Friday, October 7, 2011

Mhudumu Mmoja Alazimika Kuhudumia Vijiji Sita

UPUNGUFU, wa watumishi wa afya katika kata ya Endamilai iliyopo
wilayani Mbulu umesababisha mhudumu mmoja kuhudumia wagonjwa wanaotoka vijiji sita vya kata hiyo ambapo wananchi wa eneo hilo hawapati huduma zao za matibabu kama inavyotakiwa hali inayopelekea akina mama kujifungulia njiani huku wakiofia kuatarisha maisha yao.

Akiongea na wanahabari diwani wa kata hiyo bw Gesso Bajuta alisema kuwa
kata hiyo inakabiliwa na wahudumu wa afya pamoja na wataalam wa idara
ya kilimo na ufugaji hali inayosababisha kurudi nyuma kwa maendeleo
ya kata hiyo, Alisema kuwa kata hiyo ina zahanati moja ambayo inategemewa kutoa huduma za afya kwa vijiji sita ambapo ina mhudumu mmoja tu
anayehudumia vijiji vyote hivyo hali inayompelekea kushindwa kuttoa
huduma kwa wagonjwa wote pindi wafikapo hospitalini.

"Zahanati iliyopo katika kata yangu ni moja tu na inategemewa na
vijiji sita na mhudmumu ni mmoja na wako wahudumu ambao
walibadilishana vituo vya kazi lakini hadi sasa hawajafika katika
kituo hicho sasa wanawake ndio wanapata shida sana hasa wakati a
kujifungua hivyo hili swala lichukuliwe hatua za haraka "alisema
Bajuta.


Mbali na hilo alisema kuwa kata hiyo bado inakabiliwa na wataalamu wa
idara ya kilimo na mifugo ambapo kutokana na upungufu huo uendeshwaji
wa kata unakuwa mgumu kwa kuwa hakuna wataalamu hao wa kuwahudumia
Bw Gesso alieleza kuwa imefika mahali wakazi wa eneo hilo wanashindwa
kutumia upandaji bora wa mbegu zinazotolewa pamoja na kujikita zaidi
katika ufugaji wa kilimo kwa kuwa hakuna wataalamu wanaowaelekeza
jinsi ya kuzitumia na namna ya kufuga ufugaji bora .

Hata hivyo aliitaka halimashauri hiyo kuhakikisha kuwa inachukua hatua
za haraka za ili kuweza kutatua matatizo yanayoikabili kata hiyo
ambapo kutokana na upungufu wa wataalamu hao umerudisha maendeleo ya
wananchi nyuma

Na Gladness Mushi, Mbulu

No comments: