Friday, September 26, 2008

Shindano la Insha

Dhidi ya Kutumikisha na Kunyanyasa Watoto Kingono

Washiriki: Wanafunzi wote wa Shule za Sekondari na Msingi
nchini Tanzania, wenye umri chini ya maika 18.

Changia maoni yako kuhusu: Nini kifanyike ili watoto waepukane na vitendo vya unyanyasaji na utumikishaji kingono?

Insha yako izingatie: Kutoa suluhisho, mawazo yenye ubunifu na ambayo yanatekelezeka. Insha ifafanue jukumu la viongozi na kila mwanajamii wakiwemo Watoto wenyewe, Wazazi, Walimu, Viongozi wa Dini, Mtaa/Kijiji, Kata, Diwani, Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mkoa na Serikali kuu katika kupambana na hatimaye kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto kama ubakaji, mimba na ndoa za utotoni, kulazimishwa ngono na kupewa fedha au kutumia watoto kufanya biashara ya ukahaba. Kila Insha iliyochapishwa au kuandikwa kwa kalamu, isizidi maneno elfu moja (1,000).
Zawadi:
· Mshindi wa 1 - Tsh. 300,000/-
· Mshindi wa 2 - Tsh. 200,000/-
· Mshindi wa 3 - Tsh.100,000/-
· Washindi 10 bora (Tsh. 50,000/-) kila mmoja

Lugha: Kiswahili au Kiingereza.
Andika: Jina lako, Umri, Jinsi, Jina la Shule na Mkoa.

Insha kumi bora zitachapishwa kwenye kitabu kinachoandaliwa kwa ushirikiano na Vyama vya Wanahabari vya Kenya (AMWIK), Ethiopia (EMWA), Uganda (UMWA) na Tanzania (TAMWA). Kitabu hicho kitasambazwa kwenye shule mbalimbali ili kuwaelimisha watoto juu ya vitendo vya unyanyasaji na utumikishaji kingono na kuwawezesha kushiriki katika kampeni mbalimbali za kupinga vitendo hivyo. Washindi watatangazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini, wiki tatu baada ya kufunga shindano hilo.

Mwisho wa kupokea Insha: Ijumaa, Oktoba 24, 2008.
Tuma Insha yako kwa: Shindano CSAE, SLP 8981, Dar es Salaam
au barua pepe; tamwa@tamwa.org au admin@tamwa.org.
Simu: 0777-002002 au 022-2772681

Au fika:
Ofisi za TAMWA
Sinza-Mori, Block 47
Angalizo: Insha itakayoandikwa na watu walio na umri zaidi ya miaka 18

No comments: