RAIS wa Libya Muammar Gadaffi, amesema, wakoloni walioitawaka Afrika waliiba rasilimali na malighafi hivyo bara hili linastahili fidia ya dola za Marekani trilioni 7.7.
“Umefika wakati kwa nchi za Afrika kulipwa fidia kutokana na wingi la rasilimali zake kuibiwa katika miongo mingi iliyopita wakati wa utumwa na utawala wa kikoloni,” amesema Gadaffi leo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.
Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Afrika (AU) amezikosoa nchi tajiri duniani zinazoendele kutawala kwa mbinu mbalimbali.
Amesema, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Urusi zina nguvu kubwa na mamlaka dhidi ya mataifa zaidi ya 190.
“Wanachama wote wa UN wanatakiwa kuwa sawa, lakini kuna baadhi ya nchi zimejitwalia kinachoitwa nguvu na kutawala nchi zingine,” amesema.
Gadaffi amesema, yanahitajika mabadiliko UN yakiwemo ya mfumo ili kubadilisha tabia ya baadhi ya nchi kuwa na haki ya kutawala na kuzionea nchi nyingine.
Kiongozi huyo ametaka kuwe na demokrasia katika Baraza la Usalama la U, N na kwamba, Afrika inastahili kuwa na angalau kiti ndani ya baraza hilo.
Ameshauri Makao Makuu ya UN yahamishwe kutoka New York, yawe katika eneo ambalo ni la katikati kama vile Geneva, Uswisi.
“Kwa nini baadhi ya wajumbe walazimike kusafiri kwa zaidi ya saa 20 kwenda Makao Makuu. Wakifika hapa wanakuwa wamechoka hata kufanyakazi na wanaishia kulala badala ya kuchangia majadiliano,” amesema Gadaffi.
Awali, Rais wa Brazil Louis Ignacio Da Silva, alitaka kuwapo kwa ushirikiano wa uchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya sawa katika maeneo yote duniani.
Amesema,UN inahitaji mfumo mpya iweze kukabiliana na changamoto za karne ya 21 katika maeneo ya uchumi, siasa, na kijamii.
4 comments:
Ujumbe huo alio utoa mheshimiwa Gadaffi ni sahihi na nadhani viongozi wa Afrika wamechelewa kusema ndio maana nchi tajiri bado wanabuni mbinu uchwara za kuliibia bara la Afrika kwa kisingizio cha uwekezaji.Mnyonyaji hana kabila,dini wala rangi hivyo wahusika wakae macho kwani wale waporaji walio liibia bara la Afrika wapo palepale na wanaendelea na mbinu mbalimbali za kuliibia bara la Afrika.
Nampa hongera zote kiongozi huyo ambaye mwandishi ameseme awafyatukia hao matajiri,nampa tena hongera mheshimiwa kwa kuwapasha na hiyo iwe kweli walipe kwani waliwaiba hata watu wenye akili na kuwapeleka kuwafanyiza kazi kwao ikiwa ni pamoja na wale Waarabu waliokuwa wakiwakamata Waafrika na wao pia wawalipe Waafrika fidia ya hizohizo trioni.
John

Nampongeza sana Rais Gadaffi,wazo lake ni la msingi sana tena limechelewa sana kutolewa.wakoloni walituibia rasilimali zetu kutoka Afrika kwa wingi mno,naomba UMOJA WA AFRIKA kwa nguvu moja umuunge mkono Rais Gadaffi ili masilahi ya waafrika na haki yote ya Afrika iweze kupatikana. Big up Gadaffi
Gaddafi uko sawa kabisa.
Post a Comment