Monday, September 1, 2008

Michango iliyojitokeza Katika Uzinduzi wa kitabu cha Hali Halisi ya Jinsia Tanzania

Mchangiaji kaka Hashim S Luanda (Pichani) alichangia juu ya Ubora wa Elimu Tanzania na hasa juu ya hizi shule mpya za Kata zilizoanzishwa hivi karibuni na serikali. Mchangiaji aligusia ubora wa elimu inayotolewa na shule hizi kwa kuanglia ubora wa waalimu
wanaofundisha katika shule hizi- maarufu kama walimu wa yebo-yebo au Vodafaster kwa sababu ya maandalizi yao ya haraka haraka. Pili aligusi juu ya upatikanaji wa vitabu na dhaan zingine za kujifunzia, pamoja na mazingira ambapo shule hizi zinapatikana.
Je shule hizi za kata zinaweza kuleta maendeleo ya elimu yalikusudiwa? Wadau mnaonaje? Nini kifanyike kuboresha mazingira ya elimu katika shule hizi za kata?

1 comment:

Anonymous said...

Kwanza napenda wapongeza kwa umakini wenu na mirejesho mnayotupa kupitia glob yetu ya GDSS.Pia nashukuru kwa kuuweka mchangowangu kama nilivyochangia.
Ila inatakiwa hamasa iongezeke zaidi kwa wana-GDSS kuupitia mtandao wetu huu ili kuwaunga mkono kwa kazi yenu nzuri mnayofanya.
Hashim S.Luanda,GDSS MEMBER.