo vilivyotokana na matumizi ya
nguvu ya vyombo vya dola. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka
Serikali kutoa kauli rasmi mbele ya Bunge hili tukufu kama kauli ya
Waziri Mkuu ilitolewa kwa lengo la kuwahadaa Watanzania. Aidha, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itamke ni lini Serikali
itaunda Mahakama za Korona ili kuchunguza matukio yote ya mauaji ya
wananchi katika maeneo yote tuliyoyataja mwaka jana.
Mheshimiwa Spika,
Kwa
sababu ya Serikali kutotimiza ahadi yake ya kuchunguza matukio ya
mauaji kwa mujibu wa Sheria tajwa, vitendo vya mauaji na ukiukwaji wa
haki za binadamu vimeendelea kutokea katika nchi yetu. Kwa mfano, katika
taarifa yake ya Haki za Binadamu kwa Mwaka 2011, Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC) kinaripoti kwamba “mwenendo wa matukio ya
ukatili wa polisi na mauaji yanayofanywa kinyume cha sheria na vyombo
vya dola umeendelea kuongezeka katika nchi yetu. Kati ya Januari na
Desemba 2011 tayari watu 25 wamekwisharipotiwa kuuawa wakiwa mikononi
mwa polisi na maafisa wengine wa usalama, wakati ambapo watu wengine 50
walijeruhiwa.” Taarifa hii inaungwa mkono na taarifa ya Hali ya Haki za
Binadamu kuhusu Tanzania iliyotolewa mwaka huu na Wizara ya Mambo ya Nje
ya Marekani (State Department) inayoonyesha kuwa bado yapo mauaji
yanayotokea mikononi mwa vyombo vya dola ikiwemo jeshi la polisi,
utesaji na wananchi wanaotuhumiwa kujikuta wakipata vipigo kinyume na
mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.
MAUAJI YENYE SURA YA KISIASA
Mheshimiwa Spika,
Kutokana
na Serikali kutochukua hatua kukabiliana na matukio ya mauaji
yanayohusishwa na vyombo vya dola, sasa limezuka wimbi la mauaji na
matukio ya majaribio ya mauji yenye sura ya kisiasa katika maeneo
mbalimbali nchini. Matukio hayo ni pamoja na mauji ya kada wa CHADEMA
Mbwana Masudi yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika
Jimbo la Igunga, na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River,
Marehemu Msafiri Mbwambo, mara baada ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika
Jimbo la Arumeru Mashariki.
Aidha,
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na majaribio ya mauaji ambapo wabunge wa
CHADEMA Mheshimiwa Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela na Mheshimiwa
Salvatory Machemli wa Jimbo la Ukerewe, walioshambuliwa kwa mapanga
mbele ya maafisa polisi na watu wanaosadikiwa kutumwa na makada wa CCM
mkoani Mwanza. Vile vile, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa
Iringa Mjini (CHADEMA) alivamiwa na wafuasi wa CCM wanaodaiwa kutumwa na
Iddi Chonanga, Diwani wa Kata ya Nduli (CCM) katika Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa.
Mheshimiwa Spika,
Matukio
ya mauaji au majaribio ya mauaji yenye sura ya kisiasa yamewahusu pia
watu ambao sio wanachama au viongozi wa vyama vya siasa lakini
wanaonekana kupinga matakwa ya watawala. Haya yamemkuta Mwenyekiti wa
Jumuia ya Madaktari Dr. Steven Ulimboka ambaye alitekwa nyara na kuteswa
kwa kikatili na watu ambao taarifa za vyombo vya habari zimewataja kuwa
maafisa wa vyombo vya dola. Kwa mara nyingine tena, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inaitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iamuru
kukamatwa kwa watuhumiwa wote ambao wametajwa kuhusika na utekaji nyara
na jaribio la kumuua Dr. Ulimboka ili kufuta dhana kwamba vyombo vya
dola viko juu ya sheria na vinaweza kuua au kutesa wananchi bila mkono
mrefu wa sheria kuwaangukia.
Mheshimiwa Spika,
Tarehe
14 Julai 2012, mtu anayesemekana kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa
CCM katika Kata Ndago, Jimbo la Iramba Magharibi, Yohana Mpinga, ambaye
pia ni mtoto wa Mwenyekiti wa CHADEMA katika Kata ya Urughu alifariki
dunia kufuatia vurugu zilizotokea baada ya kumalizika kwa mkutano wa
hadhara uliohutubiwa na viongozi wa CHADEMA katika Kata ya Ndago. Kwa
vile, tayari baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali ndani ya Bunge
hili tukufu wanaelekea kuwa wameshapitisha hukumu kwamba CHADEMA
inahusika na kifo cha Marehemu Yohana Mpinga, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni ina haya ya kueleza kuhusiana na tukio hili.
Kwanza,
mkutano wa hadhara wa CHADEMA ulihudhuriwa pia na maafisa polisi
waliokuwepo wakati wote wa mkutano huo. Pili, licha ya kuwepo kwa
maafisa polisi hao, kundi la wahuni wanaodaiwa kukodiwa na makada wa CCM
wa Jimbo la Iramba Magharibi walivuruga mkutano huo kwa kupiga mawe
watu waliohudhuria mara mbili lakini mara zote polisi waliokuwepo
hawakuchukua hatua zozote dhidi ya kundi hilo la wahuni. Aidha, mara ya
wahuni hao kuvuruga mkutano mara ya pili, viongozi wa CHADEMA walitoa
taarifa rasmi katika Kituo cha Polisi cha Ndago na kufunguliwa jalada
namba NDG/RB/190/2012.
Tatu,
mara baada ya kutoa taarifa hiyo kwa polisi, mkutano wa hadhara
uliendelea bila fujo yoyote hadi ulipomalizika na msafara wa viongozi wa
CHADEMA kuondoka eneo la Ndago na kuelekea Kinampanda ambako kulikuwa
na mkutano mwingine wa hadhara. Wakati huo, kundi la askari polisi wa
Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) kutoka Kiomboi walishafika katika eneo la
mkutano na kukuta mkutano umemalizika. Nne, kwa vile mkutano wa hadhara
wa CHADEMA ulimalizika kwa amani mbali na matukio ya kihuni
yaliyoripotiwa kwa Jeshi la Polisi, na kwa vile kulikuwa na kikosi cha
FFU na askari polisi wengine katika eneo la mkutano baada ya msafara wa
CHADEMA kuondoka, ni wazi kwamba watu wanaotakiwa kutoa maelezo ya jinsi
Marehemu Yohana Mpinga alivyofikwa na mauti ni Jeshi la Polisi lenyewe.
Aidha,
Mheshimiwa Spika, ni Jeshi la Polisi pekee linaloweza kuwaeleza
Watanzania kwa nini kikundi cha wahuni waliowarushia mawe viongozi wa
CHADEMA na wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara hawakuchukuliwa
hatua zozote na polisi waliokuwepo kwa muda wote wa mkutano huo au
askari wa FFU waliofika baada ya msafara wa CHADEMA kuondoka. Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa sana na mauaji ya kijana huyo na
inatuma salamu za pole na rambi rambi kwa familia, ndugu na jamaa wa
marehemu. Hata hivyo, Kambi yetu inasikitishwa na kushangazwa sana na
ushabiki wa kisiasa ambao umejitokeza humu Bungeni na kauli za kutoa
hukumu ambazo zimetolewa na baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali
bila hata kusubiri uchunguzi kamili juu ya jambo hili.
MASLAHI YA POLISI NA MAGEREZA
Mheshimiwa Spika,
Katika
maoni yake ya mwaka jana Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ililalamikia
utamaduni wa Serikali kupuuza maslahi ya askari polisi na wale wa Jeshi
la Magereza. Utamaduni huu ni wa muda mrefu sana. Kwa mfano, katika
hotuba ya bajeti ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha
2006/2007, aliyekuwa Waziri wakati huo alikiri kwamba “... kutokana na
kipato kidogo cha askari polisi, inawawia vigumu kukopa katika mabenki
nchini kutokana na riba kuwa kubwa na kukosa dhamana za uhakika. Hivyo,
askari polisi hawana mahali popote wanapoweza kupata fedha za
kujiendeleza kiuchumi. Aidha, mishahara na posho wanayolipwa askari bado
haikidhi hali halisi ya mahitaji yao na familia zao.”
Mheshimiwa Spika,
Toka
wakati huo hadi sasa, maslahi ya askari polisi yamekuwa mabaya zaidi
kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumuko wa bei hasa za
vyakula kupanda wakati ambapo mishahara yao haijaongezeka sambamba na
ongezeko la gharama halisi za maisha. Aidha, katika hali inayoonyesha
kutokujali kabisa maslahi na hali za maisha za askari wetu, Serikali
imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyotolewa tarehe 17 Novemba, 2011 na
aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Khamis Sued
Kagasheki, aliyeliambia Bunge hili tukufu kwamba “... posho ya askari
imepandishwa na ... kwamba (inatakiwa) itoke kwenye shilingi laki moja
mpaka shilingi laki moja na hamsini.... Ni jambo ambalo tunalo na
tumelifanyia kazi na tuna uhakika kwamba, litaweza kutimia….”
Mheshimiwa Spika,
Ni
ukweli usio na mjadala kwamba askari polisi na magereza bado wanapokea
posho ya kujikimu ya shilingi laki moja badala ya shilingi laki moja na
elfu hamsini iliyoahidiwa na Serikali mbele ya Bunge hili tukufu. Aidha,
katika mazingira ya kushangaza kabisa, mara baada ya Serikali kutoa
ahadi Bungeni juu ya posho hiyo, uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi
ulituma maelekezo kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kufanya uchunguzi ili
kubaini askari wote waliokuwa wanadai walipwe posho ya shilingi laki
moja na nusu kama ilivyoahidiwa ili askari hao wafukuzwe kazi.
Mheshimiwa Spika,
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali ilieleze Bunge lako tukufu
ni lini italipa malimbikizo ya baki ya shilingi elfu hamsini kwa mwezi
kwa kila askari polisi na magereza ambayo haijawalipa askari hao hadi
hivi sasa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali
ianze kuwalipa askari polisi na magereza posho ya kujikimu ya shilingi
laki moja na nusu kwa mwezi kuanzia mwaka huu wa fedha, kwa vile ahadi
ya Serikali iliyotolewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
haijawahi kukanushwa, kubatilishwa au kubadilishwa na Serikali.
Mheshimiwa Spika,
Sio
tu kwamba Serikali haitekelezi ahadi inazotoa Bungeni juu ya malipo ya
askari polisi na magereza. Serikali pia imekuwa inawakopa watumishi hao
bila ridhaa yao. Kwa mfano, randama ya fungu la 29 inaonyesha kuwa Jeshi
la magereza linadaiwa jumla ya shilingi bilioni 23.65. Kati ya fedha
hizo, watumishi wa Jeshi la Magereza wanaidai Serikali jumla ya shilingi
bilioni10.34 ambazo ni malipo ya stahili zao mbali mbali kama vile
fedha za likizo, uhamisho, mafunzo, n.k. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili kama, na lini, italipa
madeni haya ya askari magereza wetu wanaokesha magerezani usiku na
kushinda juani mchana wakiwalinda wafungwa na mahabusu waliojaa katika
magereza ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika,
Kuna
hatari kwa askari wa Jeshi la Magereza kufanya kazi katika mazingira
magumu ambayo tumeyaeleza katika maoni haya. Mfano ni katika Jimbo langu
la Musoma Mjini. Mbali na makazi duni ya askari magereza, vile vile
kuna umbali mrefu kati ya kambi ya askari magereza ya Nyasho na Gereza
la Mkoa lililopo Kata ya Mkendo na askari magereza wamekuwa wakitembea
kwa miguu usiku wanapokuwa zamu gerezani. Hii inahatarisha usalama wao
kwani wanaweza kuvamiwa na kudhuriwa na wafungwa au mahabusu waliokwisha
kumaliza adhabu zao lakini wakawa na visasi na askari hao. Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iwapatie gari askari wa kambi ya
Nyasho na makazi mengine ya askari magereza yaliyoko mbali na magereza
wanakofanyia kazi ili kunusuru maisha ya askari magereza wetu.
Mheshimiwa Spika,
Katika
maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya mwaka jana, tulipendekeza
kwamba “... utaratibu wa sasa wa polisi wa ngazi za chini kukatwa
shilingi 5,000 kila mwezi kwenye mishahara yao, kwa ajili kugharamia
mazishi yao na wategemezi wao, ufutwe mara moja, kwani unawanyonya kwa
sababu vipato vyao ni vidogo. Badala yake ... serikali ibebe jukumu
hilo.” Hata hivyo, hadi tunaandika maoni haya, Serikali imeendelea
kupuuza mapendekezo haya kwa kisingizio kwamba ‘mfuko wa kufa na
kuzikana’ ni wa hiari ilhali askari polisi wanaendelea kukatwa mishahara
yao kwa lazima. Kwa mara nyingine tena Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
inatamka kwamba kukata mshahara wa mfanyakazi bila ridhaa yake wakati
hadaiwi chochote na mwajiri wake ni kinyume cha sheria husika za nchi
yetu na kitendo cha jeshi la Polisi kuendelea kukata mishahara ya askari
polisi kwa ajili ya ‘mfuko wa kufa na kuzikana’ bila ridhaa ya askari
polisi wenyewe kikome mara moja.
Mheshimiwa Spika,
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inafahamu kwamba askari polisi wanaofanya
kazi za lindo katika mabenki yote ya biashara hapa nchini hulipwa posho
ya shilingi elfu kumi kwa siku. Hata hivyo, Serikali haijawahi kutamka
hadharani kiasi ambacho mabenki hayo hulipa serikalini kwa ajili ya kazi
hiyo ya kulinda mabenki binafsi. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inaitaka Serikli kulieleza Bunge lako tukufu kiasi
ambacho mabenki ya biashara hulipa serikalini kwa ajili ya huduma ya
ulinzi inayotolewa na askari polisi ili Bunge lako lifahamu kama askari
polisi wanaofanya kazi hiyo wanalipwa inavyostahili.
VITENDEA KAZI VYA POLISI
Mheshimiwa Spika,
Kwa
mujibu wa ripoti ya Hali ya Uchumi wa Taifa, makosa ya jinai
yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini yalikuwa
62,133. Ripoti inasema kwamba kwa mwaka 2011 makosa 63,703 ya jinai
yaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini. Kwa kiasi kikubwa, ongezeko
hili la uhalifu linasababishwa na askari wa doria kushindwa kufika
kwenye maeneo ya matukio ya uhalifu kwa haraka pindi wapatapo taarifa
kwa kisingizio cha kukosa mafuta kwa ajili ya magari ya doria.
Hata
hivyo, Mheshimiwa Spika, nyaraka za Serikali zinaonyesha kwamba Bunge
lako tukufu limekuwa likiidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya mafuta ya
magari ya Jeshi la Polisi. Kwa mfano, kwa mujibu wa randama ya Fungu la
28 kwa mwaka huu wa fedha, matumizi halisi ya mafuta kwa ajili ya Jeshi
la Polisi kwa mwaka wa fedha 2010/2011 yalikuwa shilingi bilioni 2.81.
Aidha, katika mwaka wa fedha uliopita Bunge lako tukufu liliidhinisha
shilingi bilioni 2.61 kwa ajili ya mafuta, wakati ambapo kwa mwaka huu
wa fedha Serikali inaomba Bunge liidhinishe shilingi bilioni 2.56 kwa
ajili ya mafuta ya magari ya Jeshi la Polisi.
Wakati
Bunge limekuwa lkiidhinisha mafungu haya makubwa ya fedha kwa ajili ya
mafuta, askari polisi wamekuwa wakilalamika kwamba hawapewi fedha za
mafuta kwa ajili ya magari ya doria hivyo kusababisha askari polisi
kushindwa kufanya kazi zao hizo ipasavyo. Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inaitaka Serikali ieleze zinakopelekwa fedha za mafuta kwa ajili
ya Jeshi la Polisi kama gari moja la doria linapatiwa lita 5 za mafuta
kwa kutwa na/au usiku.
IDARA YA UHAMIAJI NA PAKACHA LA MIPAKA
Mheshimiwa Spika,
Mipaka
yetu na nchi jirani zinazotuzunguka imekuwa pakacha linalovuja. Ndio
maana katika hotuba yetu ya mwaka jana tuliliambia Bunge lako tukufu
kwamba “... kumekuwa na ongezeko la wageni wengi kutoka nchi za nje ...
kiasi cha kujiuliza kama nchi hii ina utaratibu wowote wa kuratibu na
kudhibiti uingiaji wa wageni hapa nchini.” Tulionyesha jinsi ambavyo
kumekuwa na ongezeko la wageni haramu kutoka nchi za Somalia, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Pakistan,
Nigeria, China, India na Bangladesh “ambao wanaishi Tanzania kwa mfumo
usio rasmi, bila ya kuwa na hati zinazowaruhusu kufanya hivyo.”
Tulitahadharisha kwamba “utaratibu wa kuachia kila mgeni kuingia
Tanzania na kuishi atakavyo bila ya vyombo husika kujua kuwepo kwake ni
hatari kiusalama, hasa katika zama hizi za kusambaa kwa ... ugaidi na
uharamia wa kimataifa katika masuala ya fedha, biashara za binadamu ...”
n.k.
Mheshimiwa Spika,
Maneno
na tahadhari zetu ziliangukia kwenye masikio ya Serikali kiziwi. Na
sasa yale tuliyoyasema yameanza kutimia kwani ni mwezi mmoja tu umepita
tangu wahamiaji haramu zaidi ya arobaini kutoka Ethiopia kukutwa
wamekufa ndani ya lori la mizigo ambalo kwa vyovyote vile lilitokea nchi
jirani. Watu hawa waliingiaje nchini na kusafiri hadi katikati ya nchi
yetu bila kujulikana na maafisa wa Uhamiaji, polisi wa usalama
barabarani na usalama wa taifa kama kweli nchi yetu iko salama? Ni afisa
gani wa Idara ya Uhamiaji aliyewapitisha katika mpaka wetu wa Namanga
au Horohoro au Sirari au Kogaja au Borogonja? Na ni askari polisi gani
aliyewasindikiza hadi Kongwa? Aidha, ni afisa mizani gani wa TanRoads
aliyepitisha lori walimokuwa watu hao bila kulikagua na kujua
kilichokuwamo?
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni ilitegemea – kwa kuzingatia ukubwa na uzito
wa kashfa hii – viongozi waadilifu katika Wizara, Idara ya Uhamiaji na
Jeshi la Polisi wangewajibika kutokana na uchafu huu. Hata hivyo, hakuna
hata mmoja ambaye amefanya hivyo. Kwa vile uwajibikaji wa hiari
unaelekea kushindikana, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamtaka Rais
Kikwete kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuwawajibisha wale wote
waliohusika kuanzia viongozi wa Wizara walioko humu Bungeni na uongozi
wa juu wa Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi ili kuondokana na aibu
hii ya nchi yetu kuwa transit route ya biashara ya kusafirisha binadamu
katika sehemu hii ya Bara la Afrika.
Mheshimiwa Spika,
Matatizo
ya ongezeko la wahamiaji haramu katika nchi yetu linatokana na Idara ya
Uhamiaji kuendekeza vitendo vya kifisadi katika kuajiri, kupandisha
madaraja au vyeo wa maafisa wa Idara hiyo. Kwa mujibu wa taarifa tulizo
nazo, ajira katika Idara ya Uhamiaji haizingatii tena elimu, uwezo na
weledi wa maafisa husika. Bali, kwa mujibu Taarifa ya Utafiti wa Mpango
Mkakati wa Mageuzi Katika Utumishi wa Uhamiaji (Immigration Service
Reform Programme Strategic Plan Research Report) iliyochapishwa na
Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 27 Novemba, 2011, “mara nyingi mgawanyo
ya kazi (katika Idara) hautegemei sifa bali unategemea upendeleo,
rushwa, kujuana na urafiki vitu ambavyo viko kinyume na maana halisi ya
mgawanyo wa kazi.” (“Most of the time placement is not based on merits
but depends on nepotism, bribery and technical know-who, friendship and
favouritism that have been contrary to the whole meaning of placement.”)
Mheshimiwa Spika,
Ushahidi
wa kauli hii unapatikana katika Taarifa hiyo ya Utafiti inayoonyesha
kwamba maafisa wengi wa ngazi za juu katika Idara ya Uhamiaji ni watu
wenye uwezo mdogo kielimu kulinganisha na maafisa wa ngazi za chini wa
Idara hiyo. Kwa mfano, katika ngazi ya Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji
kwenda juu hadi kwa Kamishna Mkuu, kuna maafisa kumi wenye shahada ya
uzamili (masters degree), wawili wenye post-graduate diploma (PGD),
ishirini na nne wenye shahada ya kwanza, tisa wenye stashahada, saba
wenye diploma, kumi na moja wenye kidato cha sita na 248 wenye elimu ya
kidato cha nne. Katika maafisa hawa wa ngazi za juu, kuna Kamishna mmoja
mwenye elimu ya kidato cha nne wakati kuna Makaimu Kamishna 216 wenye
elimu hiyo ya kidato cha nne na Kamishna Wasaidizi Wakuu 31.
Kwa
upande mwingine, Mheshimiwa Spika, kuanzia ngazi ya Mrakibu Mwandamizi
(Senior Superintendent) kwenda chini mpaka koplo kuna maafisa wenye
shahada ya uzamili 36, wenye post-graduate diploma wako saba, wenye
shahada ya kwanza wako 340, wenye stashahada wako 78, diploma wako kumi
wenye cheti (certificate) wako 52, waliomaliza kidato cha sita wako 585
wakati waliohitimu kidato cha nne wako 337. Katika mazingira ambayo
maafisa wenye uwezo mkubwa wa elimu hawapewi nafasi za juu katika Idara
badala yake uongozi wa juu umejazwa na wenye elimu za mashaka kama
inavyoonyeshwa katika Taarifa ya Utafiti ya Wizara, ni wazi kwamba
matukio kama ya maafa ya wahamiaji waliokutwa wamekufa Jimboni kwa Naibu
Spika wa Bunge hili tukufu hayawezi kuepukika!
Aidha,
Mheshimiwa Spika, katika mazingira ya upendeleo na rushwa katika ajira
ya Idara ya Uhamiaji ya aina hii, maafisa uhamiaji hawawezi kuacha
kutumiwa na wanasiasa wa chama tawala kuwatuhumu washindani wao kisiasa
kuwa sio raia wa Tanzania ili kuwaondoa katika kinyang’anyiro cha
chaguzi zetu. Hivi ndivyo ilivyotokea kwa Mheshimiwa Ali Mohamed Keissy
alipotaka kugombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA na kuzushiwa tuhuma kuwa
siyo raia. Hata hivyo, alipojiunga na CCM bila ridhaa yake tuhuma za
kutokuwa raia ziliyeyuka na sasa ni Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi
Kaskazini katika Mkoa anakotokea Waziri Mkuu!
Mheshimiwa Spika,
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa kauli rasmi mbele ya
Bunge hili tukufu juu ya mambo haya ambayo yamethibitishwa na Ripoti ya
Utafiti ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Aidha, Kambi inaitaka Serikali itoe
kauli kama kuna haja yoyote ya kutumia mamilioni ya fedha za wananchi
kusomesha maafisa wa Idara ya Uhamiaji ambao baada ya kufuzu hawapatiwi
vyeo na majukumu yanayolingana na uwezo wao wa kielimu.
JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI
Mheshimiwa Spika,
Ni
dhahiri kuwa umuhimu wa Jeshi hili unaonekana pale yanapotokea majanga
ya moto, mafuriko au maafa mengine kama vile tetemeko la ardhi ambapo
athari za matukio haya ni makubwa sana na mara nyingi hupelekea wananchi
kupoteza maisha. Malalamiko ya wananchi katika maeneo mbalimbali juu ya
Jeshi la Zimamoto kuchelewa kufika katika maeneo ya tukio yamekuwepo
kwa miaka mingi na yamepigiwa kelele sana hapa Bungeni. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inarudia ushauri wake kuwa Serikali iboreshe mfumo
mzima wa zimamoto katika nchi yetu ili kukabiliana na majanga ya moto
yanayoongezeka kutokana na kupanuka na kukua kwa miji yetu.
Mheshimiwa Spika,
Baada ya maelezo na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ninaomba kuwasilisha.
.....................……………………………………..
VINCENT JOSEPHAT NYERERE
MSEMAJI MKUU WA
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
17/07/2012
Thursday, July 12, 2012
Nusu ya Bajeti ya Ardhi kujenga Kigamboni mpya
Na Florence Majani, Dodoma
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga zaidi ya nusu ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha, 2012/2013 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza mji huo ni Sh60 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 59 ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo, ambayo ni Sh101.731 bilioni.
Hata hivyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema Bungeni jana kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ni sawa na asilimia 10 tu ya mahitaji ya kiasi cha Sh605.
“Kwa hiyo tutatumia mbinu za kisasa kutafuta pesa nyingine Sh605 bilioni nje ya Bajeti kutekeleza mradi huu bila kuchelewa zaidi. Mradi huu unahitaji kiasi hicho cha fedha kwa miaka mitatu ya kwanza,” alisema Profesa Tibaijuka alipokuwa akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake jana na kuongeza:
“Nitasimamia mradi huu kwa kasi, ari na nguvu mpya. Ingawa pia sitakuwa nimetenda haki iwapo sitawashukuru wananchi wa Kigamboni kwa uvumilivu na ushirikiano wanaotuonyesha.”
Katika Bajeti ya wizara hiyo ya Sh101.7 bilioni, matumizi ya kawaida ni Sh30.7 bilioni na Sh71 bilioni ni za maendeleo. Katika fedha hizo za maendeleo, Sh61 bilioni ni fedha za ndani na Sh10 bilioni ni fedha za nje.
Kuhusu wananchi wanaoishi katika eneo hilo, Profesa Tibaijuka alisema hakuna mkazi yeyote wa Kigamboni atakayehamishwa kwani idadi ya wananchi waliopo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya makazi mapya yanayotakiwa kujengwa katika eneo hilo.
Alisema ni ushauri wake kwamba wakazi wote wa Kigamboni wachague kubaki katika mji huo kwani wawekezaji wa ndani na nje watapewa maeneo kwa ajili ya kujenga makazi ambayo yatatumika kuwahamishia wananchi watakaoamua kubaki.
“Tunashauri wote wabaki kwa kuwa sasa hivi kuna wananchi takribani 82,000 wakati tunajenga mji mpya wenye uwezo wa wakazi 400,000. Hakuna sababu ya wananchi kuhama eneo hili ila makazi yao yatapangwa upya na kuboreshwa,” alisema.
Gharama za mradi
Profesa Tibaijuka alisema ujenzi wa Mji wa Kigamboni utafanywa kwa awamu tatu, ambazo zitatekelezwa kati ya mwaka huu na 2032 na gharama zinazotarajiwa kutumika hadi utakapokamilika ni Sh11.6 trilioni.
Alisema awamu ya kwanza itakuwa kati ya mwaka 2012 na 2022, awamu ya pili kati ya 2022 na 2027 na awamu ya tatu ni kati ya 2027 na 2032.
Profesa Tibaijuka alisema miongoni mwa kazi zitakazofanywa katika mwaka huu wa fedha ni kuundwa kwa wakala mpya wa kusimamia mradi huo anayejulikana kama Kigamboni Development Agency (KDA).
Kazi nyingine ni kuidhinisha mpango na kuanza utekelezaji, kufanya uthamini wa mali zilizomo katika maeneo ya miundombinu, huduma za maji na eneo mbadala na kulipa fidia kwa mali zilizomo katika maeneo yaliyofanyiwa uthamini.
Kuhusu fidia, Waziri Tibaijuka alisema wananchi ambao hawajakiuka maagizo ya mradi kwa kufanya maendelezo haramu, wasiwe na wasiwasi kuhusu fidia kwa sababu mradi utazingatia haki na ni endelevu... “Fidia itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa tathmini ya kiujumla ambayo itakokotolewa kutokana na viwango vya soko na kuhusishwa ili iwe sahihi.”
Alisema atafanya ziara ya mafunzo kwa wawakilishi kutoka Kigamboni kutembelea mji mpya ili uwepo uelewa wa pamoja juu ya jinsi mji huo utakavyokuwa.
Hazina ya Ardhi
Katika hatua nyingine, Profesa Tibaijuka alisema wizara yake inakamilisha uanzishaji wa Hazina ya Ardhi pamoja na Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Alisema vyombo hivyo vitasimamia utoaji wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na nje kwa misingi ya kuingia ubia wa kumiliki pamoja hisa zitakazotolewa kwa uwiano kati ya wananchi na wawekezaji husika.
Kuhusu kuweka na kutunza alama za mipaka ya Tanzania na nchi jirani, Profesa Tibaijuka alisema majadiliano ya kupima maeneo hayo yalishakamilika.
Alisema majadiliano yalishafanyika baina ya Tanzania na nchi za Comoro na Msumbiji na mkataba wa kwanza kati ya Tanzania, Msumbiji na Comoro kwenye alama za utatu baharini inayotenganisha nchi hizo ulikamilika na kutiwa saini Desemba 5, mwaka jana.
“Mkataba wa pili kati ya Tanzania, Shelisheli na Comoro ulitiwa saini Februari 17, mwaka huu. Hivyo basi, Tanzania imekamilisha upimaji wa mipaka katika Bahari ya Hindi na itatangaza eneo lake la ukanda wa kiuchumi baharini bila kipingamizi kwa nchi jirani,” alisema.
Alisema wizara yake imewasilisha andiko la kudai nyongeza ya eneo ya ukanda wa kiuchumi baharini Januari, mwaka huu na Tume ya Mipaka ya Baharini ya Umoja wa Mataifa, inapitia andiko hilo.
Profesa Tibaijuka alisema kupatikana kwa eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 61,000 kutaiwezesha Tanzania kuvuna rasilimali za chini ya bahari kwa manufaa ya sasa na kwa vizazi vijavyo.
Kurasini kulipwa fidia
Kuhusu mradi wa uendelezaji wa eneo la Kurasini ulioanza 2006 kwa ajili ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka alisema wizara imetenga fedha chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo katika eneo la Kurasini na Shimo la Udongo.
“Wizara itaendelea na malipo hayo kwani hata mwaka jana tulilipa kiasi cha Sh550 milioni kwa wakazi wa Mtaa wa Kurasini waliopo jirani na Mabwawa ya Majitaka,” alisema.
Alisema wizara yake itaendelea kutatua migogoro ya ardhi, urasimishaji wa makazi holela, mikopo ya nyumba, ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ujenzi wa nyumba za biashara na makazi.

‘Katiba mpya itoe miaka 10 tu kwa wabunge, wawakilishi’
Na Masoud Sanani, Zanzibar
BAADHI ya wakazi wa Zanzibar wametaka Katiba Mpya iweke kipindi cha ubunge na uwakilishi kiwe miaka 10 kama ilivyo kwa Rais ili kuimarisha demokrasia nchini.Wakitoa maoni kwenye Mkutano wa kusaka maoni ulioandaliwa na Tume ya Katiba mjini hapa walisema lazima wabunge wawe na miaka 10 kama ilivyo kwa Rais badala ya kutaka wawe wabunge milele.
Abdallah Khamis Abdallah (54) na Bakar Mwinyi Mussa (63) wa Mitakawani walitaka wabunge wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wawe na muda maalumu wa uongozi wa miaka 10 kama ilivyo kwa Urais.
Abdallah pia alitaka Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na vyeo vingine vya juu wakistaafu wawe kama wananchi wa kawaida wasienziwe kama ilivyo sasa kwani ni gharama kubwa kwa uchumi wa Taifa.
“Rais ana pensheni kubwa na marupurupu mengi kwa hiyo alipwe akawe kama mwananchi wa kawaida asiendelee kutunzwa ma Serikali,” alitoa maoni yake kwa Tume inayochukua maoni juu ya kuandikwa kwa Katiba Mpya.Alitaka pia rasilimali za Taifa ziwe za Muungano na zimilikiwe na dola.
Katika hatua nyingine wakazi wengi waliotoa maoni yao juu ya kuandikwa Katiba Mpya nchini walitaka mfumo wa sasa uendelee, lakini Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Rais wa Muungano.
Wakitoa maoni yao katika maeneo ya Mgeni Haji, Mitakawani na Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja jana walipendekeza mfumo wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar uendelee.
Lakini wananchi hao walitaka Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Rais wa Muungano badala ya kuwa waziri katika Muungano kama ilivyo sasa.Pia wananchi hao walitaka kero zote za Muungano ziondolewe ili Muungano uimarike na misaada kutoka nje igawiwe kwa pande zote mbili za Muungano yaani Bara na Zanzibar.
Awali mkazi Zanzibar, alishauri Katiba Mpya iwe na kipengere kitakachowatoa Ikulu Marais wanaomaliza muda wao na kutaka kugombea awamu nyingine ili wanapogombea wawe wanatoka nyumbani kwao badala ya kutoka Ikulu.
Akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Katiba iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Pandu Ibada (40) mkazi wa Mpapa, Wilaya ya Kati alieleza kuwa Rais anapaswa kutoka Ikulu wakati wa uchaguzi.
Alitaka Katiba Mpya itoe nafasi ya kuwapo kwa Rais wa muda ambaye baada ya uchaguzi atamkabidhi madaraka aliyeshinda katika uchaguzi mkuu.
“Rais akiwa wa Muungano au wa Zanzibar asitoke Ikulu na kwenda kwenye viwanja vya kampeni kuwania urais, aondoke Ikulu ili awe sawa na wagombea wengine,” alieleza mwananchi huyo .

Baraza La Habari La Kiislamu Kuwafungulia Kesi Mahakamani Madaktari Waliogoma
Baraza
la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) limesema linakusudia
kuwafungulia mashitaka Madaktari Mabingwa wote pamoja na Madaktari
waliokuwepo kwenye Mafunzo kwa Vitendo (Interns) ambao walishiriki
katika mgomo kwenye hospitali mbalimbali nchini na kusababisha wagonjwa
kukosa huduma za matibabu huku wengine wakipoteza maisha yao.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya baraza hilo kukaa na Madaktari waliokua katika
mgomo na kukubaliana kuwa waiombe radhi Serikali pamoja na wananchi
kisha warudi kazini, lakini Madaktari hao wamekiuka makubaliano hayo na
kuendelea na mgomo jambo lililoonyesha kwamba hawakuwa tayari kupata
suluhu.
Katibu
wa BAHAKITA, Said Mwaipopo amesema wameshauriana na Wanasheria wao na
kuamua kuwafungulia kesi ya mauaji Madaktari hao katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai 2012.
Amesema,
“kwa tukio zima jinsi lilivyokwenda, limeonyesha kwamba Madaktari
hawataki wala hawana shida tena ya kurudi kazini kwa sababu ni wazi
kwamba kuna mtu yuko nyuma yao wanaemtumikia. Sisi kama Watanzania,
sehemu ya jamii tumekaa na Wataalamu wetu wa Sheria tumekubaliana kwamba
Jumatatu tunakwenda kufungua kesi Mahakamani kwa Madaktari wote
waliogoma wakati wamesomeshwa na kodi zetu na Serikali yetu
imewasomesha, tutawafungulia kesi ya kusababisha mauaji pale Muhimbili,
kwa hiyo tunachofanya hivi sasa ni kwenda pale Muhimbili kwa mganga mkuu
kuchukua orodha ya watu waliopoteza maisha.”
“Sisi
tuliingilia kati mgomo huu kwa nia njema ya kutapata suluhu kati ya
madaktari na serikali…lakini baada ya taarifa zetu kutoka kwenye vyombo
vya habari Ikulu ilitoa tamko la kukataa kukutana na sisi... ...lakini
Ikulu walieleza vizuri kwamba hawajawahi kukataa kukutana na viongozi wa
madaktari kwa maana hiyo basi serikali imeonekana dhahiri kutaka
suluhu. Baada ya taarifa hizo sisi tuliwatafuta viongozi wa MAT ambao
tuliwaeleza kwamba kutokana na taarifa hizo wao waombe msamaha kwa
serikali na umma wa watanzania kwa kuendesha mgomo ambao umesababisha
vifo. Lakini baada ya kuwaeleza hivyo hawa viongozi wa MAT
hawakukubali…sisi kama viongozi ambao lengo letu ilikuwa kutafuta suluhu
tukaona hawa vijana (madaktari) wana nia mbaya. Lakini sisi si kujitoa
tu bali tutawafungulia mashtaka ya mauaji wote walioshiriki katika mgomo
huo. Tutafanya hivyo ili fundisho kwa wengine ambao wana nia kama za
madaktari wanaoendesha migomo.
Kwa
hiyo sisi tunaunga mkono kufikishwa mahakamani kwa Rais wao ni njia
sahihi kabisa ya kurudisha nidhamu, lakini pia tunaunga mkono matamko
yote yaliyotolewa na serikali dhidi ya madaktari,”alisema Mwaipopo.
Akijibu
hoja hizo, Katibu wa MAT, Dkt. Edwin Chitage amesema hawaogopi
kufikishwa mahakamani na kwamba wao waliwapokea viongozi hao kwa nia
njema wakiamini ni viongozi wa dini.
“Kama
wamesema watatufikishwa mahakamani wao waende halafu tutakutana
nao…sisi tuliwapokea kwa nia njema kabisa kwa sababu walituomba
wenyewe..lakini baada ya kikao cha Jumamosi siku ya Jumapili wakatupigia
simu kuomba tukutane nao,sisi tulikutana nao lakini cha kushangaza
walitueleza kwamba wamepigiwa simu na mtu wa Ikulu akiwataka kutuambia
kwamba inabidi tuandike barua ya kuomba msamaha halafu tuwape wao ili
waipeleke…sisi tulishangaa jambo hili… sisi hatutafanyi kazi hiyo,”
alisema Dkt.Chitage.
Chanzo: http://www.wavuti.com
Wednesday, July 11, 2012
MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni
BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote
waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana
na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo
iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza
sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi
kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka
madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya
Msajili wa Madaktari.
“Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”
“Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”
Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.
Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.
Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... “Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu.”
Kiongozi wa madaktari kortini
Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.
Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.
Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.
Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.
Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.
Afya ya Dk Ulimboka
Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: “Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu.”
Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.
Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.
UN yanena
Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.
Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.
Mgomo wamalizika
Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.
Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang’oro

SEMINA: Je,Ukatili wa Kijinsia ni Suala la Kikatiba?
SEMINA ZA JINSIA
NA MAENDELEO
UNAKARIBISHWA KATIKA MFULULIZO WA SEMINA ZA JINSIA NA
MAENDELEO (GDSS) KILA JUMATANO, AMBAPO WIKI HII KIWOHEDE WATAWASILISHA
MADA: Je,Ukatili wa Kijinsia ni Suala la
Kikatiba?
Lini: Jumatano Tarehe 11/7/2012
Muda: Saa 09:00 Alasiri – 11:00 Jioni
MAHALI: Viwanja
vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo
Sokoni
WOTE
MNAKARIBISHWA
Subscribe to:
Posts (Atom)