Washiriki walieleza madhara ya utumiaji wa pombe kupita kiasi katika ngazi ya mtu binafsi, familia, na jamii. Katika ngazi ya mtu binafsi ni pamoja na: magonjwa ya ini, macho, kifua kikuu, upungufu wa nguvu za kiume/kike, umasikini, na kushindwa kufikiri sawasawa.
Katika ngazi ya familia madhara ni pamoja na; mlevi kushindwa kutunza familia na kumuachia mama mzigo wote, watoto kukosa malezi ya baba na kusababisha mmonyoko wa maadili, Umasikini, na ubakaji ndani ya ndoa. Katika ngazi ya kijamii walevi wamshindwa kuchangia ujuzi wao katika kuleta maendeleo kwa sababu muda mwingi wanakuwa wamelewa ama wagonjwa kutokana na ulevi kupindukia. Pia ulevi ni chanzo cha ubakaji wa wanawake. Taifa pia limekuwa likipata hasara kwa; kuwatibia wananchi wanaodhurika na pombe, na njaa za mara kwa mara zinazotokana na utumiaji mbaya wa nafaka kwa ajili ya utengenezaji wa pombe.
Je, wanaharakati wamefanya nini kuhakikisha utumiaji wa pombe kupita kiasi hauendelei kuleta madhara kwa wanawake?
2 comments:
Ahsante kwa taarifa nzuri. Nadhani ni muhimu kutambua vile vile kwamba wanawake wengi wanatengeneza na kuuza pombe ikiwa vijijini au mijini -- ni mradi wa uchumi kwa wengi katika hali ambayo hakuna miradi mbadala mingi zaidi .. kwa hiyo muhimu kutafakari pamoja mikakati ya kuongeza aina ya shughuli ya kiuchumi kwa ajili ya wanawake hasa wasiwe na uwezo mkubwa.
Hata kiafya kama Baba ni mlevi na mama ni mlevi wakizaa mtoto huwa ana mapungufu ya kiakili hawi sawa kama mtoto aliyezaliwa na wasiokunywa pombe hadi akue akifikia umrifulanindipo anapokuwa na akili timamuyaani akishapata kinga zake za kujitegemea.
SAFINA HUSSENI
Shirikisho Msanii Afrika.
Post a Comment