Bunge la Katiba linaahirishwa hii leo kupisha Bunge la Bajeti,
likiwa limetumia gharama ya karibia
billion 27, za walipa kodi kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya. Ndani
ya siku 67 ambayo Bunge hilo limekaa kujadili Rasimu ya pili ya Katiba, haijaweza
kupitisha hata ibara moja, kati ya ibara 240. Swala la kujiuliza ni kwamba, je
hizo siku 60 walizo ongezewa ambazo zitaanza August 5 mwaka huu zitaweza kuzaa
matunda ama wataendelea na malumbano bila kuleta kitu cha maana kwa Watanzania.
Wajumbe walioko ndani ya Bunge la Katiba wanabidi watambue kwamba fedha hizo
wanazozitumia zingeweza kufanyia shughuli nyingi sana za maendeleo kama
kuboresha vituo vya afya, kuongeza vituo vya elimu ama kuboresha miundombinu
yetu. Hivyo, wanapaswa kutumia muda waliopewa kuujadili na kupitisha rasimu
zote 240, bila ya kuongezewa muda zaidi.
No comments:
Post a Comment