Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali
kupitia Wizara ya Afya inaendelea na mikakati ya kuandaa muswada wa
Baraza la Ustawi wa Jamii Tanzania, litakalokuwa ndio msimmizi wa
masuala yote ya ustawi wa jamii nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano
lililoandaliwa na Chama Cha Wanataaluma wa Ustawi wa Jamii Tanzania
(TASWO) kwa kushirikiana na Muungano wa Taasisi za Kiafya kutoka
Marekani (AIHA), Dk. Mwinyi alisema kuwa kutokana na kutokuwepo kwa
sheria na kanuni za kuongoza chama hicho, kunapelekea chama kukosa
mazingira mazuri ya utendaji kazi.
Aidha, alisema uhaba wa maafisa wa usatawi wa jamii ni changamoto, hivyo
Wizara yake itashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), kutoa elimu pamoja na ajira ili
kukabiliana na changamoto hiyo.
Waziri Mwinyi pia alizindua tovuti ya TASWO ambayo inahusu taarifa za wanachama na chama hicho.
Longamano hilo lililohudhuriwa na maofisa ustawi wa Jamii kutoka ndani na nje ya nchi ili kupeana uzoefu pamoja na taaluma.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment