Thursday, May 15, 2014

Wanaharakati Dar waandamana kulaani utekaji wasichana Nigeria



Wasichana wakiwa na mabango kudai kurudishwa kwa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na Boko Haram


maandamano yakielekea viwanja vya Jinsia TGNP mabibo kwaajili ya kusomwa kwa tamko la kuda wasichana warudishwe kuendelea na shule

pamoja na wasichana wa sekondari pia walikuwepo wanaharakati mbalimbali wa haki za wanawake na watoto

Bring our girls home, ndio ulikuwa wimbo wa maandamano

waandamanji wanapokelewa na Wakurugenzi wa mashirika yaliyoandaa maandamano hayo

waandamanaji wakionesha mabango mbalimbali wakati wakipokelewa

Wakurugenzi wa mashirika hayo wakipokea maandamano tayari

washiriki walivyokuwa

wanafunzi wakihakikisha mabango yao yanasomwa na kila mmoja aliyekuwepo

we want our girls back

Na Mwandishi wetu
Wanaharakati kutoka asasi za kiraia zinazotetea Haki za wanawake na watoto nchini Tanzania wamefanya maandamano ya amani kupinga kitendo cha kuwateka na kuendelea kuwashikilia wasichana wa shule zaidi ya 200 waliotekwa na kundi la Boko Haram nchini Nigeria.

Maandamano hayo ambayo awali yalitangazwa kuwa yangeanzia katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo na kuelekea katika kanisa la Mt. Petro Osterbay na kumalizikia katika ofisi za Ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania eneo la Masaki jijini Dar es salaam na kutoa tamko lao kuhusu udhalimu unaofanywa dhidi ya watoto wa kike waliotekwa na kikundi cha Boko Haram nchini Nigeria.

Kutokana na jeshi la Polisi kushindwa kutoa kibali kwa wanharakati hao kuandamana kwa amani kuekelea ubalozi wa Nigeria kupeleka barua yao, walikubaliana kukutana katika viwanja vya TGNP Mabibo, na kufanya maandamano ya kuzunguka ndani ya eneo hilo na kutoa tamko  huku jeshi la Polisi likiweka ulinzi mkali ndani na nje ya eneo hilo.

Akisoma tamko hilo,  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, alisema kuwa mashirika hayo yameamua kuunganisha nguvu kuchukua hatua hiyo baada ya kuona wasichana hao wanaendelea kuteseka wakiwa chini ya watekaji bila mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka.

Sisi, Mtandao wa mashirika huru ya kijamii (CSOs) nchini Tanzania tunaotetea haki za wanawake na watoto tunaungana na mitandao na wanaharakati wengine duniani kote  kulaani kitendo cha kinyama cha kuwateka nyara wasichana wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa shuleni nchini Nigeria, tukio lililofanywa na wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram” alisema Liundi.

Aliongeza kuwa kwa pamoja wanakitaka kikundi cha Boko Haram  kuwaachia mara moja watoto hao na kuwarudisha haraka majumbani kwao.  “Kama wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake na wasichana tunaitaka serikali ya Nigeria kuchukua hatua zote muhimu zinazotakiwa ili kuokoa maisha ya wasichana hao wasio na hatia, na kuwahakikishia haki yao ya msingi ya kupata elimu na kutembea kwa uhuru bila vitisho” aliongeza.

Barua hiyo aliyoandikwa na mashirika yapatayo 14  yanayotetea haki za wanawake na watoto  iliitaka pia serikali ya Nigeria kuzingatia na kutekeleza tamko la Umoja wa Mataifa la haki za watoto (United Nations Convention on the Rights of the Child (CRC) ambalo liliridhiwa na Tanzania mwaka 1989 na Nigeria mwaka 2003.

Barua hiyo iliyosainiwa na wakurugenzi wa mashirika ya WILAC, TAMWA, TGNP Mtandao, WiLDAF, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), TWCWC, CWCA, Jukwaa la Wabunge Wanawake Tanzania, Jukwaa la Katiba Tanzania, Jukwaa la Wanawake na Katiba Tanzania, Asasi ya Jinsia na Vyombo vya Habari Tanzania (GEMSAT), African Life Foundation, Mtandao wa Wasanii Tanzania, (Binti Leo),Women Assistance and Development (WADE) imepelekwa nakala kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, na  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto,Sophia Simba. Inapatikana www.gdss2008.blogspot.com

No comments: