Malawi
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.
Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya
kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa
rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo
biashara ya ukahaba inaharamishwa.
“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo
yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana
na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya
uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu,
Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao
50 ambao ni makahaba.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.
Miaka mitatu iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na
Polisi na kulazimishw akupimwa Virusi vua Ukimwi (VVU) na wote kukutwa
wakiwa wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani kwa kufanya biashara
ya ngono huku wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza, ambapo
walichajiwa Dola7 kila mmoja na kuachiwa huru.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.
Wataalamu wa afya nchini humo wanasema maambukizi
ya Ukimwi miongoni mwa makahaba hao yanafikia asilimia 70. Mawakili wao
wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha
kuepuka maambukizi hayo.
No comments:
Post a Comment