Wednesday, July 1, 2009

HITMA ZA KUMUOMBEA PROFESA HAROUB OTHMAN KUSOMWA DAR KESHO


Marehemu Profesa Haroub Othman

HITMA MBILI KUMUOMBEA MAREHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN ALIYEFARIKI MAJUZI NA KUZIKWA HUKO ZANZIBAR ZITAFANYIKA KATIKA MISIKITI MIWILI TOFAUTI JIJINI DAR KESHO ALHAMISI. NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI MNAALIKWA KUHUDHURIA.

KWA MUJIBU WA MWANA WA MAREHEMU, TAHIR OTHMAN, HITMA YA KWANZA ITAFANYIKA KESHO ALHAMISI SAA KUMI NA MOJA JIONI KATIKA MSIKITI WA NGAZIJA ULIOPO MTAA WA MAKJUNGANYA KATIKATI YA JIJI LA DAR.

TAHIR AMESEMA HITMA INGINE ITAFANYIKA HIYO HIYO KESHO ALHAMISI BAADA YA SALA YA I'SHA (BAADA YA SAA MBILI USIKU) KATIKA MSIKITI WA MASJID MA'AMOUR ULIOPO UPANGA JIJINI DAR.

FAMILIA YA MAREHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN INATOA SHUKRANI NYINGI SANA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA MSAADA MKUBWA MLIOTOA WAKATI HUU WA MAJONZI.

NI VIGUMU KUMSHUKURU MMOJA MMOJA NA SI RAHISI KUFANYA AMA KUSEMA LOLOTE ZAIDI YA KUMUOMBA MOLA AWAONGEZEE, MAANA YEYE NDIYE MPANGAJI WA YOTE.

1 comment:

Anonymous said...

Nashauri marafiki wote wa Marehemu wafanye mkutano wa kumkumbuka (memorial)utakaohudhuriwa na watu wa kila dini na madhehebu

Ben Barka