Friday, September 5, 2008

Michango iliyojitokeza katika Uzinduzi wa Kitabu cha Hali Halisi ya Jinsia Tanzania

Kaka Badi Darusi (Pichani) alichangia juu ya afya ya uzazi, na aligusia juu ya kulega-kulega kwa hali ya utoaji wa huduma hii kwa wazazi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya akina mama hapa Tanzania. Mchangiaji alitolea mfano Hospitali ya Mwananyamala kwa kuhusika mara kwa mara kwa vifo vya wazazi na kutaka hali hii ikomeshwe na serikali kwani ni jambo ambalo kama serikali ikiamua kulitatua inaweza kufanya hivyo.
Wadau mnasamaje juu ya ubora wa afya ya uzazi? Ipo juhudi yoyote ambayo serikali imeonyesha katika kuboresha hali hii? Je Wanaharakati wanaweza kufanya nini ili kuleta mabadiliko na kuboresha hali hii?

No comments: