UJUMBE WA LEO: Jukumu la kuwatunza wanaoishi na VVU nyumbani ni letu sote, na sio la watoto, wanawake na wazee wa kike peke yao.
Jamii: Ina wajibu wa kusaidia kwa hali na mali kaya zinazotunza wagonjwa wa VVU nyumbani.
Serikali za Mitaa: Zina wajibu wa kuhakikisha huduma zote muhimu, kama elimu ya msingi ya utunzaji wa wagonjwa wa VVU, zahanati, maji n.k. zinapatikana ili kurahisisha utunzaji wa wagonjwa wa VVU nyumbani.
Serikali Kuu: Ina wajibu wa kutoa na kufuatilia matumizi ya rasilimali zinazoelekezwa kwenye Serikali za Mitaa, ili kusaidia utunzaji wa wagonjwa wa VVU nyumbani.
1 comment:
serikali isijifanye "kuuchuna" kuhusu hiki kilio cha wanaharakati na wananchi waliotambua tangu awali kwamba mfumo huu mpya wanaouanzisha utaleta madhara kwa wananchi maskini na ambao ndio wengi, wito kwa wanaharakati wazidishe mapambano ili serikali itoe ruzuku zaidi kwa wagonjwa walio majumbani.... mdau
Post a Comment