Thursday, October 25, 2012

MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SSRA WAOTA MBAWA,WAFANYAKAZI WALIOACHA KAZI AU KUACHISHWA KAZI KUENDELEA KUTESEKA



Hatimaye  msimamo wa serikali juu ya kupeleka marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii leo umeota mbawa baada ya kuthibitishwa mbele ya kamati ya kudumu ya maendeleo ya jamii ya Bunge iliyokutana na katika ukumbi wa wizara ya maendeleo ya jamii mjini Dar es salaam kwamba wizara ya kazi na ajira haijaandaa muswada huo. Akithibitisha juu ya swala hilo wakati akitoa maelezo ya wizara mbele ya kamati,katibu mkuu wa wizara hiyo ndugu shitindi amedai kwamba wizara imejipanga kupeleka miscellaneous amendments kwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Katika amendments hiyo katibu mkuu amesema kwamba kifungu kitakachorekebishwa ni kile Na.44 cha sheria ya PPF ambacho ndo pekee kitaruhusu wanachama wa PPF kuchukua mafao yao.Wanachama wa mifuko mingine kama NSSF fao la kujitoa halitarudishwa katika sheria hivyo kubaki wakisubiri miaka 55 au 60 kuchukua mafao yao.Katika mjadala huo hoja mbalimbali zilijitokeza,mojawapo ni ile iliyoibuliwa na bwana Benjamin Dotto.

Akitoa mchango wake bwana Dotto alitaka kujua kwa nini wizara imekaidi kutekeleza mapendekezo ya bunge la nane,ambalo kupitia kwa mbunge Jaffo liliitaka wizara kurudisha fao la kujitoa kwa wafanyakazi wanaoacha au kuachishwa kazi wakati mchakato wa marekebisho ya sheria ukiendelea.Lakini vilevile alitaka kujua kwa nini wizara imekaidi kuandaa muswada wa sheria badala yake unaleta miscellaneous ammendments.

Akiwasilisha mapendekezo ya wafanyakazi mbele ya kamati,Dotto alisema kwamba rasilimali zote na fedha zilizoko kwenye mifuko ni mali ya wanachama wa mifuko hii.Kwa hiyo ili pesa hizi ziweze kulindwa na kukaa salama,wakati umefika uendeshaji wa mifuko hii usimamiwe na wanachama wenyewe.Hivyo akapendekeza mwenyekiti wa mamlaka ya SSRA,na wenyeviti wa mifuko mingine wasiteuliwe na rais bali wachaguliwe na wanachama wa mifuko ili wakienda kinyume waweze kuwajibishwa na wanachama wenyewe.pendekezo hili lilipingwa vikali na Mustafa mkulo na wabunge wengine kwa sababu linainyima serikali nafasi ya kuteua wenyeviti hao.

Akifafanua Dotto alisema kwamba lengo kubwa la pendekezo hilo ni kuiondolea serikali mamlaka ya kutumia fedha za wanachama jinsi wanavyotaka wao,kwa mfano ujenzi wa Udom,Daraja la kigamboni na njia za mabasi yaendayo kasi ni miradi inayotumia pesa za wanachama kwa sababu wasimamizi wa mifuko hiyo ni wateule wa rais.Kauli hiyo ilimsababishia kasheshe bwana dotto kwani alizuiliwa kuendelea kutoa mapendekezo mengine maana yalionekana kugusa masilahi ya wakubwa.

Hata hivyo baadhi ya mapendekezo aliyozuiliwa kuyataja na kufafanua mbele ya kamati ni pamoja na;

1. FAIDA INAYOPATIKANA KUTOKANA NA UWEKEZAJI WA MIFUKO HIYO IGAWIWE KWA KILA MWANACHAMA KILA MWISHO WA HESABU ZA MWAKA KWA KUWEKWA KATIKA AKAUNTI YA MWANACHAMA.

2. MWANACHAMA ARUHUSIWE KUHAMA MFUKO MMOJA KWENDA MWINGINE KWA KUHAMA NA MAFAO YAKE FAIDA NA HAKI ZINGINE.

3.MFANYAKAZI AKIACHA AU KUACHISHWA KAZI MAFAO YAKE YALIPWE NDANI YA SIKU SABA.

4. KUWEPO NA MIKOPO YA WANACHAMA NA WARUHUSIWE KUCHUKUA HADI NUSU YA MAFAO YAO,DHAMANA YA MKOPO IWE MAFAO YAKE YALIYO KATIKA MFUKO.

Kwa ufupi hayo ndo baadhi ya mambo yaliyojiri.ANGALIZO wafanyakazi bado tuna safari ndefu sana kuweza kufika kwenye nchi ya ahadi na bila MSHIKAMANO DAIMA tutabaki kutendwa na kugeuzwa na serikali kama mafungu ya nyanya kama hali halisi ilivyojidhihirisha leo.

Naomba kuwasilisha.
Mchango wa John Mnyika (Mbunge wa Ubungo)

No comments: