Tuesday, February 24, 2009

Mtoto wa miaka 10 apewa ujauzito Kenya


Mtoto huyu mwenye umri wa miaka 10 amepewa ujauzito hivyo ameharibiwa maisha yake kwani hataweza kuendelea na masomo kwa kipindi kirefu akimlea mtoto wake. Hii ni sawa jamani?

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sasa atasoma shule mpya ya kujifunza namna ya kulea watoto. atakuwa mama bora na hii ni changamoto nzuri kwani kuna maswali juu ya kuoza wasichana, ili waanze kulea mapema, au waende shule zisizokuwa na walimu, wala vifaa vya kufundishia na kukaa huko miaka kibao, harafu waje kupata mimba zisizo na baba.

sisi ni wazuri wa kuongea lakini wagumu wa kutenda. niwaonapo mabinti wanaosoma na waliomaliza sekondari kijijini kwetu, wako nyuma kuliko waliooloewa na sasa wanaitwa mama, mke, shemeji, wanalea familia zao vyema,kuliko huyu aliyetanga tanga shule miaka kibao, harafu hajui kusoma, kuandika, na wala hana muelekeo au kapata elimu isiyoweza kumsaidia lolote maishani.

imekaaje hiyo??

Anonymous said...

tusilete mzaha katika jambo hili,
huyu mtoto hajatendewa haki kabisa kuzalishwa katika umri mdogo kama huo. kwanza huo ni unyama kabisa, sidhani kwamba mtu nmwenye akii timamu na ubinadamu anaweza kumzalisha mtoto mdogo kama huyo. hainiingii akilini kama huyo mtoto aliridhia kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi. kwa umri wake yawezekana hakuwa na uelewa wa kilichokuwa kinaendelea. nani ajuaye, labda alibakwa, au alitishiwa! kwa umri wake ni rahisi hata kutishiwa paka! ni vyema unyama huo usifumbiwe macho, manake aliyetenda anaweza kuendelea kutenda unyama kama huo kwa wengine.