SHERIA ya kukataza ndoa za jinsia moja nchini Malawi imesitishwa kwa muda mpaka hapo uamuzi utakapotolewa na Serikali.
Serikali
ililiagiza jeshi la polisi kutowakamata watu wanaojihusisha na ndoa za
jinsia moja , mpaka hapo uamuzi utakapotolewa rasmi na Serikali.
Awali
Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa
kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.
Baadhi ya viongozi wa kimagharibi walitishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga.
Ushoga
ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete
katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.
Mmoja
wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, Kaomba, aliiomba
serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni
kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.
Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.
Kesi
hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata
kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa
pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Rais
wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa
misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili
,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.
Hata hivyo Rais
Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka
kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment