Mapendekezo ya Wanaharakati Kuhusu Mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971
Semina ya tarehe 17th Septemba, mada ilikuwa ni Mapendekezo ya wanaharakati katika sheria ya ndoa, iliyowakilishwa na wawakilishi kutoka kituo cha haki za binadamu. Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ina vipengele yenye mapungufu ambavyo wanaharakati wamekuwa wakiyapigia kelele vipengele hivyo vifanyiwe marekebisho kwa sababu vipengele hivyo vinawanyima haki za msingi watoto wa kike za kulitumika Taifa. Sheia hiyo inatoa uhalali wa ndoa za umri mdogo kwani inaruhusu watoto wadogo kuolewa waakiwa na umri wa miaka 14 (kwa ridhaa ya wazazi) au miaka 15 kwa amri ya mahakama. Pamoja na juhudi nyingi za wanaharakati bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho na inaendelea kutumika na kuwakandamiza watoto wa kike. Wanaharakati wanaipinga sheria hiyo ya ndoa kwa sababu inamadhara yafuatayo:
• Kutokana na maumbile yao madogo mabinti wanaolewa wakiwa na umri mdogo wanaweza kupata fistula wakati wanapojifungua au kufa au watoto kuafariki au vyote.
• Binti hanakuwa hayupo tayri kisaikolojia, mabinti wanaolewa wakiwa wadogo sana wanakuwa hawapo tayari kuishi katika maisha ya ndoa, hivyo kusababisha matatizo makubwa ya kisaikolojia kwa wasichana wanaoolewa katika umri mdogo.
• Husababishia maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo wanaoolewa. Kwa watoto kuolewa katka umri mdogo kunawasababishia wawepo katika hatari ya kupata maambukizi kwa sababu wanakuwa hawana maamuzi katika tendo la ndoa na kushindwa kujitetea ama kujikinga na maambukizi, pia maungo yao madogo yanawafanya wawepo katika hatari kubwa ya mambukizi.
• Mfumo wa elimu unamtaka katika umri huo binti awe shuleni, hivyo sheria hii inakinzana na sheria nyingine za nchi ambazo zinamtaka kila mtoto awepo shuleni katika umri kama huo wa mika 14 na 15.
• Sheria hii inaendeleza ukatili wa kijinsia, kwa sababu inachangia watoto wa kike kuendelea kunyanyaswa kwa kunyimwa haki yao ya msingi ya kuweza kuchagua aina ya maisha wanayotaka kuishi.
Je wadau mnasemaje kuhusiana na sheria hii ya ndoa? Je Serikali imefanya vya kutosha kuibadilisha sheria hii ya ndoa? Je wanaharakati wanaweza kufanya nini ili kuweza kuleta mabadiliko ya sheria hii?
No comments:
Post a Comment