Monday, May 26, 2014

TGNP MTANDAO WAKUTANA NA KAMATI ZA BUNGE DODOMA

TGNP Mtandao wamekutana na kamati za Bunge Mjini Dodoma katika warsha ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi ya Hazina ndogo ililenga kuwawezesha Wabunge zaidi ya 100 kushiriki katika kuhakikisha bajeti inayotungwa na serikali inakuwa ya mrengo wa kijinsia.

pia wabunge waweze kutambua masuala yanayowakabili wanawake na makundi yaliyoko pembezoni na kudai yaingizwe kwenye bajeti ikiwemo kutengewa fedha. Aidha ni kuwaongezea watunga sera hao uelewa  kuhusu Tamko la bajeti ya kijinsia (Gender Budget Statement) na matumizi yake kama nyenzo ya kufanikisha  malengo ya bajeti  yenye mtazamo wa kijinsia.
warsha hiyo iliendeshwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi na wanachama wa TGNP Aseny Muro na Gemma Akilimali ambao walitoa mada na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wabunge hao wakisaidiana na wafanyakazi wa TGNP na Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwakaribisha wabunge kwenye warsha hiyo mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati aliyeteuliwa na washriki, Mhe. Magreth Sita akifuatilia

Mhe. Sita na wabunge wengine

wabunge wakifuatilia mawasilisho

Mbunge wa Ubungo John Mnyika na Hamad Rashid wa WAWI wakifuatilia

Kaimu Mkurugenzi akizungumza

Kaimu Mkurugenzi wakiwa na Mwenyekiti wa Mkutano Mhe. Sitta

mwezeshaji Gemma Akilimali akijaindaa kuwasilisha

wabunge wakifuatilia

mwezeshaji Aseny Muro akizungumza

No comments: