Tuesday, November 6, 2012

TANZIA


MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP) unasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi na Mwanaharakati mwenzao Ndg. Claudian Ndayi kilichotokea jana siku ya Jumatatu usiku tarehe 05/11/2012 katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam. 

Mipango ya Mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu Kigamboni - Kibada jijini Dar es Salaam na Sengerema - Mwanza. Marehemu aliyekuwa mwajiriwa wa Idara ya Fedha na Utawala (TGNP) ameacha Mjane na Watoto wawili.

Habari ziwafikie Wanaharakati wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

  Bwana Ametoa
Bwana Ametwaa

Jina lake Lihimidiwe.

Raha ya milele Umpe eeBwana Na Mwanga wa milele Umwangazie, apumzike Kwa Amani. 


Amina!

No comments: