Tuesday, September 16, 2008

Mfululizo wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS)

Uchambuzi na Maoni ya Wasomaji kwa Machapisho ya: Hali Halisi Ya Kijinsia Tanzania na Tathmini ya Miaka 10 Baada Ya Beijing.

Hali ya Uchumi

Wanasemina waliona mfumo wa kiuchumi unaoendelea ni wa kibabe na unoendeleza unyonyaji wa rasilimali kutoka kwa wananchi walio wengi na maskini na kuwanufaisha watu wachache matajiri na umesababisha wananchi wengi maskini kukosa huduma za msingi za kijamii. Washiriki waliweza kuonyesha mapungufu katika hali ya uchumi wa Tanzania kwa katika vipengele ambavyo wanahisi vinachangia kudorora kwa uchumi wa nchi, maeneo hayo ni pamoja na;

1. Ukosefu mkubwa wa ajira- wananchi wengi hawana ajira za kueleweka kitu ambacho kinasababisha wengi wao kuishi katika hali duni ya kimaisha. Vijana na wanawake wengi hawana ajira hivyo hufanya kazi ambazo zina kipato kidogo kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

2. Ukosefu wa fursa sawa kwa wote. Mfumo wa kiuchumi bado unalea watu wachache kuendelea kujineemesha kiuchumi na ukiacha kundi kubwa katika hali mbaya ya kiuchumi. Watu wachache wenye nafasi nzuri wanawapeleka watoto wao katika shule nzuri, na baadae wanapata nafasi nzuri za kazi katika mashirika mbalimbali hivyo kuendelea kujipatia utajiri zaidi. Pia nafasi na kazi mbalimbali za umma zinatolewa kwa ambao wana nafasi nzuri ya kifedha au wale wanaoweza kuhonga kidogo kwa ajili ya nafasi au kazi hizo.

3. Sekta isiyo rasmi haijapewa kipaumbele katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini. Sekta hii ambayo inachukua asilimia kubwa ya wananchi lakini bado haijapewa kipaumbele, na serikali imekuwa ikiwanyanyasa watu ambao wamekuwa wakijiari wenyewe kwa mfano, wafanyabiashara ndogo ndogo kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyaswa na askari wa jijini Dar es Salaam mara kwa mara.

Wadau mnasamaje kuhusiana na haali ya uchumi nchini Tanzania? Je serikali imefanya vya kutosha katika kuinua uchumi wa nchi?

1 comment:

Anonymous said...

Hapa serikali yetu imechemka, mimi sijaona juhudi yoyote ya kuendeleza uchumi wetu kama wanasiasa wanavyosema. Hata hivyo wananchi wanapaswa kutumia haki yao ya kupiga kura kuchagua uongozi safi kwa ajili yamaendelao ya yao na ya vizazi vyao.