Thursday, September 25, 2008

Maandamano ya Kulaani Mauaji ya Maalbino.

Muda sasa umepita tangu wimbi la mauaji ya Maalbino liaanze kutokea hapa kwetu Tanzania kwa Imani za kishirikina za kupata utajiri, karibu Maalbino 30 wameshapoteza maisha. Tayari serikali imetangaza adhabu kali kwa wahusika endapo watakamatwa, mpaka sasa wahusika hawajatiwa mbaroni na kusababisha ndugu zetu albino kuishi kwa hali ya wasiwasi kwani mauaji yanaendelea kwa kasi kubwa. Soma zaidi kuhusu mauaji ya Malbino yanayoendelea.

Chama cha Maalbino Tanzania kwa kushirikiana na Wanaharakati wameandaa Maandamano ya kulaani vitendo hivyo na kuikumbusha serikali kwamba inapaswa kukemea na kuchukulia uzito Jambo hilo. Maandamano hayo yataanzia katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) na kuishia katika Viwanja vya Jangwani, yatafanyika tarehe 18/10/2008 na yanatarajiwa kuhudhuriwa na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu na wapenda amani kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Wanaharakati na Wapenda Amani Wote Mnakaribishwa katika Maaandano haya ya Kupinga Ukatili Wanaofanyiwa Ndugu Zetu Maalbino.

.

No comments: