Mkurugenzi Mtendaji wa WFT Mary Rusimbi akichangia mada |
Washiriki wa Kongamano la masuala ya Haki za Wanawake na Katiba Tanzania lililoandaliwa na Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT) |
Washiriki wakifahamiana wakati wa Mapumziko |
WANAWAKE kutoka mikoa yote
nchini wamepata fursa ya kushiriki Kongamano la kwanza la Kitaifa la
wanawake kujadili masuala muhimu ya haki za wanawake wanazotaka ziingie kwenye
Katiba mpya.
Kongamano hilo liloandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), linafanyika kwa siku tatu kuanzia 22-24 Oktoba 2012 katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, ambapo watajadili kwa kina na kuchambua mapungufu ya katiba inayotumika hivi sasa na kuwekeana maazimio ya masuala yatakayotakiwa kuingizwa kwenye maudhui ya Katiba mpya inayotarajiwa kuanza kukamilika ifikapo 2014.
Pamoja na mambo mengine,
mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo ni Umuhimu wa katiba katika maendeleo
ya wanawake, mapungufu ya Kijinsia Katika Katiba iliyopo, haki za msingi za
mwanamke za kuzingatia Katika katiba mpya, masuala muhimu ya kuzingatia katika
haki za wanawake na kuwekeana mikakati ya kutumia vizuri fursa ya
mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.
1 comment:
Ni vyema sana wanawake wakifundishwa na kushirikishwa katika katiba ya nchi. Wanawake wasipoendelea nchi nzima haiwezi kuendelea
Post a Comment