Mtandao wa Jinsia Tanzania
[TGNP] kwa kushirikiana na Mitandao ya Wanaharakati wa Masuala ya Jinsia, Haki
za Binadamu na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi wanawaletea Tamasha la 2 la Jinsia
katika ngazi ya Wilaya.
MADA KUU Ya mwaka huu ni:
Haki ya Uchumi: Ni Suala la Kikatiba , Rasilimali
Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni
Tamasha hili
litafanyika Morogoro Vijijini, Mkoa wa Morogoro katika viwanja vya Moseka
vilivyoko Mkambarani nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Kuanzia
Tarehe 21-23 Novemba
2012 , SAA 3 ASUBUHI HADI – SAA
10 JIONI
Ushiriki
ni wa wazi kwa watu binafsi, vikundi,
taasisi, mashirika na mitandao mbalimbali. Unaweza
kushiriki kwa njia ya kutoa burudani – ngoma, nyimbo maigizo, mashairi, visa
mkasa, maonesho, kuandika na kuwasilisha mada kwa njia mbalimbali,kualika na kufadhili
ushiriki wa watu wengine.
Kwa
mawasiliano zaidi wasiliana na Waratibu wa Tamasha
Simu
0754 362373 au 0754 613082 au andika barua pepe anna.sangai@tgnp.org, festa.andrew@tgnp.org
Wanawake,
Shika Hatamu , Leta Mabadiliko!
WOTE
MNAKARIBISHWA!
No comments:
Post a Comment