Uchambuzi na Maoni ya Wasomaji kwa Machapisho ya: Hali Halisi Ya Kijinsia Tanzania na Tathmini ya Miaka 10 Baada Ya Beijing.
Mjadala huu ulifanyika Jumatano ya tarehe 10/08/08 na uliongozwa na dada Anna Kikwa na uliweza kuibua mambo kadha ya
kufuatilia katika kila eneo ambalo wanasemina walijadiliana. Mjadala uligawanyika katika maeneo makuu matano ambayo ni: Afya na Afya ya Uzazi, Hali ya Kiuchumi, Elimu, Haki na Usawa wa Jinsi na nafasi ya Mtoto wa kike katika vyombo vya habari, uongozi(Maamuzi) na familia, na mwisho Hali ya Utamaduni na Mila.
Wanasemina Walikaa katika makundi matano na kujadiliana juu ya maeneo hayo na kutoa michango mbalimbali ambayo inahitaji ufuatiliaji wa pamoja na wanaharakati wote. Hapa chini nimeanza na baadhi ya michango ya wanasemina katika sekta ya afya, ili kutoa nafasi ya kupata maoni kutoka kwa wadau.
1. Sekta ya Afya
Katika sekta hii wanasemina walijadili kwa ujumla hali ya utoaji wa huduma ya afya katika hospitali za serikali lakini mkazo mkubwa uliwekwa katika afya ya uzazi. Mapaungufu yalionekana katika utekelezaji wa sera ya afya ya uzazi ambayo inampa ruhusa mama mzazi kupata huduma bure kitu ambacho hakitekelezwi. Pili, swala la rushwa limeota mizizi na kuonekana kana kwamba haliwezi kudhibitiwa. Rushwa imesemekana ndio chanzo cha vifo vingi vya akina mama wajazito, hasa wale ambao hawana kipato na waishio maeno ya vijijini. Tatu, Swala la kutoa huduma kwa wagonjwa wa UKIMWI ambalo serikali limelirudisha kwa wananchi, washiriki waliona hatua hii ni kuwaongezea mzigo mkubwa wananchi ambao tayari wamezongwa na umasikini wa kutupa, na ikizingatiwa mzigo huu wa ulezi wa wagonjwa majumbani mara nyingi wanaoachiwa ni akina mama, hivyo ni sawa na kusema swala hili nalo ni nyongeza ya mzigo kwa akina mama.
Washiriki wa semina waliazimia walichukue swala hili la afya ya uzazi na kulifanyia
kazi mpaka hali itakapobadilika na kuboreka. Mbinu kadhaa zimeafikiwa zitumike, ikiwa ni pamoja na; kupiga picha(hata za simu) katika wodi za wazazi na kuzipeleka katika vyombo vya habari, kuandika makala katika magazeti (walau kila wiki makala moja), kushiriki katika vipindi vya runinga na redio(nafasi hiyo ipo ni kuifuatilia tu)
Je mwanaharakati utashiriki vipi katika kampeni hii ya kuleta mabadailiko katika sekta ya afya nhini Tanzania? Au ni upi mchango wako katika kampeni hii ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya hapa Tanzania?
2 comments:
Kweli kuna haja kubwa ya kuhahkikisha huduma ya afya kwa akina mama inarekebishwa ili kupunguza vifyo vya akina mama wanapojjifungua, wanaharakati wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika hili.
Mambo mengi yameshaongelewa bado kufanyia kazi, Je wanaharakati wamejipanga vya kutosha katika swala hili, kwa kuwa wao wenyewe wamejiwekea muda maalumu kuleta mabadaliko, basi tusubiri jambo hilo kutokea. Mimi nawaunga mkono wanaharakati katika hili. Harakati njema.
da,sekta ya AFYA kama mtoto ambaye hana future hapa TANZANIA! NAISHANGAA Serikali inadai kwenye sera yake kwamba kila mgonjwa wa kansa itamtibia bure,leo hii kina mama,watoo,vijana na wanaume wengi wana zidi kuteketea na kansa huku sera ikiwa imegharamiwa mamailioni ya fedha za semina kutatyarishwa.
by, Hashim LUANDA,GDSS.
Post a Comment