Tuesday, May 13, 2014

TGNP yakinoa kikundi kazi cha Uchambuzi wa bajeti

TGNP Mtandao wameanza kukijengea uwezo kikundi kazi cha uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa Kijinsia (BATT), kinachojihusisha na uchambuzi wa bajeti kila mwaka na mipango ya uchummi na mwelekeo wa bajeti wa serikali.

kikundi hicho ambacho kinawashiurikisha vijana waliobobea kwenye uchambuzi wa kina katika maeneo mbalimbali ya kisekta wanashiriki kuchambua bajaeti za kisekta na ile kubwa ya serikali itakayotangazwa na waziri wa Fedha mwezi Juni mwaka huu.
kila mwaka TGNP Mtandao hukutana na kikundi kazi hiki chenye wajumbe zaidi ya 30 kuwajengea uwezo zaidi wa kiuchambuzi katika maeneo yote muhimu ili waweze kucjhambua bajaeti za kisekta.  aidha mpango wa kujenga uwezo kwa kundi hili unasaidia pia kuhakikisha taifa linakuwa na vijana wengi ambao wana uelewa wa kuchambua bajaeti kila mwaka  kwenye taasisi mbalimbali za kijamii na serikalini.
akizungumzwa kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Meneja wa idara ya ushawishi, utetezi, utafiti na uchambuzi Mary Nsemwa amasema kuwa  kikundi kazi hicho kitapaswa kuelewa muktadha  uliopo  ukihusianaa na uchambuzi.

""katika mkujtano huu wa siku tatu, mtaelewa dhana mbalimbali zinazohusiana na bajeti mbalimbali  kwa mrengo wa kijinsia, kuainisha masuala makuu ya kipaumbele yakihusishwa na matokeo ya uraghibishi uliofanyika katiika  mikoa ya shinyanga, Morogoro, Mbeya na DSM" alisema Mary
aidha washiriki hao kutoka katika taaluma mbalimbali watapata  mafunzo  ya uchambuzi wa  wa bajeti wa mrengo wa kijinsia,  kwa kuzingatia kampeni ya haki ya uchumi rasilimali ziwanufaishe wanawake na wanaume walioko pembezoni kuwa ni suala la Kikatiba.
Pia kupanua wigo wa wachambuzi wa bajeri  kwa mtazamo wa makundi yaliyoko pembezoni( Gender Budgeting Analysis task team).

No comments: