Tuesday, October 23, 2012

Wanawake wapigwa msasa kuhusu katiba mpya

Mkurugenzi Mtendaji wa WFT Mary Rusimbi akichangia mada

Washiriki wa Kongamano la masuala ya Haki za Wanawake  na Katiba  Tanzania lililoandaliwa na Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT)

Washiriki wakifahamiana wakati wa Mapumziko
WANAWAKE kutoka mikoa yote nchini  wamepata fursa ya kushiriki Kongamano la kwanza la Kitaifa la wanawake kujadili masuala muhimu ya haki za wanawake wanazotaka ziingie kwenye Katiba mpya.

Kongamano hilo liloandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), linafanyika kwa siku tatu kuanzia  22-24 Oktoba 2012 katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, ambapo watajadili kwa kina na kuchambua mapungufu ya katiba inayotumika hivi sasa na kuwekeana maazimio ya  masuala yatakayotakiwa kuingizwa kwenye maudhui ya Katiba mpya inayotarajiwa kuanza kukamilika ifikapo 2014.


Pamoja na mambo mengine,  mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo ni Umuhimu wa katiba katika maendeleo ya wanawake, mapungufu ya Kijinsia Katika Katiba iliyopo, haki za msingi za mwanamke za kuzingatia Katika katiba mpya, masuala muhimu ya kuzingatia katika haki za wanawake na kuwekeana mikakati  ya kutumia vizuri  fursa ya mchakato  wa uundwaji wa katiba mpya.

1 comment:

seo company singapore said...

Ni vyema sana wanawake wakifundishwa na kushirikishwa katika katiba ya nchi. Wanawake wasipoendelea nchi nzima haiwezi kuendelea